Serikali yakanusha kuwepo mlipuko wa Ugonjwa wowote kata ya Ifumbo, Mbeya. Wizara ya Afya kuichukulia hatua ITV

Wangedili na huyo Mganga Mkuu wa eneo husika, hao ITV mtawaonea bure.
 
Mheshimiwa diwani ambaye ndiye shahidi namba moja hakuhojiwa
Hta angehojiwa hana ujasiri wa kusema chochote. Hii serikali inaongozwa kwa matashi ya mtu mmoja na mbaya zaidi ana hitalafu fulani upstairs. Kama covid iko wazi na watu wanafariki lakini serikali inakanusha ije kuwa huo ugonjwa ambao uko sehemu moja huko vijijini? Inawezekana hata ikawa ebola lakini mtu mmoja akishasema hakuna iwe siri basi hakuna wa kumbishia.
 
Wala hawakwenda kuchunguza chochote, sana sana utakuta wameishia kwenda kutoa vitisho.
Ile shule ya Moshi ilitoa tamko la kweli na wakatishiwa ikabidi wakanushe hivyo awamu hii tuombe Mungu kusitokea milipuko mingi ya magojwa la sivyo tutaisha´. Ugonjwa kama ebola ukiingia (Mungu pisha mbali) itakuwa maafa. Si ajabu ikatoka amri wanaougua apigwe risasi ili isijulikane.
 
Sema wazi kuwa na wewe ni timu ya kusifu na kumwabudu Jiwe.
 
Wala hawakwenda kuchunguza chochote, sana sana utakuta wameishia kwenda kutoa vitisho.
Sure maana kuna statement ukiitoa inaonyesha unajali na unachukua hatua...mf tumefika eneo la.tukio tumehoji watu kadhaa tumechukua sample za wahonjwa na postmoterm za maiti so tutawaletea mrejesho kama ni ugonjwa ni ugonjwa gani na kama sio ugojwa ni nini....

Hawa wamefika tuu sikuhiyo hiyo vitisho vitusho vitisho.
 
Wazee wa kukanusha...kazi ipo awamu hii
 
Hivi nyie hua mnajua taratibu za kazi,hivi kama dokta amegundua ugonjwa mpya kwa nini hakuwasiliana na wakuu wa kazi,ili wao ndio watutangazie wana inchi kuna mamulaka zina husika na hayo mambo kwa kufuata utaratibu,sio kila mutu tu ameshiba makande anajitokeza kuleta taharuki kwa taifa bila sababu za musingi ote mnaopinga hamjielewi kabisa,hata hao itv wali paswa kuwasiliana na mamulaka ili kujirizisha kwanza kwa sababu hizohizo za kutokuleta taharuki kwa taifa.
 

Ok, huenda una hoja, covid ipo na sio hapa nchini tu, mbona hapa kwetu serikali inaleta blabla? Mpaka leo mbona hawatoi takwimu za wagonjwa kulingana na kanuni za WHO? Hata Maalim Seif kama sio chama chake kutangaza kuwa amepata covid wala isingetangazwa. Kabla ya awamu hii kuingia madarakani tulikuwa tunasikia magonjwa mbalimbali yalitangazwa na vyombo vya habari, na serikali ilifika na kuchukua hatua. Hatari ya magonjwa kutokutangazwa kunapelekea serikali kutokuwajibika.

Tuna uzoefu na serikali zinazodhibiti vyombo vya habari, nyingi huwa haziwajibiki kwa watu wake, bali hufanya vile watakavyo huku wananchi wakiendelea kutaabika. Mfano mrahisi sasa hivi mafuta ya kula bei iko juu, lakini kwakuwa vyombo vya habari vinaogopa kutangaza, basi serekali haipati pressure hivyo wananchi kuendelea na ugumu wa maisha.
 
Too much..Wanauwa upatikanaji wa taarifa.
Litakuja kutokea janga watu hawatoi taarifa
 
Kwahiyo hao watatu ni ugonjwa gani umewakumba..!?
Si umeambiwa walikuwa na vidonda vya tumbo (Peptic Ulcer Disease) vilivyo erode blood vessel na kusababisha hemetemesis (kutapika damu).
Wa kwanza ilikuwa tarehe 17/09/2020 na alifariki. Wa pili ilikuwa tarehe 28/12/2020 na alipona. Wa tatu alikuwa jana tarehe 06/02/2021 na anaendelea na matibabu lakini ndiye kasababisha hii taharuki iliyoanzishwa na huyo diwani wa chadema na huyo daktari lezy affair.
 
Hii taarifa ya Mama Waziri mbona ni ya kufokea zaidi kuliko kujibu swala husika?

Mara hakuna kitu kama hicho, mara kunahitajika uchunguzi zaidi, mara leo uchunguzi umefanyika, mara hata kama upo hutakiwi kusema,anasema Waziri!

Upuuzi mtupu!
 
Wanaogopa itakuwa Ni special mutated Covid 19
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…