Serikali yafuta vijiji na vitongoji vyote vya wamasai wa Ngorongoro kupitia Amri ya tangazo la Serikali namba 673

Serikali yafuta vijiji na vitongoji vyote vya wamasai wa Ngorongoro kupitia Amri ya tangazo la Serikali namba 673

Wewe ni mnafiki mkubwa, umeweka heading ya Ngorongoro as if ndio iliyofutwa pekee, wakati Kasulu, na nyingine hukuziweka hapo juu!!
Serikali kupitia kifungu cha 30 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287 kinachotoa ruhusa kwa mamlaka za Serikali kufanya mgawanyo wa Halmshauri za Wilaya;

Imetoa AMRI rasmi iliyotangazwa kwenye Gazeti la Serikali namba 673 la tarehe 02 Agosti, 2024; ili kufuta baadhi ya maeneo ya kiutawala kwenye mamlaka za Serikali za Mitaa hapa nchini kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa tarehe 27 Novemba, 2024.

Amri hii rasmi sasa inafuta Kata, Vijiji na Vitongoji katika Halmashauri za Wilaya zifuatazo; Ngorongoro, Bahi, Chemba, Kasulu, Kakonko, Hai na Rombo.

Katika Halmshauri ya Wilaya ya Ngorongoro pekee, kupitia AMRI hii, Serikali imezifuta Kata 11, Vijiji 25 na Vitongoji 96.

Garatwa,
Dar es Salaam, Tanzania.
20 Agosti, 2024.
View attachment 3074791
 
Tena hao wamasai washukuru sana wamekutana na uongozi unaobembeleza ilibidi wafukuzwe mara moja. Uharibifu wa hifadhi ni mkubwa mno.
 
“Hatua ya kufuta vijiji na vitongoji ni hatua inayoenda mbali sana. Maana yake ni kwamba wananchi wahusika hawatakuwa na serikali zao za mitaa vijijini na vitongojini. Hii ni kinyume cha ibara ya 145 na 146 ya Katiba ambayo inazungumzia Madaraka ya Umma na kuweka Serikali za Mitaa. Kuwa na madaraka ngazi ya vijiji ni mosi, kuimarisha demokrasia ngazi za chini; pili kuwezesha wananchi waishio vijijini kushiriki katika utawala ambayo ni haki yao kwa mujibu wa ibara 21(1); na tatu, waishio katika eneo hilo kupata haki ya kuchagua na kuchaguliwa katika Halmashauri zao kama wananchi wenzao waishio katika maeneo mengine. Kwa kuwa vijiji vimefutwa wananchi hao watakosa haki hizo. Kwa maneno mengine wamekuwa disenfranchised (Kuporwa haki). Jamani tunaelekea wapi? Nini lengo la kufanya hivyo? Je tuelewe vipi? Tuambiwe waziwazi kama jamii ya Kimaasai waishio Ngorongoro ni wananchi au wakimbizi wa ndani? Prof. Shivji

Maneno ya Mhadhiri Mwandamizi Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Profesa wa Sheria Profesa Issa Shivji kupitia mtandao wake wa X.
20240820_162254.jpg
 
Wewe ni mnafiki mkubwa, umeweka heading ya Ngorongoro as if ndio iliyofutwa pekee, wakati Kasulu, na nyingine hukuziweka hapo juu!!
Wewe umeona hizo wilaya ulizozitaja zimefutwa au mipaka imerekebishwa?
 
Masai kasomeni Sheria ya Ardhi namba 4 ya mwaka 1999. Tatizo mnajazwa upepo na wanasiasa uchwara wasioishi Ngorongoro
Wewe mwenyewe hata huijui hiyo sheria inasema nini zaidi ya kujua kuitamka tu..

Umekaririshwa tu toka huko ulikotoka na kuandika hivi..

Kama kweli unaijua na contextual meaning yake kifungu kwa kifungu, hebu sema inahusu nini na kivipi Wamasai wanahusiana nayo..?
 
“Hatua ya kufuta vijiji na vitongoji ni hatua inayoenda mbali sana. Maana yake ni kwamba wananchi wahusika hawatakuwa na serikali zao za mitaa vijijini na vitongojini. Hii ni kinyume cha ibara ya 145 na 146 ya Katiba ambayo inazungumzia Madaraka ya Umma na kuweka Serikali za Mitaa. Kuwa na madaraka ngazi ya vijiji ni mosi, kuimarisha demokrasia ngazi za chini; pili kuwezesha wananchi waishio vijijini kushiriki katika utawala ambayo ni haki yao kwa mujibu wa ibara 21(1); na tatu, waishio katika eneo hilo kupata haki ya kuchagua na kuchaguliwa katika Halmashauri zao kama wananchi wenzao waishio katika maeneo mengine. Kwa kuwa vijiji vimefutwa wananchi hao watakosa haki hizo. Kwa maneno mengine wamekuwa disenfranchised (Kuporwa haki). Jamani tunaelekea wapi? Nini lengo la kufanya hivyo? Je tuelewe vipi? Tuambiwe waziwazi kama jamii ya Kimaasai waishio Ngorongoro ni wananchi au wakimbizi wa ndani? Prof. Shivji

Maneno ya Mhadhiri Mwandamizi Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Profesa wa Sheria Profesa Issa Shivji kupitia mtandao wake wa X.View attachment 3074956
Msomera mbona pazuri tu
 
Haki inaweza ikatendeka, mkahisi mkiwapa fidia yataisha. Lkni asikudanganye mtu, kuna jamii za watu ziko attached na ardhi walioyotokea, angalia waPalestina na wayaHudi wanavyopambana kisa ardhi. kwa hiyo mimi kwa namna fulani nawaelewa.

Dunia imewafuata wamasai, wamasai hawakuifuata dunia
 
Back
Top Bottom