Serikali yafafanua kauli ya Rais Samia kuhusu Bei za Mafuta

Serikali yafafanua kauli ya Rais Samia kuhusu Bei za Mafuta

Serikali kupitia Msemaji Mkuu wake, Gerson Msigwa, imetoa ufafanuzi wa kauli ya Rais Samia aliyotoa mchana wa leo Aprili 8, 2026, kuhusu bei za mafuta;

Soma: Rais Samia: Bei ya mafuta Marekani na Ulaya ni Dola 800 na Euro 400/600 lita 1, Sisi tuko vizuri, tuna uhakika wa miezi 3

UFAFANUZI​

Leo tarehe 08 Aprili, 2026, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akiwaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni amezungumzia changamoto ya kupanda kwa bei za mafuta Duniani.

Kutokana na baadhi ya watu kuhitaji ufafanuzi wa kauli hiyo, Mheshimiwa Rais alimaanisha ifuatavyo;

1. Bei za mafuta ya dizeli katika soko la dunia zimeongezeka kwa dola za Marekani 800 kwa tani ambapo zimetoka dola 650 ya mwezi Februari 2026 hadi kufikia dola 1,450 mwezi Machi 2026.

2. Bei za mafuta ya petroli katika soko la dunia zimeongezeka kwa dola za Marekani 434 kwa tani ambapo zimetoka dola 618 ya mwezi Februari 2026 hadi kufikia dola 1,052 mwezi Machi 2026.

3. Bei za mafuta ya taa na mafuta ya ndege katika soko la dunia zimeongezeka kwa dola za Marekani 821 kwa tani ambapo zimetoka dola 679 ya mwezi Februari 2026 hadi kufikia dola 1,500 mwezi Machi 2026.

Pamoja na kuwepo kwa athari za kupanda kwa bei za mafuta kwa watumiajiu duniani kote, bado viwango vya bei za mafuta vya Tanzania ni vidogo ikilinganishwa na nchi zingine.

Kupanda kwa bei za mafuta kumesababishwa na athari za vita inayoendelea kati ya Irani dhidi ya Israel na Marekani iliyosababisha kufungwa kwa lango la Hormus ambalo hupitisha mafuta mengi yanayotumiwa Tanzania na nchi zingine za Afrika.

Gerson Msigwa
Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Msemaji Mkuu wa Serikali



Pia soma: Hotuba ya Samia kwenye page ya Ikulu imefutwa muda mfupi baada ya kuhutubia
Huu sio ufafanuzi,hii ni kijihotuba kipya,yeye alisema 1 liter,halafu mafuta hayauzwi kwa tani,toka lini mafuta yakauzwa kwa tani?
 
Hahaha aah gongo hapana Mzee mimi nakata ngano tu ni mwendo wa bia
Nikipata nafasi ya kuchagua bia na gongo basi amini nitakunywa gongo. Bia hua naitumia kama kichanganyio cha pombe kali, sijawahi kunywa bia tupu nikalewa.
 
Hata huo unaoitwa ufafanuzi siyo sahihi.

Mtoa hotuba alizungumzia bei inayolipwa na watumiaji wa mafut sehemu husika; siyo bei ya ununuzi katika soko la dunia.
 
Metric tone mzee huwezi jua kila kitu.
Haihitaji kujuwa kila kitu kutambua kwamba mlaji wa kawaida mtaani hanunui mafuta kwa viwango vya tani.

Upuuzi huu ndio mmeueneza kila mahali hata watoto mashuleni wanakuwa viazi!

Baada ya huyu Mhalifu Samia, itahitajika kazi kubwa sana kurekebisha viwango kila mahali. Tanzania limekuwa taifa la kipuuzi kabisa katika kila nyanja.
 
Back
Top Bottom