Serikali yampa ajira Mwanamke anayekumbatia Watoto njiti hospitali ya Amana

Huyo dada atakuwa na nyuzijoto 40C mwilini.
Na huko kwenye papuchi kutakuwa na 50C
Just Joking 😂
 
Zawadi na ajira ni stahiki yake kwa wema alio fanya. Tusiishie kusifia, yapo ya kujiuliza. Serikali inashindwa kuweka vyumba vya joto katika hospitali walau ngazi ya wilaya? Na hapo ni dar, mikoani hali ikoje? Tutapata kina Mariamu kila hospitali? Njiti wangapi wamekufa kwa kukosekana kina Mariamu? Mariamu akiugua inakuaje? Kuna njiti waliuawa na kunyofolewa viungo wakiandaliwa kusafirishwa hospitali wilaya, kisa kituo hakuna huduma ya kutunza njiti. Ni vema rais(serikali) akatatua chanzo, tatizo ni kubwa.
 
Huu nao ni upumbavu.
Kama hana sifa kwanini aruhusiwe kutoa huduma?
Kwanini apewe kazi ya mkataba kama hana sifa?
Kigezo hicho kilichotumika kumpa temporary contract kitumike hichohicho kumpa permanent contact
 
Hizo nguvu si wangewekeza kwenye kununua incubators za kutosha.

Wabongo wapo busy kutetea Dp kisa inatumia mashine lakini wapo busy tena kumpongeza Rais kwa kutoa pesa za kukumbatia watoto badala ya kushauri zinunuliwe mashine za kutosha
Watanzania tumedumazwa akili. Serikali inashindwa kuwajibika, bado inatetewa.
 
Hizo nguvu si wangewekeza kwenye kununua incubators za kutosha.

Wabongo wapo busy kutetea Dp kisa inatumia mashine lakini wapo busy tena kumpongeza Rais kwa kutoa pesa za kukumbatia watoto badala ya kushauri zinunuliwe mashine za kutosha
Imagine dunia ya leo tunatumia.mtu kukumbatia watoto, hygenically naona haipo sawa jamani, tunarudi nyuma wakati dunia inasonga mbele
 
Joto la binadamu ni nzuri zaidi.
Hata km atawekwa kwenye incubator kuna muda atahutajo joto la mama.
 
mashine ndio zipo lakini hazitoshi Sasa Kuna shida gani dada kujitolea kuokoa maisha ya hao watoto ambao walikosa nafasi katika hizo mashine
Kwahiyo serikali inapaswa kuongeza mashine za kuokoa watoto au kumpongeza Mariamu?
Kama Mariamu ameokoa watoto watatu, je, kabla yake wangapi wamekufa?. Je hospital zingine ambazo Mariamu hayupo hakuna tatizo la upungufu wa mashine?
 
Kuna makala niliwahi kuangalia, ilisema kwa watoto njiti joto linalofaa zaidi ni la mwanadamu, linasaidia kwa haraka kuliko hizo incubator, sasa mnaomnanga huyu dada hebu tafuteni maarifa msiwe mnakurupuka tu
Usikariri. Joto la mwanadamu linajulikana, machine za joto zinasawazishwa kuwa sawa na joto hilo. Uzembe wa usimamizi unaweza leta majanga, lakini kwa technology iliopo heat sensors na automation zina ondoa madhara yote . Mariamu akiugua joto linapanda, inabidi uwe nao wa akiba na ni kuongeza gharama.
 
mashine ndio zipo lakini hazitoshi Sasa Kuna shida gani dada kujitolea kuokoa maisha ya hao watoto ambao walikosa nafasi katika hizo mashine
Ficha ujinga wako. atawakumbatia wangapi? hao watoto wanazaliwa wangapi kwa siku?? akiwaambukiza magonjwa ya ngozi inakuwaje???

Serikali inatakiwa kununua mashine za kutosha za kulea watoto nditi. siyo kutafuta kiki ya watoto kukumbatiwa.
 
Mother and baby skin contact...
 
Nadhani wewe ndie mbumbumbu hasa anaesemwa
 
Imagine dunia ya leo tunatumia.mtu kukumbatia watoto, hygenically naona haipo sawa jamani, tunarudi nyuma wakati dunia inasonga mbele

Punguzeni ujuaji jamani!

Sio vibaya pia mkatafiti japo kidogo kuhusu kinachojadiriwa hapa na sio kuweka mapingamizi na ukosoaji kwa kila kitu Kisa tu mnauhuru wa kufanya hivyo!

Eti “hygenically”?!?
Ni aibu kwa kweli, Aibu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…