Serikali yamrejeshea Pascal Mayalla Press card yake iliyozuiliwa kwa takriban miaka 3 ataanza kuonekana Saba Saba!

Mwandishi wa habari nguli nchini Pascal Mayalla ameishukuru serikali na hususani msemaji wa serikali Dr Abbas kwa kumrejeshea Press card ambayo ilizuiliwa kwa takribani miaka mitatu.

Pascal Mayalla amesema kuanzia wiki ijayo ataanza kuonekana live kwenye maonesho ya Saba saba na soon ataanza kurusha vipindi vya kuhamasisha uzalendo nchini.

Source: Jicho Letu ndani ya habari Star TV!
Hongera zake,he is very hardworking...
 
Wiki iliyopita nilimwambia namjua Pasco wa enzi za JK, na Paskali Mayalla wa enzi hii ya Magufuli. Yeye alisema ni yule yule, wakati mimi nilimwambia tofauti ipo wazi.
Pasco sidhani kama njaa ndo ilimbadilisha.
Nafikiri Ben Saanane na Azory zilimuogopesha.
Kwahiyo anauma na kupuliza..
 
Hivyo ni viwanda vya hisia. Hapo pwani napita kila mara mbona sivioni? Hebu nisaidie nipatie hiyo list ya viwanda na location yake hapo pwani. Wiki ijayo napita huko.
Jiulize bidhaa zilizopo mtaani zinatoka wapi?
 
Mwandishi wa habari nguli nchini Pascal Mayalla ameishukuru serikali na hususani msemaji wa serikali Dr Abbas kwa kumrejeshea Press card ambayo ilizuiliwa kwa takribani miaka mitatu.

Pascal Mayalla amesema kuanzia wiki ijayo ataanza kuonekana live kwenye maonesho ya Saba saba na soon ataanza kurusha vipindi vya kuhamasisha uzalendo nchini.

Source: Jicho Letu ndani ya habari Star TV!
Pascal Mayala anafaa kuwa Msemaji wa Serikali akichukua nafasi ya Dr Abbas ambaye ni Katibu Mkuu kwa sasa. Na mtu wa kumpika afikie viwango ni Dr Abbas.
 
Richard ninajua kuwa ww ni mjinga, ila sikujua kuwa ni mjinga kiasi hiki! Wazungu wamuandae Tundu Lisu kwa ajili ya madini yaliyopo hapa nchini. Kwani mpaka sasa wanaochimba hayo madini ni wazaramo? Hawa wazungu waliopo sasa hivi ni tofauti na wazungu huko Lisu alipo? Ni madini gani ambayo yako hapa nchini wazungu wameyataka wakayakosa, ila Lisu akiwa rais ndio watayapata? Je hayo madini yaliyopo hapa nchini hayapo pengine Afrika, bali yako tu hapa Tanzania? Hivi hizi propaganda za kizee bado mnawalisha vijana wa kizazi hiki, na mtegemee kuwahadaa?

Nilitarajia utakuja na utatoa majibu uloandika.

Lakini ni mazungumzo tu ya mtandaoni hayanipi tabu.

Mjinga ni wewe (listen to what you are saying) unaetetea vibaraka wa hao wazungu wenu wanaowatumia.

Na hufahamu kuwa huo ndo ujinga.

Get the concept.
 
Nilitarajia majibu hata kutoka kwako.

Lakini ni mazungumzo tu ya mtandaoni hayanipi tabu.

Mjinga ni wewe (listen to what you are saying) unaetetea vibaraka wa hao wazungu wenu wanaowatumia.

Na hufahamu kuwa huo ndo ujinga.

Mzungu gani amtume mtu, karne ya 21 bado mnaleta siasa za karne iliyopita! Ni kipi wazungu watataka ndani ya nchi hii wakose mpaka wamtume mtu? Acheni siasa za kupuuzi.
 
Mzungu gani amtume mtu, karne ya 21 bado mnaleta siasa za karne iliyopita! Ni kipi wazungu watataka ndani ya nchi hii wakose mpaka wamtume mtu? Acheni siasa na kupuuzi.

Wauliza masuali ya kitoto sana.

