Ndio umeanza kujua mambo ya sera sasa? Hayo mambo yako miaka na miaka. Au sera ni mpaka ziwafurahishe ccm ndio ujue ni sera? Inatakiwa kuwe na tume huru ya uchaguzi ndio utajua wananchi wanaweza kuchagua kwa sera, na sio utashi wa kikundi kilichoko madarakani ndio kiamue sera zipi ni sahihi. Umeeleza upinzani kuwa strategic kwa vigezo vya kiccm!
Rais huandaliwa na nani zaidi ya kura za wananchi? Kama huandaliwa, wananchi wanaenda kupoteza muda wao kwenye vituo vya kura ili iwe nini?
Mgombea uraisi huandaliwa na CC kisha hupitishwa na mikutano mkuu wa Halmashauri kuu ya Taifa.
Baada ya hapo ni kunadi sera na ilani ya CCM.
Sasa unadai tume huru tuambie hapa ni nchi gani hapa duniani huendesha uchaguzi unaosimamiwa na tume huru ya uchaguzi?
Kwa mfano hata Marekani tume ya uchaguzi inawajibika kwa bunge la senate na bunge hilo lina uwezo wa kupinga matokeo yalotangazwa na tume hiyo.
Uingereza nako tume yao ya uchaguzi inawajibika kwa spika wa bunge na kamati yake inayoundwa na wabunge kutoka vyama mbalimbali.
Haya ni mataifa makubwa duniani na huwa kuna wakati yanakumbana na utata kwenye chaguzi zake za uraisi.
Kama wakumbuka uzuri matokeo ya Al Gore dhidi ya George Bush junior ambapo kura zilirudiwa kuhesabiwa kwenye jimbo la florida na Bush akashinda.
Uingereza mwaka 2010 kuna wananchi wapiga kura walizuiwa kwenye baadhi ya vituo kuendelea kupiga kura ambayo kama ingekuwa hivyo basi, David Cameron asingeshinda kwa urahisi dhidi ya chama cha Labour.
Na mwaka 2015 kuliitishwa azimio la kutaka tume hiyo (huru) ya Uingereza ifanyiwe reform kwa madai kwamba inapendelea upande mmoja kwenye maamuzi ya uchaguzi.
Sasa ukiangalia utaona kwamba hakuna tume iliyo huru kabisa na ambayo inaundwa na watu ambao hawako kwenye payroll ya serikali.
Sasa wewe wataka tume huru ya aina gani?