Sheria ni mpya na imekuja kuwaumiza zaidi wale wanaofanya transactions za viwango vya chini.
Kutoka kwenye lile jedwali, nimeona watakaoumia ni wale watakaotuma au kutoa kuanzia shilingi 5000/= mpaka 30,000/=
Mfano, kutoka shilingi 10,000/= mpaka 14,999/= wanakata.
Lakini pia, kutoka shilingi 15,000/= mpaka 19,999/= napo wanakata, wamefanya hivi makusudi wakijua watanzania wengi hivi ndivyo viwango vyao vya kutoa na kupokea pesa.
Hali ni tofauti kwa yule atakayetoa mfano kuanzia 100,000 -200,000/= huyu atakatwa mara moja pekee, wamefanya hivi wakijua hawa ni wachache na wanaojiweza.