Serikali yakwama ujenzi Mji mpya wa NSSF Dege Eco Village Kigamboni, yatangaza kuuza mradi

Serikali yakwama ujenzi Mji mpya wa NSSF Dege Eco Village Kigamboni, yatangaza kuuza mradi

Vingine vyakucha, huu mradi umesimama kitambo sana
Achana nae Huyo anabwabwaja
Hajui A wala Che ya mradi
Huyo mtu wake anaemsifu ndani ya uongozi wake ndio kakongoroa kabisa hii mifuko ya hifadhi ya jamii, anzia NSSF, PSSF hadi NHIF

Hakujawahi kuyumba kwa mifuko ya hifadhi ya jamii katika awamu zote zilizopita zaidi ya wakati WA JPM, NHIF imefilisiwa halafu wanakuja na sababu uchwara kuwa madai ya uongo yamefilisi mfuko.

Huyu huyu Mwendazake kipindi chake aliruhusu mabilioni ya NSSF yatumike kujenga kiwanda cha sukari chini ya Kampuni ya Mkolazi Holding Company Limited, mpaka leo hii hawajazalisha hata kijiko kimoja wakati billions za NSSF zimekwenda, yule bwana alikuwa mbadhirifu.
 
Kweni huu mradi umefikia umefikia asilimia ngapi mpaka pale walipoutelekeza?
 
Nyie si ndo wale mnayemuona seth na rugemalira mashujaa baada yakutoka gerezani.
Seti na ruge hawakuwa na makosa na walikuwa hawashitakiki, hata ungewapeleka mahakama ya dunia,,
Jk aliwambia wazi, hazikuwa pesa za umma, yalikuwa malipo stahiki ya umeme tuliotumia,,
Politics ikaingia,, kina mnyika wanaoongea kwa kufoka foka wakawakalia kidedea,
Awamu ya tano ikalichukua na kuwakamata,, tatizo likawa palepale,, walikuwa innocent🤷🏽‍♂️
 
Mwenye uelewa wa kuandika zabuni ya huu mradi aje PM, navutiwa nao, nataka nimiliki mji na Mimi
 
11 December 2017 Ziara ya vigogo DEGE ECO Village


According to the Controller and Auditor General (CAG)’s 2014/15 Audit Report, NSSF entered a joint venture with Azimio Housing Estates to form Special Purpose Vehicle Company, Hifadhi Builders Limited.
Under the contract, Azimio undertook to develop 20,000 acres located in Rasi Dege, Kigamboni, of which NSSF holds 45 per cent, while Azimio holds 55 per cent shares
More info:

26 October 2022
Dar es Salaam, Tanzania

The National Social Security Fund NSSF has announced the sale of the Dege Eco Village project

The project was being developed jointly between the National Social Security Fund (NSSF) and Azimio Estate Housing Limited, and it is not clear why the pensions fund has decided to put it up for sale.

The Dege Eco Village project which is located in Kigamaboni was in 2021 flagged by the Parliamentary Accounts Committee as a risk after it had stalled since 2016 something that PAC said the project was risking to get into as depreciation phase.

Construction of the Dege Eco Village kicked off in January 2014 and was supposed to be implemented into three phases and phase one was meant to be completed 2015, whereas phases two and three were set to be completed in 2016 and in 2017 respectively.


At its inception, the project was mainly meant for the middle and higher income earners, raising eyebrows given the need for a project for lower income earners
Source : NSSF puts up Dege Eco Village for sale
 
Hizi nyumba zisiuzwe kiholela kuna hatari ya kumaliziwa chini ya viwango.
Huu mradi ni muhimu kwa kuupendezesha Dar-es-salaam.
TPDC,City Council, NHC,TIB,TPA,washirikiane kuujenga na kuendesha mradi huu kwa maslahi ya umma.
Hivi kwani Azimio wamejitoa kwenye mradi huu?
 
