Serikali yafafanua kauli ya Rais Samia kuhusu Bei za Mafuta

Serikali yafafanua kauli ya Rais Samia kuhusu Bei za Mafuta

Mtu ambae hawezi kujua bei ya soko la mafuta duniani yanauzwa bei gani ndo huyu huyu mnasema tuna wivu tukimkosoa au tunamchukia kwasababu ya dini yake ? Hapana IQ ni ndogo na hana EQ kila wanachomletea anameza hawezi kusoma hata kidogo na kukifanyia challenge kitu ambacho analetewa . Wanaofaidika na huu upumbavu miaka hata ipite mingapi vizazi vyenu vitaenda jela tu
 
Serikali kupitia Msemaji Mkuu wake, Gerson Msigwa, imetoa ufafanuzi wa kauli ya Rais Samia aliyotoa mchana wa leo Aprili 8, 2026, kuhusu bei za mafuta;

Soma: Rais Samia: Bei ya mafuta Marekani na Ulaya ni Dola 800 na Euro 400/600 lita 1, Sisi tuko vizuri, tuna uhakika wa miezi 3

UFAFANUZI​

Leo tarehe 08 Aprili, 2026, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akiwaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni amezungumzia changamoto ya kupanda kwa bei za mafuta Duniani.

Kutokana na baadhi ya watu kuhitaji ufafanuzi wa kauli hiyo, Mheshimiwa Rais alimaanisha ifuatavyo;

1. Bei za mafuta ya dizeli katika soko la dunia zimeongezeka kwa dola za Marekani 800 kwa tani ambapo zimetoka dola 650 ya mwezi Februari 2026 hadi kufikia dola 1,450 mwezi Machi 2026.

2. Bei za mafuta ya petroli katika soko la dunia zimeongezeka kwa dola za Marekani 434 kwa tani ambapo zimetoka dola 618 ya mwezi Februari 2026 hadi kufikia dola 1,052 mwezi Machi 2026.

3. Bei za mafuta ya taa na mafuta ya ndege katika soko la dunia zimeongezeka kwa dola za Marekani 821 kwa tani ambapo zimetoka dola 679 ya mwezi Februari 2026 hadi kufikia dola 1,500 mwezi Machi 2026.

Pamoja na kuwepo kwa athari za kupanda kwa bei za mafuta kwa watumiajiu duniani kote, bado viwango vya bei za mafuta vya Tanzania ni vidogo ikilinganishwa na nchi zingine.

Kupanda kwa bei za mafuta kumesababishwa na athari za vita inayoendelea kati ya Irani dhidi ya Israel na Marekani iliyosababisha kufungwa kwa lango la Hormus ambalo hupitisha mafuta mengi yanayotumiwa Tanzania na nchi zingine za Afrika.

Gerson Msigwa
Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Msemaji Mkuu wa Serikali



Pia soma: Hotuba ya Samia kwenye page ya Ikulu imefutwa muda mfupi baada ya kuhutubia
Na tangu lini mafuta huuzwa kwa tani badala ya pipa?🛢️🛢️
 
Hahahahahaaaa.. Hii nchi me sihami hata iweje.. Bongo kila mtu msanii, hivi unapata wapi ujasiri wa kuwaambia watu zaidi ya milioni 60 kua mafuta yanauzwa kwa tani.!!! Unajua nimesikitika sana leo, lakini basi sina namna ikabidi nibaki nacheka kwa uchungu nikishushia na konyagi hangu taratibu
Kwa hio wewe unasemaje ni Tani au Lita? Ni nani kilaza aliesema Tani au aliesema Lita?
 
Hiyo msigwa aliyijaribu kuelezea naamini rais hata yeye haelewi na hawezi kuelewa,laiti angeeleweshwa hivyo angekataa kusema hadharani😁😁😁

Sasa tuwe na maelekezo yetu kuelezea mafuta nfano: Gari yangu inatumia Tani 12 kwa kilometer😁😁😁😁😁 hii nayo kiboko

Mafuta hayanunuliwi kwa ballel yanapigiwa mahesabu kwa Barrel.

Unaponunua in bulk ni tonnes of tonnes na kuna bei za Metric Tonnes ambayo ilikuwa hiyo 800.

Tafuteni elimu kabla ya kulalamika.
 
Back
Top Bottom