Serikali yakiri makosa kuwalazimisha Wafanyakazi wa Umma kununua laini ya simu ya TTCL

Serikali yakiri makosa kuwalazimisha Wafanyakazi wa Umma kununua laini ya simu ya TTCL

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema kwamba haukuwa utaratibu sahihi kuwalazimisha viongozi wa serikali kumiliki na kutumia laini za Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).

Amesema kufanya hivyo kunaweza kusiwe na matunda yanayotarajiwa kwani kiongozi anaweza kuinunua kwa sababu amelazimishwa, lakini akatumia ya mtandao ambao yeye anaupenda.

“Huduma hizi hazilazimishwi. Ukiwalazimisha watu wachukue laini, watachukua hiyo uliyowalazimisha halafu watachukua na ile wanayoipenda,” amesema Nape na kuongeza kwamba “I don’t think if it was a good model [sidhani kama ulikuwa utaratibu mazuri.”

Nape amesema hayo akijibu swali la mmoja wa waandishi wa habari aliyetaka kujua wizara ina mpango gani kuhakikisha kwamba TTCL inafikisha mawasiliano vijijini ikizingatiwa kwamba Hayati Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliagiza awatumishi wote wa serikali kuwa na laini za TTCL.

Aidha, katika mkutano huo wa kueleza mafanikio ya wizara kwa mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan iliibuliwa tena hoja ya gharama za intaneti na waziri akasema kwamba gharama zilivyo sasa zipo chini ya kiwango kinachokubalika kisheria.

“… kwa presha ya siasa tumeshuka hadi tukapitiliza kiwango kilichoiwekwa kisheria. Sasa hatuwezi kuendelea kushuka kama tunahitaji huduma bora,” amesema.

Amesema kuwa ukitaka huduma bora sharti ukubali kuigharamikia kidogo na kuwataka wananchi kuacha malalamiko, kujiona wanyongea au kudhani kwamba wanaonewa.

Hata hivyo, amesema Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inaendelea na mazungumzo na wadau kuona namna ya kuboresha gharama hizo ili kuimarisha na kukuza matumizi ya huduma za intaneti nchini.

Swahili Times
 
Kwani Flyover Marehemu alijenga kwa pesa za baba yake? Hebu acheni uzwazwa ninyi Lile jamaa lilikuwa jizi na katili kama jamaa zake akina Sabaya tuu na makonda.
ila mbowe anayeteua viti maalumu mpaka wapige mti ndiyo siyo katili?
 
🤣🤣🤣 Kitendo kile cha Magufuli kilisababisha wengi kuichukia TTCL hadi leo!

Kama watu wanavyoichukia ccm. Alilazimisha viongozi wote wa nchi wawe wa ccm. Halafu kuna wajinga eti walikuwa wanasema ccm ni imara maana walizawadiwa madaraka na Magufuli!
 
Hili lina tija gani kusemwa leo ?

Je haoni kwamba lina effect mbaya kwa kampuni ya TTCL ? Kwamba bila kulazimishwa hakuna aneyechukua...

Sio kwamba nawatetea @TTCL hata mimi siwakubali ila there is no point in kicking a dying man...., Especially kama its one of your Own...
Inabidi lisemwe ili lisirudiwe kamwe.
 
Inabidi lisemwe ili lisirudiwe kamwe.
For the detriment of the Company ?

Na anayesema ni nani ? Je anaitakia mema Kampuni ?, Vilevile kama hao watumishi wangeona kweli hizi line hazifai basi waumize kichwa na washikane mashati ili zifae..., after all wote ni watumishi wetu sisi wananchi na wengine wanakula ruzuku zetu (wote ni wale wale tu i.e. under performing)
 
Muhimu nukufuta cheo Cha uenyekiti wa chama kwa rais wa nchi niuchonganishi mkubwa kwa wananchi wakawaida na watumishi
 
Kwani si ilishafafanuliwa ni kwa kuwa viongozi tu, na wao ni kuwa wanapewa vocha za TTCL
 
Kwanza TTCL wajikite na simu za mezani(landlines) waachane na simu za mkononi.
For the detriment of the Company ?

Na anayesema ni nani ? Je anaitakia mema Kampuni ?, Vilevile kama hao watumishi wangeona kweli hizi line hazifai basi waumize kichwa na washikane mashati ili zifae..., after all wote ni watumishi wetu sisi wananchi na wengine wanakula ruzuku zetu (wote ni wale wale tu i.e. under performing)
 
Wakati wa utawala wa awamu ya 5 chini ya Dr Magufuli, viongozi wa serikali, wakiwemo Mawaziri na wafanyakazi wa serikali walilazimishwa kununua line ya simu ya TTCL kibabe, huku wengine wakipigwa mkwara kwamba wasipokuwa na line ya TTCL watang'olewa kwenye uongozi, lengo la jambo hilo kwa akili ya viongozi wa wakati ule ilikuwa kulazimisha mtandao wa TTCL kupata wateja wengi, hata hivyo idadi ya wafanyakazi wote wa serikali ya Tanzania inakadiriwa kufikia laki 6 tu.

