Serikali kupitia kifungu cha 30 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287 kinachotoa ruhusa kwa mamlaka za Serikali kufanya mgawanyo wa Halmshauri za Wilaya;
Imetoa AMRI rasmi iliyotangazwa kwenye Gazeti la Serikali namba 673 la tarehe 02 Agosti, 2024; ili kufuta baadhi ya maeneo ya kiutawala kwenye mamlaka za Serikali za Mitaa hapa nchini kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa tarehe 27 Novemba, 2024.
Amri hii rasmi sasa inafuta Kata, Vijiji na Vitongoji katika Halmashauri za Wilaya zifuatazo; Ngorongoro, Bahi, Chemba, Kasulu, Kakonko, Hai na Rombo.
Katika Halmshauri ya Wilaya ya Ngorongoro pekee, kupitia AMRI hii, Serikali imezifuta Kata 11, Vijiji 25 na Vitongoji 96.
Garatwa,
Dar es Salaam, Tanzania.
20 Agosti, 2024.