Serikali yafafanua kauli ya Rais Samia kuhusu Bei za Mafuta

Serikali yafafanua kauli ya Rais Samia kuhusu Bei za Mafuta

Hata huo unaoitwa ufafanuzi siyo sahihi.

Mtoa hotuba alizungumzia bei inayolipwa na watumiaji wa mafut sehemu husika; siyo bei ya ununuzi katika soko la dunia.
Kwahiyo mkuu kwenye soko la dunia wananunua shingapi kwa tani??
 
Muongo muongo muongo,
Bei za mafuta ghafi huwa zinatolewa kwa pipa, sio kwa tani.
Wananunua kwa tani yaliyochenguliwa hao wachuuzi wanaoleta kwenye soko letu wananchi.
 
Kwahiyo mkuu kwenye soko la dunia wananunua shingapi kwa tani??
Hotuba ya Mhalifu Samia haikulenga bei ya soko la dunia.
Ufafanuzi unazungumzia jambo tofauti na lililolengwa na mtoa hotuba.

Huko duniani Tanzania hainunui bei tofauti na hao wengine tuliolenganishwa nao.

Ufafanuzi ulipaswa ueleze bei ya mitaani kama alivyolenga mtoa hotuba.

Kwa hiyo, huo haukuwa ufafanuzi wa taarifa iliyowasilishwa mwanzo.
 
Waambie wasije wakafuta tu maana hawachelewi kifutafuta wanasema vitu bila uhakika wa kutosha mwisho wanafuta kufichaficha unaficha nini na umetoa boko mbele ya camera eti wanahabari msiende kusema kwamba nimesema wakati hapo upo mbele ya camera inachukua kila kitu live kabisa kudadek hivi anatumia bia gani?
Aliyekuja kuleta ufafanuzi ndio kazidi kuharibu maana amekuja na habari mpya tena za kuchanganya zaidi.
 
Hotuba ya Mhalifu Samia haikulenga bei ya soko la dunia.
Ufafanuzi unazungumzia jambo tofauti na lililolengwa na mtoa hotuba.

Huko duniani Tanzania hainunui bei tofauti na hao wengine tuliolenganishwa nao.

Ufafanuzi ulipaswa ueleze bei ya mitaani kama alivyolenga mtoa hotuba.

Kwa hiyo, huo haukuwa ufafanuzi wa taarifa iliyowasilishwa mwanzo.
Kifupi msigwa kaja na jambo jipya dhahiri zaidi kaonyesha kuwa bosi alichoongea ni uongo yeye kaja na mambo mapya
 
Kwahiyo huyu bwana anataka kusema raisi hajui kusoma, hajui kutofautisha tani na lita!!
Kipimo cha ujazo cha kimiminika ni lita, na ndio rahisi zaidi..
Kumtetea mama kizimkazi unapaswa ujitoe akili mnooi
 
vipimo vya urefu m sm mm dm na nk

Vipimo vya uzito g kg tan

Vpm vya ujazo ml m^3 lita na nk

mbona msigwa anatuchanganya tenaaa
 
Leo tarehe 08 Aprili, 2026, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akiwaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni amezungumzia changamoto ya kupanda kwa bei za mafuta Duniani.
Kuna mtu amewahi kusikia bei za mafuta katika soko la dunia zikitolewa kwa tani? Au ni suala la kujaribu kuhalalisha makosa?

Msione aibu kusema raisi amekosea. Na of course ni ajabu raisi kutojua anakosea kuhusu kitu kama bei ya mafuta, tena mara mbili. Hofu yangu ni kwamba, je alikuwa na tatizo kusoma na kuelewa alichoandikiwa? Sasa kama kusoma bei ya mafuta aliyoandikiwa tu ni shida, hiyo mikataba tunayotia sahihi ana elewa cost implications zake kweli?

Ni jambo hatari sana kwa taifa ikiwa raisi hana ufahamu wa vitu rahisi kama hivi. Yaani mtu anaweza kuja akasema, unajua raisi Samia, bei ya diesel soko la dunia ni Dolla 8000 kwa lita. Basi sie tutawasaidia Watanzania. Tia sahihi huu mkataba ili tuwaletee diesel kwa bei ya Dola 1500 kwa lita! Ila tutafanya hivyo ukitia sahihi haya makubaliano sasa hivi, la sivyo mtakuwa mmepoteza nafasi maana kuna wenzenu wanasubiri mkikataa watie sahihi wao.
 
Mafuta hayanunuliwi kwa ballel yanapigiwa mahesabu kwa Barrel.

Unaponunua in bulk ni tonnes of tonnes na kuna bei za Metric Tonnes ambayo ilikuwa hiyo 800.

Tafuteni elimu kabla ya kulalamika.
Kwa hiyo Ton 1 ni sawa na litres ngap?
 
Serikali kupitia Msemaji Mkuu wake, Gerson Msigwa, imetoa ufafanuzi wa kauli ya Rais Samia aliyotoa mchana wa leo Aprili 8, 2026, kuhusu bei za mafuta;

Soma: Rais Samia: Bei ya mafuta Marekani na Ulaya ni Dola 800 na Euro 400/600 lita 1, Sisi tuko vizuri, tuna uhakika wa miezi 3

UFAFANUZI​

Leo tarehe 08 Aprili, 2026, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akiwaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni amezungumzia changamoto ya kupanda kwa bei za mafuta Duniani.

Kutokana na baadhi ya watu kuhitaji ufafanuzi wa kauli hiyo, Mheshimiwa Rais alimaanisha ifuatavyo;

1. Bei za mafuta ya dizeli katika soko la dunia zimeongezeka kwa dola za Marekani 800 kwa tani ambapo zimetoka dola 650 ya mwezi Februari 2026 hadi kufikia dola 1,450 mwezi Machi 2026.

2. Bei za mafuta ya petroli katika soko la dunia zimeongezeka kwa dola za Marekani 434 kwa tani ambapo zimetoka dola 618 ya mwezi Februari 2026 hadi kufikia dola 1,052 mwezi Machi 2026.

3. Bei za mafuta ya taa na mafuta ya ndege katika soko la dunia zimeongezeka kwa dola za Marekani 821 kwa tani ambapo zimetoka dola 679 ya mwezi Februari 2026 hadi kufikia dola 1,500 mwezi Machi 2026.

Pamoja na kuwepo kwa athari za kupanda kwa bei za mafuta kwa watumiajiu duniani kote, bado viwango vya bei za mafuta vya Tanzania ni vidogo ikilinganishwa na nchi zingine.

Kupanda kwa bei za mafuta kumesababishwa na athari za vita inayoendelea kati ya Irani dhidi ya Israel na Marekani iliyosababisha kufungwa kwa lango la Hormus ambalo hupitisha mafuta mengi yanayotumiwa Tanzania na nchi zingine za Afrika.

Gerson Msigwa
Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Msemaji Mkuu wa Serikali



Pia soma: Hotuba ya Samia kwenye page ya Ikulu imefutwa muda mfupi baada ya kuhutubia
20260409_034839.jpg
 
Back
Top Bottom