Hii ni Tanzania mpya kwenye njia mpya ya kuelekea uchumi wa kati.

Hakuna upuuzi wa kuiba tena rasilimali za watanzania, ref (kuwepo sheria mpya ya madini)

Nakupatia ushauri wa bure, badilisheni siasa zenu za upinzani muwe na mkakati mlenge kwenye makosa ya kisera ya CCM na kwenye ilani yao ya uchaguzi.

Hapo labda mnaweza kuanza kuonekana mko serious.

Kuna sehemu nimeeleza namna ya upinzani kuwa strategic.

Vinginevyo sahau, kwani raisi wa nchi huwa hapatikani sokoni au mabarabarani.

Raisi wa nchi huandaliwa au huteuliwa kutokana na miongoni mwao kulingana na mazingira ya wakti huo.
 
Ndio umeanza kujua mambo ya sera sasa? Hayo mambo yako miaka na miaka. Au sera ni mpaka ziwafurahishe ccm ndio ujue ni sera? Inatakiwa kuwe na tume huru ya uchaguzi ndio utajua wananchi wanaweza kuchagua kwa sera, na sio utashi wa kikundi kilichoko madarakani ndio kiamue sera zipi ni sahihi. Umeeleza upinzani kuwa strategic kwa vigezo vya kiccm!

Rais huandaliwa na nani zaidi ya kura za wananchi? Kama huandaliwa, wananchi wanaenda kupoteza muda wao kwenye vituo vya kura ili iwe nini?
 
Mgombea uraisi huandaliwa na CC kisha hupitishwa na mikutano mkuu wa Halmashauri kuu ya Taifa.

Baada ya hapo ni kunadi sera na ilani ya CCM.

Sasa unadai tume huru tuambie hapa ni nchi gani hapa duniani huendesha uchaguzi unaosimamiwa na tume huru ya uchaguzi?

Kwa mfano hata Marekani tume ya uchaguzi inawajibika kwa bunge la senate na bunge hilo lina uwezo wa kupinga matokeo yalotangazwa na tume hiyo.

Uingereza nako tume yao ya uchaguzi inawajibika kwa spika wa bunge na kamati yake inayoundwa na wabunge kutoka vyama mbalimbali.

Haya ni mataifa makubwa duniani na huwa kuna wakati yanakumbana na utata kwenye chaguzi zake za uraisi.

Kama wakumbuka uzuri matokeo ya Al Gore dhidi ya George Bush junior ambapo kura zilirudiwa kuhesabiwa kwenye jimbo la florida na Bush akashinda.

Uingereza mwaka 2010 kuna wananchi wapiga kura walizuiwa kwenye baadhi ya vituo kuendelea kupiga kura ambayo kama ingekuwa hivyo basi, David Cameron asingeshinda kwa urahisi dhidi ya chama cha Labour.

Na mwaka 2015 kuliitishwa azimio la kutaka tume hiyo (huru) ya Uingereza ifanyiwe reform kwa madai kwamba inapendelea upande mmoja kwenye maamuzi ya uchaguzi.

Sasa ukiangalia utaona kwamba hakuna tume iliyo huru kabisa na ambayo inaundwa na watu ambao hawako kwenye payroll ya serikali.

Sasa wewe wataka tume huru ya aina gani?
 
Sitaki tume huru ya malaika, maana najua haiwezi kuwepo. Lakini sio tume hii inayoagizwa kumtangaza mtu aliyeshindwa, ili kufikia utashi wa rais. Hii tume yetu imefikia mahali inaitwa tume tu kwakuwa iko kisheria, lakini ni mtu mjinga, au mwenye upofu wa itikadi pekee ndio anaweza kutetea utendaji wa tume hii. Uzi huu sio wa udhaifu wa tume iliyopo, ila ningeweza kuorodhesha udhaifu wa wazi wa hii tume, kisha uniambie hizo za nchi ulizotaja zina mapungufu haya?
 
Welcome back Kamarade Paschal Mayala Laizer, tip hii ikukae kichwani barabara " utawala wa kambale Tanzania umekwisha"
 
Back
Top Bottom