Serikali yakwama ujenzi Mji mpya wa NSSF Dege Eco Village Kigamboni, yatangaza kuuza mradi

Kama wangejua hesabu wasingekuwa katika hali hii,pili hata kama wanajua hesabu hawana uhuru wa kujiamlia mambo yao bila kuingiliwa na external forces.
Tatu waliambiwa walime miwa wakatenga pesa ya ujenzi wa mtambo 6 mil usd,yasemekana pesa walipewa Tanroad wawanunulie mtambo huo,na hela imeyeyuka.
Nne waliingia mkataba wa mradi na kampuni iliyokuwa haina sifa yoyote zaidi ya kufyonza pesa za taasisi.
Kuna siku waliamka asubuhi wakasikia mjomba Magu ameunganisha mifuko yote!!just like that.
Ufanisi watautoa wapi katika hali ya kubadirisha bodi na manejimenti kama vitumbua ndani ya karai yenye mafuta moto?
Their not good enough to handle the project
Ushaambiwa baada ya kuingia awamu ya tano, mwendazake aliamini kutokana na maneno ya wanasiasa kuwa huo mradi ulikuwa hauna maana,, huo na ule wa gesi mtwara, kwahiyo nadhani hakuwa na nia ya kuendelea nao,,
Ushaambiwa mbia wa mradi mr Akbar ambae pengine labda angeleta wawekezaji, alipatikana na muhaho na nadhani nae akaloose interest😇🙆🏻‍♀️,
Yaani wapinzani wametucost sana,, saa hizi tungekua tunauzwa gesi europe na kuingiza matrilioni ya dola😂
 
Sasa mkuu tangu lini TANROAD ikahusika na mitambo ya sukari? 😄,
Tanroad wao waulize ishu za lami, kokoto, katapila, excavators, etc
 
Mtu wa kulaumiwa katika hili kwa sehemu kubwa ni Magufuli. Ni yeye aliyesitisha mwendelezo wake (kutokana na tuhuma za ufisadi) lakini akakosa njia mbadala ya kuhitimisha hilo, hivyo akayaacha magofu.
 
Sasa kuna shida gani mtu akinunua?, Nssf wanachohitaji ni pesa yao irudi ili wawekeze kwingine kuliko na faida,, hivyo ndo biashara hufanyika duniani kote,, au mlitaka hayo majengo tuyafanye shule ya kata labda? 🤷🏻‍♂️😲
Si ni mpaka irudi sasa Boss 🤣.... tufanye itarudi kama lilivyo lengo.
 
View attachment 2398070

Baada ya kusuasua kukamilika kwa mradi wa Dege Eco Village kwa thamani ya dola 653 milioni za Marekani (zaidi ya Sh1.3 trilioni), Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) lililokuwa linautekeleza limetangaza kuuza kwa mwekezaji mwingine atakeyevutiwa nao.

Ujenzi wa mradi huo wa mji mpya wa Kigamboni jijini Dar es Salaam ulioanzishwa na NSSF mwaka 2014 ulisimama tangu Januari 2016 ukidaiwa kufisidi zaidi ya Sh179 bilioni hivyo kutokamilika kwa nyumba za kifahari, hoteli, maduka makubwa, eneo la wazi la mapumziko, baa, shule, hospitali, kumbi za mikutano, nyumba za ibada na migahawa.

Taarifa iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba na kusambazwa Jumanne Oktoba 25 imetangaza kutafutwa kwa mzabuni atakayeuendeleza mradi huo.

“NSSF inakusudia kuuza mradi mzima wa Dege Eco Village, shirika halitowajibika tena baada ya mauzo haya. NSSF inakaribisha zabuni zilizofungwa kuununua mradi huu kwa viwango vya kimataifa vilivyoainishwa kwenye Kanuni za Ununuzi wa Umma zilizochapishwa kwenye gazeti la Serikali namba 446,” inasomeka sehemu ya taarifa ya NSSF.

Kwa wawekezaji watakaovutiwa kuuendeleza mradi huo uliosimama kwa miaka saba sasa, NSSF imesema wanaweza kuutembelea huko Rasi ya Dege iliyopo Kigamboni jijini hapa ili kuukagua na kujiridhisha na mandhari yake kuanzia saa 4:00 asubuhi mpaka saa 7:00 mchana wa Novemba 3.