Nani atanunua mradi wa kipigaji huo? Huko viwanja SQM moja 10,000 NSSF wamenunua heka moja billion sio wizi huo? Kwanza ukishajenga mpangaji wako Nani? Kwanini akae au Anunue kiota huko na si sehemu kama Upanga,kawe au Morocco square?
Avic town ni mara Mia Bora kuliko hizo na mpaka Leo haziuziki.
Nssf wana mradi kama huko kijichi umedoda ndio maana wanataka kumtupia mtu huo mzigo. Watu washakula 10% zao wanavimba mitaani tu.
 
Nani atanunua mradi wa kipigaji huo? Huko viwanja SQM moja 10,000 NSSF wamenunua heka moja billion sio wizi huo? Kwanza ukishajenga mpangaji wako Nani? Kwanini akae au Anunue kiota huko na si sehemu kama Upanga,kawe au Morocco square?
Avic town ni mara Mia Bora kuliko hizo na mpaka Leo haziuziki.
Nssf wana mradi kama huko kijichi umedoda ndio maana wanataka kumtupia mtu huo mzigo. Watu washakula 10% zao wanavimba mitaani tu.

Changamoto hizi ulizozielezea kuhusu mradi huu wa Dege Eco Village wadau NSSF, AZIMIO na serikali wazichukue na kuzifanyia kazi
 
Hii NSSF ni chaka la wanasiasa kuchuku michango ya watu ndio maana kila kukicha wana kuja na visheria vya ajabu ajabu ili mradi wasitoe hela za wanachama wanao acha kazi. Huu ndio uwenda wazimu wa NSSF
 
Azimio hivi si ndio inamilikiwa nq bwana Akrab ambae alinyooshwa na mwendazake?
Ndo huyo na ni hapo ndiposa mradi ulipoanza kuyumba,, mwendazake aliwaamini wapinzani walipo u demonise mradi na wakamwita akbar ni fisadi,, so mwendazake alipokamata madaraka akaanza kudeal nae, katika style ile ya watazitapika na kuzitolea kwenye tundu lolote la mwili,,
Wapinzani walitu mislead sana hii nchi🙆🏻‍♀️
 
11 December 2014

DEGE MEETING PART 2 :

Dr. Ramadhani Dau aelezea undani wa miradi NSSF na jinsi walivyo na azma Dar es Salaam iondokane na vibanda iwe Magomeni, Temeke, Mbagala n.k na maeneo yote yafanane na DEGE ECO Village


Source : Dege Eco Village
 
Watu ambao mlipambana na magufuri akawashinda mnawakati mgumu sana aiseee.

Sasa magufuri anahusikaje hapo na huo mradi ulifeli tokea kipindi cha mkwere.
Aliyeusimamisha kwa kusema watu wamepiga ni nani? Na aliwafanya nini hao wapigaji?
 
View attachment 2398070

Baada ya kusuasua kukamilika kwa mradi wa Dege Eco Village kwa thamani ya dola 653 milioni za Marekani (zaidi ya Sh1.3 trilioni), Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) lililokuwa linautekeleza limetangaza kuuza kwa mwekezaji mwingine atakeyevutiwa nao.

Ujenzi wa mradi huo wa mji mpya wa Kigamboni jijini Dar es Salaam ulioanzishwa na NSSF mwaka 2014 ulisimama tangu Januari 2016 ukidaiwa kufisidi zaidi ya Sh179 bilioni hivyo kutokamilika kwa nyumba za kifahari, hoteli, maduka makubwa, eneo la wazi la mapumziko, baa, shule, hospitali, kumbi za mikutano, nyumba za ibada na migahawa.

Taarifa iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba na kusambazwa Jumanne Oktoba 25 imetangaza kutafutwa kwa mzabuni atakayeuendeleza mradi huo.

“NSSF inakusudia kuuza mradi mzima wa Dege Eco Village, shirika halitowajibika tena baada ya mauzo haya. NSSF inakaribisha zabuni zilizofungwa kuununua mradi huu kwa viwango vya kimataifa vilivyoainishwa kwenye Kanuni za Ununuzi wa Umma zilizochapishwa kwenye gazeti la Serikali namba 446,” inasomeka sehemu ya taarifa ya NSSF.

