Serikali yakwama ujenzi Mji mpya wa NSSF Dege Eco Village Kigamboni, yatangaza kuuza mradi

Hapana.jpm alitaka kuwashughulikia walioufisadi bahati mbaya akatutoka.kwa sasa mafisadi wamerudi na wanataka wajiuzie wao ili waendeleze kunufaika hao mafisadi
Acha porojo wewe...

Yaani since 2016 hadi 2020 bado tu "alitaka kuwashughulikia"?!

Btw, kama ambavyo aliwahi "kumshughulikia" mnene yupi serikalini na taasisi zake?!

Na kama alitaka kuwashughulikia kwavile aliona kuna ufisadi, ilikuaje tena DG wa NSSF akampa Ubalozi na kumpeleka Malaysia?!

Hivi mtaendelea kudanganyana hadi lini?!

Magu HAKUWA na guts za kushughulikia watu wazito... yeye aliishia ku-deal na civil servants tu tena wale ambao hawajafikia ministerial level.

Ukiondoa hao, gut yake nyingine ilikuwa kwa BAADHI tu ya Wafanyabiashara manake watu kama Rostam Azizi aliendelea kugonga nao cheers kama kawaida!!
 
Hizi pesa za wafanyakazi ni za kuchangia wajanja wachache wafanye miradi ya ujanja ujanja kama hii kwa malengo ya kujitajirisha huku wastaafu wakisota kupata mafao yao na kubanwa na kikokotoo......nchi ya kindezi sana hii.
Aliyeshiba hamjui mwenye njaa !! Tutabaki tunasema Lakini Mungu yupo !!
 
lini NSSF na mashirika mengine ya umma yakafanya biashara ndugu zangu kama si mwanya wa kufisadi michango ya wanachama wao maskini as a result.

Kwa mfano Daraja la Kigamboni wanashindwa nini kumtafuta mzabuni aendeshe pale wao wakusanye pesa, rather than wao wenyewe ku-run... wana ujuzi gani wa kukusanya mapato hawa NSSF ? walisomea wapi ?
 
Nadhani alitaka kwanza kupata uhakika wa kuwepo madarakani kwa muda mrefu zaidi ndipo angekuwa na uhakika wa kuwashughulikia hao magwiji aliokuwa anazijua habari zao !! Nadhania tu. !!!
 
Kama wanauza kiwepo kiwango cha chini kitakachohakikisha fedha ya umma ie nssf inarudi. Vinginevyo tutaona wizi wa mali ya umma kwa mradi kuuziwa mhuni au wahuni fulani kwa bei ya kutupa. Serikali isiachie bodi ya nssf maana ufisadi ndio unatawala shirika hilo.
Hebu tujiulize ni nani aliingia mradi huu na ilikua kwa faida ya nani?
Magufuli alipoamua nyumba za mradi huo ziwe hosteli za vyuo vikuu, je sio ndio ulikua uamuzi bora kuliko risk ya kuporwa mradi na fisadi kwa kujidai wanauza au kununua mradi?
Je si bora nyumba hizo kuuziwa wananchi kwa bei nafuu maana ujenzi wake umejaa gharama za upigaji wa wakurugenzi na management ya nssf?
 
Kwani hizo kelele lini zilimzuia kuwakamata? Na kwanini hakuwashughulikia akina dau basi kama ni kweli maana akina manj kama waliiba nssf basi walishirikiana na bodi ya nssf.
 
🤣🤣🤣kaka Pascal PPR itaweza hiyo ligi kweli?hapo tayari wakubwa washapangana,DG anakamilisha tu maandalizi ya mchezo.PPR jikite kwenye low cost housing,maeneo ya Kibaha,Kimara Bonyokwa,Kirungure,Mkuranga,Vianzi.nk.
Kutakatisha!!
 
Mpaka wakasema wanaboresha kikokotoo kumbe pesa hamna zimeishia kwenye magofu
 
Unawaza ki masikini sana
Jifunze kuwaza kibiashara
 
🤣🤣🤣kaka Pascal PPR itaweza hiyo ligi kweli?hapo tayari wakubwa washapangana,DG anakamilisha tu maandalizi ya mchezo.PPR jikite kwenye low cost housing,maeneo ya Kibaha,Kimara Bonyokwa,Kirungure,Mkuranga,Vianzi.nk.
PPR kama PPR haiwezi, bali una download tender documemts na ku parter na wanene, wao ndio watafanya kila kitu, wewe unakuwa local partner.
P
 
Purchasing power ya Wa Tanzania ni ndogo sn especially kwenye really Estate kupata muwekezaji DEGE ni ndoto ya asubuhi wewe Tazama tu palm village wanavyo hangaika kuuza apartments zao ndio utajua soko lipoje Tz mifano ipo mingi tizama yale majengo ya PSPF asilimia kubwa yapo wazi Tena City center huko ni Mji kama umekufa kabisa.
 

FOR SALE DEGE ECO VILLAGE, RESIDENTIAL PROPERTIES IN KIGAMBONI TANZANIA


Before abandoned Dege Eco village was designed to be a satellite township of Dar es salaam, being built on an area covering 300 acres at Kigamboni. A mixed use residential project addressing all segments of society, from high end to medium, as well as those who need affordable housing.
Source : Uniq Traveller
 
Toka maktaba:
Mnada ulitangazwa toka mwezi September 2017 leo October 2022 unatangazwa tena baada ya miaka mitano kupita.

Nini kimefeli ? Hatuna kampuni za udalali zenye ubavu na ujuzi wa kuchukua tenda hii hapa Tanzania kutokana na upungufu wa uwezo wa kufanya biashara ya shilingi trilioni 1 na zaidi za kiTanzania.

Je serikali na NSSF hawajaona upungufu huu hivyo kushirikisha wadau wa kimataifa wenye uwezo wa kifedha na ujuzi kutangaza mnada huu kimataifa

20 September 2017
BREAKING: Nyumba za NSSF Kigamboni zapigwa mnada
Mradi mkubwa wa ujenzi wa mji mpya wa Kigamboni Dar es Salaam uitwao Dege Eco Village ulioanzishwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya jamii 'NSSF' na kusimama ujenzi wake mwaka 2016 unapigwa mnada. Kuliripotiwa kuwepo kwa ufisadi wa zaidi ya TSH bilioni 179 katika mradi huo na sasa anatafutwa Mwekezaji atakaeuchukua.
Source : millard ayo
 
Duh...!. Bonge la fursa hili!.
Hapa Mchechu hawezi kuacha hii opportunity!.
Hapa matajiri watauwana!.
Huu ni wakati sasa wa PPR kuachana na media business na kuingia kwenye real estate na property!.
P
Pascal....acha kuota. Hapo anachukua Mwarabu mmoja kwa ulaini. Watu washakula vyao. Ikibuma hii, pale patakuwa magofu ya ukumbusho tu kwa vizazi vijavyo
 
SEMDOI REAL ESTATE madalali wa kiTanzania wajitupa ktk deal hili lakini mradi huu ni mkubwa umewazidi kimo

SITE VISITS AT DEGE - KIGAMBONI

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…