Zabuni zote, shirika hilo limesema zinapaswa kuwasilishwa mpaka Novemba 14, saa 9:00 alasiri kabla hazijafunguliwa mbele ya waombaji wote watakaokuwa wamejitokeza kwenye ukumbi wake uliopo ghorofa ya saba katika Jengo la Benjamin William Mkapa.

View attachment 2398094

Pia, soma=> Dar: Mradi wa Dege Eco village uliotelekezwa Kigamboni
Sawa sasa waliofuja zile bilioni imekuwaje?!
 
Nambie kimewashinda kipindi kuendeleza?
Miradi wa kifisadi from the beginning unaweza kuwa na matokeo chanya?
Akili zako ndogo hufikirii kwa nini miradi mingi ya majengo ya kibiashara hazina wapangaji?
Hayo magorofa unayoyaona hapo Dar gorofa za juu haina wangaji miaka nenda rudi!
Walikuwa wanaazisha miradi ya kifisadi wapige ten percent lakini wewe juha umekazania kumlaumu JPM!
Juzi hapa mlisema mmeshafungua nchi! What's wrong going on?
Kuna ka ukweli flani
 
View attachment 2398070

Baada ya kusuasua kukamilika kwa mradi wa Dege Eco Village kwa thamani ya dola 653 milioni za Marekani (zaidi ya Sh1.3 trilioni), Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) lililokuwa linautekeleza limetangaza kuuza kwa mwekezaji mwingine atakeyevutiwa nao.

Ujenzi wa mradi huo wa mji mpya wa Kigamboni jijini Dar es Salaam ulioanzishwa na NSSF mwaka 2014 ulisimama tangu Januari 2016 ukidaiwa kufisidi zaidi ya Sh179 bilioni hivyo kutokamilika kwa nyumba za kifahari, hoteli, maduka makubwa, eneo la wazi la mapumziko, baa, shule, hospitali, kumbi za mikutano, nyumba za ibada na migahawa.

Taarifa iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba na kusambazwa Jumanne Oktoba 25 imetangaza kutafutwa kwa mzabuni atakayeuendeleza mradi huo.

“NSSF inakusudia kuuza mradi mzima wa Dege Eco Village, shirika halitowajibika tena baada ya mauzo haya. NSSF inakaribisha zabuni zilizofungwa kuununua mradi huu kwa viwango vya kimataifa vilivyoainishwa kwenye Kanuni za Ununuzi wa Umma zilizochapishwa kwenye gazeti la Serikali namba 446,” inasomeka sehemu ya taarifa ya NSSF.

Kwa wawekezaji watakaovutiwa kuuendeleza mradi huo uliosimama kwa miaka saba sasa, NSSF imesema wanaweza kuutembelea huko Rasi ya Dege iliyopo Kigamboni jijini hapa ili kuukagua na kujiridhisha na mandhari yake kuanzia saa 4:00 asubuhi mpaka saa 7:00 mchana wa Novemba 3.

Zabuni zote, shirika hilo limesema zinapaswa kuwasilishwa mpaka Novemba 14, saa 9:00 alasiri kabla hazijafunguliwa mbele ya waombaji wote watakaokuwa wamejitokeza kwenye ukumbi wake uliopo ghorofa ya saba katika Jengo la Benjamin William Mkapa.

View attachment 2398094

Pia, soma=> Dar: Mradi wa Dege Eco village uliotelekezwa Kigamboni
Haya ni Ya Wastaafu. Ndio kisa wameamua kuwapa Wazee Mafao ya Kikokotooo. Wanawekeza fedha zao hazirudi, wanaamua kuwapunja Mafao Yao ya mkupuo Ili kuficha madudu haya kuwekeza bila Faida.
 
Sasa mkuu tangu lini TANROAD ikahusika na mitambo ya sukari? 😄,
Tanroad wao waulize ishu za lami, kokoto, katapila, excavators, etc
Matatizo juu ya matatizo. Hiyo ndio Bongoland.
 