Nchi yenye Raia wanaotajwa kuzidi mil 60, hata ukichukua wafanyakazi wote ukawapelekea line za TTCL kwa mtutu wa bunduki mtandao huo hauwezi kuteka soko kwa idadi hiyo ya wateja, Binafsi nilipinga vibaya sana jambo hilo na nikashauri viongozi wa wakati ule kwamba, ikiwa wanataka TTCL ishamiri basi Wanaccm wote waliodaiwa kuwa wengi sana nchini Tanzania ndio walazimishwe kununua line za TTCL, pamoja na kwamba Mwenyekiti wa ccm alikuwa Magufuli huyohuyo lakini ushauri wangu hakuufuata .

Leo Waziri Nape amekiri hadharani kwamba uamuzi ule haukuwa na lolote la maana.

===

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema kwamba haukuwa utaratibu sahihi kuwalazimisha viongozi wa serikali kumiliki na kutumia laini za Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).

Amesema kufanya hivyo kunaweza kusiwe na matunda yanayotarajiwa kwani kiongozi anaweza kuinunua kwa sababu amelazimishwa, lakini akatumia ya mtandao ambao yeye anaupenda.

“Huduma hizi hazilazimishwi. Ukiwalazimisha watu wachukue laini, watachukua hiyo uliyowalazimisha halafu watachukua na ile wanayoipenda,” amesema Nape na kuongeza kwamba “I don’t think if it was a good model [sidhani kama ulikuwa utaratibu mazuri.”

Nape amesema hayo akijibu swali la mmoja wa waandishi wa habari aliyetaka kujua wizara ina mpango gani kuhakikisha kwamba TTCL inafikisha mawasiliano vijijini ikizingatiwa kwamba Hayati Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliagiza awatumishi wote wa serikali kuwa na laini za TTCL.

Aidha, katika mkutano huo wa kueleza mafanikio ya wizara kwa mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan iliibuliwa tena hoja ya gharama za intaneti na waziri akasema kwamba gharama zilivyo sasa zipo chini ya kiwango kinachokubalika kisheria.

“… Kwa presha ya siasa tumeshuka hadi tukapitiliza kiwango kilichoiwekwa kisheria. Sasa hatuwezi kuendelea kushuka kama tunahitaji huduma bora,” amesema.

Amesema kuwa ukitaka huduma bora sharti ukubali kuigharamikia kidogo na kuwataka wananchi kuacha malalamiko, kujiona wanyongea au kudhani kwamba wanaonewa.

Hata hivyo, amesema Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inaendelea na mazungumzo na wadau kuona namna ya kuboresha gharama hizo ili kuimarisha na kukuza matumizi ya huduma za intaneti nchini.

Pia soma: Serikali: Sio Watumishi wote wa Umma wanatakiwa kuwa na laini ya TTCL bali Viongozi wanaopewa vocha watapewa za TTCL
Yule bwana alikuwa kichaa
 
Kwanza TTCL wajikite na simu za mezani(landlines) waachane na simu za mkononi.
Ni nini manufaa ya Simu za mezani ?

Unadhani teknolojia ya Chip ingegunduliwa kabla na hizi infrastructure za Mobile kuwepo kungekuwepo hata Simu za Mezani ?

That technology is dead and buried haina faida yoyote labda as an historical artifact...
 
Hizo zilikuwa akili za matope
Biashara inataka ubunifu na ushindani na sio kulazimisha watu wanunue bidhaa yako

TTCL kama wangecheza karata vizuri leo Soko lao lingekuwa juu sana na ndio wangekuwa wanakodisha mpaka line za underground walizoweka Halotel zingekuwa zao
Simu za mezani ni muhimu kila sehemu hilo wangelipa nguvu na kujitangaza kwa bei poa

Shirika la Posta angalia hamna kitu

Posta ya UK Ina miaka 500 na mpaka leo wanasambaza parcel Bilioni 16 kwa mwaka yes 16b items
Nao population ni kama sisi daaa
 
Ni nini manufaa ya Simu za mezani ?

Unadhani teknolojia ya Chip ingegunduliwa kabla na hizi infrastructure za Mobile kuwepo kungekuwepo hata Simu za Mezani ?

That technology is dead and buried haina faida yoyote labda as an historical artifact...
Kwa Biden na Uraya zinatumika sana kama vile Posta tu ambavyo ziko vizuri huko kwa mabeberu lakini hapa kwetu inachechemea.
 
Back
Top Bottom