Serikali yafafanua kauli ya Rais Samia kuhusu Bei za Mafuta

Serikali yafafanua kauli ya Rais Samia kuhusu Bei za Mafuta

Serikali inayodai kuwa bei za Tanzania "ni ndogo ikilinganishwa na nchi zingine" inajaribu kupakua hasira ya wananchi eeh (Genz)

wakati huo huo haitoi mkakati wowote wa kupunguza mzigo kwa wanyonge.
Wananchi hawataki sababu. Wanataka ufumbuzi


huku damu ya vijana wa Oktoba 29 bado haijafutwa. Ni aibu kubwa kusimama kuzungumza masuala ya kiuchumi wakati maelfu ya familia bado zinatafuta miili ya wapendwa wao
😭😭😭😭
 
Serikali kupitia Msemaji Mkuu wake, Gerson Msigwa, imetoa ufafanuzi wa kauli ya Rais Samia aliyotoa mchana wa leo Aprili 8, 2026, kuhusu bei za mafuta;

Soma: Rais Samia: Bei ya mafuta Marekani na Ulaya ni Dola 800 na Euro 400/600 lita 1, Sisi tuko vizuri, tuna uhakika wa miezi 3

UFAFANUZI​

Leo tarehe 08 Aprili, 2026, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akiwaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni amezungumzia changamoto ya kupanda kwa bei za mafuta Duniani.

Kutokana na baadhi ya watu kuhitaji ufafanuzi wa kauli hiyo, Mheshimiwa Rais alimaanisha ifuatavyo;

1. Bei za mafuta ya dizeli katika soko la dunia zimeongezeka kwa dola za Marekani 800 kwa tani ambapo zimetoka dola 650 ya mwezi Februari 2026 hadi kufikia dola 1,450 mwezi Machi 2026.

2. Bei za mafuta ya petroli katika soko la dunia zimeongezeka kwa dola za Marekani 434 kwa tani ambapo zimetoka dola 618 ya mwezi Februari 2026 hadi kufikia dola 1,052 mwezi Machi 2026.

3. Bei za mafuta ya taa na mafuta ya ndege katika soko la dunia zimeongezeka kwa dola za Marekani 821 kwa tani ambapo zimetoka dola 679 ya mwezi Februari 2026 hadi kufikia dola 1,500 mwezi Machi 2026.

Pamoja na kuwepo kwa athari za kupanda kwa bei za mafuta kwa watumiajiu duniani kote, bado viwango vya bei za mafuta vya Tanzania ni vidogo ikilinganishwa na nchi zingine.

Kupanda kwa bei za mafuta kumesababishwa na athari za vita inayoendelea kati ya Irani dhidi ya Israel na Marekani iliyosababisha kufungwa kwa lango la Hormus ambalo hupitisha mafuta mengi yanayotumiwa Tanzania na nchi zingine za Afrika.

Gerson Msigwa
Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Msemaji Mkuu wa Serikali



Pia soma: Hotuba ya Samia kwenye page ya Ikulu imefutwa muda mfupi baada ya kuhutubia
🤣🤣🤣🤣
 
Kwa hio mafuta yanapimwa kwa Gramu, KG au Tani? Inabidi watuchongee mizani kwenye kila sheli zetu tunazonunulia mafuta
Hahahahahaaaa.. Hii nchi me sihami hata iweje.. Bongo kila mtu msanii, hivi unapata wapi ujasiri wa kuwaambia watu zaidi ya milioni 60 kua mafuta yanauzwa kwa tani.!!! Unajua nimesikitika sana leo, lakini basi sina namna ikabidi nibaki nacheka kwa uchungu nikishushia na konyagi hangu taratibu
 
Hahahahahaaaa.. Hii nchi me sihami hata iweje.. Bongo kila mtu msanii, hivi unapata wapi ujasiri wa kuwaambia watu zaidi ya milioni 60 kua mafuta yanauzwa kwa tani.!!! Unajua nimesikitika sana leo, lakini basi sina namna ikabidi nibaki nacheka kwa uchungu nikishushia na konyagi hangu taratibu
Nadhani alitaka manisha metric tonnes
 
Back
Top Bottom