Serikali haifilisiki kirahisi hivyo, kila siku vyanzo vya mapato vinaongezeka, haiwezi kushindwa kulipa wastaafu mafao stahiki, japo inaweza tokea kuchelewa kwa baadhi ya watu kwasababu fulani fulani, mifuko ya hifadhi za jamii huwekeza pesa na hata kununua bond za Serikali, huwezi kuacha mabilioni benki yamelala tu, ni hasara
Haya ni Ya Wastaafu. Ndio kisa wameamua kuwapa Wazee Mafao ya Kikokotooo. Wanawekeza fedha zao hazirudi, wanaamua kuwpunja Mafao Yao ya mkupuo Ili kuficha madudu haya kuwekeza bila Faida.
 
si nimpaka irudi sasa Boss 🤣.... tufanye itarudi kama lilivyo lengo.
Itarudi hata kama si kwa kiwango kile, inaweza kuzidi au kupungua,, kiufupi mifuko ya jamii isipowekeza, pesa zikakaa tu bank, ni hasara kubwa sana, duniani kote mifuko ya jamii ina invest na hata kuikopa Serikali kwa kununua bond.
 
Ushaambiwa baada ya kuingia awamu ya tano, mwendazake aliamini kutokana na maneno ya wanasiasa kuwa huo mradi ulikuwa hauna maana,, huo na ule wa gesi mtwara, kwahiyo nadhani hakuwa na nia ya kuendelea nao,,
Ushaambiwa mbia wa mradi mr Akbar ambae pengine labda angeleta wawekezaji, alipatikana na muhaho na nadhani nae akaloose interest😇🙆🏻‍♀️,
Yaani wapinzani wametucost sana,, saa hizi tungekua tunauzwa gesi europe na kuingiza matrilioni ya dola😂
Gas ipi mkuu? Ile iliyowekewa bondi kisa Rizmoko?
 
Gas hipi mkuu? Ile iliyowekewa bondi kisa Rizmoko?
Ndio wapinzani walivumisha huo uongo eti gesi ya Mtwara ishauzwa China, mwendazake nae akaamini hivyo, matokeo yake mradi ukaishia njiani🤷🏼‍♂️, saa hii tungekuwa na gesi refinery tayari tusingekuwa tunahangaika kuagiza gesi ya kupikia nje ya nchi.
 
Ndio wapinzani walivumisha huo uongo eti gesi ya mtwara ishauzwa china,, mwendazake nae akaamini hivyo,, matokeo yake mradi ukaishia njiani🤷🏼‍♂️,saa hii tungekuwa na gesi refinery tayari tusingekuwa tunahangaika kuagiza gesi ya kupikia nje ya nchi
Project ya Gas haikukwama kwasabbu hiyo ila Magufuli na Serikali yake hawakuridhika na Proposal ya mwekezaji wa LNG, sawa na mradi wa Bandari ya Bagamoyo tu hivyo ulisimama huku wakimshinikiza Mwekezaji asijipendelee yeye kuliko nchi.
 
Project ya Gas haikukwama kwasabbu hivo ila Magufuli na Serikali yake hawakulidhika na Proposal ya mwekezaji wa LNG, sawa na mradi wa Bandari ya Bagamoyo tu hivo ulisimama huku wakimshinikiza Mwekezaji asijipendelee yeye kuliko nchi.
Wale wanakuja na capital, wanakuja na mitambo, wanakuja na technology yao, bado TPDC walipewa partinership, sikumbuki kwa asilimia ngapi, lakini ilikuwa fair.

Kilichotokea majungu na siasa zikaingilia kati,
Hakuna wapinzani hasa wa bongoland watafurahia kuona Serikali inafanikisha jambo, kitu ambacho kita influence wananchi kwenye sanduku la kura🤷🏾‍♂️
 
Ndio wapinzani walivumisha huo uongo eti gesi ya mtwara ishauzwa china,, mwendazake nae akaamini hivyo,, matokeo yake mradi ukaishia njiani🤷🏼‍♂️,saa hii tungekuwa na gesi refinery tayari tusingekuwa tunahangaika kuagiza gesi ya kupikia nje ya nchi
Unataka kuwabebesha zigo wapinzani. Si ilikuwa inasemwa kwamba jamaa ana akili sana? Ilikuwaje kuambiwa jambo lisilo la kweli halafu akaliamini?

Kuna bandiko humu la Pascal Mayalla kuhusu mkopo wa Gesi kwamba tutalipa asilimia 20 za utangulizi na 80 italipwa kwa miaka 80 kila mwaka asilimia moja na hapo deni halisi halijalipwa.
 
Back
Top Bottom