Serikali yakiri kupokea malalamiko zaidi ya 6000 ya Uvunjifu wa Haki za Binadamu

Serikali yakiri kupokea malalamiko zaidi ya 6000 ya Uvunjifu wa Haki za Binadamu

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Damas Ndumbaro amesema jumla ya malalamiko ya wananchi kuhusu uvunjifu wa haki za binadamu 6,928 yalipokelewa katika kipindi cha mwaka 2018 hadi 2019.

Dk Ndumbaro ameyasema hayo wakati wa kilele cha Maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB).

“Malalamiko 564 yalichunguzwa na yapo katika hatua ya kuhitimishwa ambapo 211 yalikuwa ya nje ya mamlaka ya tume yalielekezwa taasisi zenye mamlaka ya kuyashughulikia" amesema

Mwenyekiti wa THBUB, Jaji Mathew Mwaimu amesema katika kutekeleza jukumu la uchunguzi wa uvunjifu wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora nchini, katika kipindi cha miaka 20, THBUB ilichunguza jumla ya malalamiko 31,462.

“Uchunguzi wa malalamiko hayo ulisaidia kupatikana kwa ufumbuzi wa migogoro mbalimbali sambamba na kupatikana haki za wananchi zilizovunjwa na kuimarisha misingi ya utawala bora iliyokiukwa,”amesema.

Jaji Mwaimu amesema kwa kuwa ikama ya watumishi kwa kuzingatia mtandao wa ofisi zilizopo kwa sasa ni 267, kuna upungufu wa watumishi 132.

Amesema kwa muda mrefu sasa tume haijapata fursa ya kuajiri watumishi wapya hasa katika maeneo ya wachunguzi, wanasheria, watafiti, wachumi na maafisa habari.

“Ili kuongeza ufanisi tunaiomba Serikali iipatie tume kibali cha kuajiri watumishi ili kuziba pengo hilo,”amesema.

Naye Katibu Mtendaji wa tume hiyo, Patience Ntwina amesema Jumla ya wadau 36 kutoka wizara, idara, mamlaka na wakala za Serikali pamoja na asasi za Kiraia walitoa huduma mbalimbali kwa wananchi kuanzia Septemba 10,2022 kama sehemu ya maonyesho ambayo ni sehemu ya madhimisho hayo.

“Hadi kufikia Septemba 14,2022 jumla ya wananchi 3,257 walishiriki katika maonyesho hayo,”amesema.
 
04 November 2022

Ruto akizungumza | Uzinduzi wa Ripoti ya Mwaka | Hali ya Mahakama na Utawala wa Haki

 
Back
Top Bottom