Kwa wawekezaji watakaovutiwa kuuendeleza mradi huo uliosimama kwa miaka saba sasa, NSSF imesema wanaweza kuutembelea huko Rasi ya Dege iliyopo Kigamboni jijini hapa ili kuukagua na kujiridhisha na mandhari yake kuanzia saa 4:00 asubuhi mpaka saa 7:00 mchana wa Novemba 3.

Zabuni zote, shirika hilo limesema zinapaswa kuwasilishwa mpaka Novemba 14, saa 9:00 alasiri kabla hazijafunguliwa mbele ya waombaji wote watakaokuwa wamejitokeza kwenye ukumbi wake uliopo ghorofa ya saba katika Jengo la Benjamin William Mkapa.

View attachment 2398094

Pia, soma=> Dar: Mradi wa Dege Eco village uliotelekezwa Kigamboni
Mimi sitashangaa hata kidogo mradi wa bwawa la Nyerere nao ukatafutiwa mwekezaji. Tusubiri yatakuja mengi nchi hii. Tuliambiwa nchi imerudi kwa wenyewe na kamwe wale watu wa kuja hawataruhisiwa tena kuongoza nchi hii. Wako wenyewe ujue hakuna kupona.
 
Duh...!. Bonge la fursa hili!.
Hapa Mchechu hawezi kuacha hii opportunity!.
Hapa matajiri watauwana!.
Huu ni wakati sasa wa PPR kuachana na media business na kuingia kwenye real estate na property!.
P
Mbona hatujaambiwa tathmini ya huo mradi hasara au faida watumishi wa Tanzania mchawi wenu ni CCM yaani michango yenu imeingia kwenye mifuko ya watawala wa ccm
 
DG akili ikiwa ndogo hawezi kuhimili mradi mkubwa unaohitaji akili kubwa. Dau alikuwa na akili kubwa sana ndio maaana pia alibuni na kuanzisha mambo makubwa. Sasa hawa DG ambao hawana exposure atawezea wapi Mega Project kama hiyo akili yake imeishia kuuza tu.
Mbona huyo Dau naye ulimshinda?
 
67f4631c-208a-4f65-bd38-653264149e0c-jpeg.2398468


Watanzania ni watu ambao wanadhani nchi aina sheria.


Wakurugenzi wa taasisi za umma hawana huo uhuru wa kujifanyia mambo kwa utashi tu kama baadhi ya watu wanavyodhani.

Hizo taasisi zipo kisheria azijiwikezei tu hela zipo regulated on amount ya kuwekeza kwenye kila aina ya miradi.

Mradi wowote wa commercial property pension funds airuhusiwi kuwekeza peke yake na ubia wake autakiwi kuzidi asilimia 30% ya capital investment ya mradi wote. Sasa ulizia mpaka ulipoishia NSSF iliweka kiasi gani Kigamboni.

Watu walikuwa hawaeshimu sheria enzi za JK na Dr Dau miradi yake mingi kwanza overpriced halafu NSSF inawekeza capital zaidi ya kile kinachoruhusiwa na serikali. Ata daraja la Kigamboni NSSF aikutakiwa kuwekeza zaidi ya 5% wakati tunaambiwa wana 35% or something.

Sasa unadhani miradi yenye miaka mingi ya return of investment itaacha pengo kiasi gani kwenye reserve za pension funds.

Ni hivi Magufuli alikuwa na kazi ngumu sana ya kuirudisha nchi kwenye mstari; hiyo mifuko aliikuta chali na kuanza kuipa uhai.

Hakuna mtu alietimuliwa na Magufuli kwa kuonewa walikuwa watu ovyo wengi wao; isipokuwa kwenye jamii ya watu wasiopenda kujifunza mambo yanavyotakiwa kufanyika ni rahisi kuwaongopea na kumtupia kila lawama Magufuli.
 
Hapana, JPM alitaka kuwashughulikia walioufisadi bahati mbaya akatutoka. Kwa sasa mafisadi wamerudi na wanataka wajiuzie wao ili waendeleze kunufaika hao mafisadi
Yeye ndio alikuwa kubwa la mafisadi huyo mungu wenu
 
Back
Top Bottom