Serikali yapiga marufuku matumizi ya vitabu 16 vikiwemo Wimpy Kid ili kulinda mila, desturi na tamaduni za Kitanzania

Covax

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2021
Posts
10,198
Reaction score
35,323
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda leo February 13, 2023 kwa Mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 59 cha sheria ya Elimu Sura 353 amepiga marufuku matumizi ya vitabu 16 vya ziada katika Shule za umma na binafsi nchini.

Vitabu vya 16 vilivyopigwa marufuku vimekutwa katika baadhi ya Shule si kama vitabu vya kiada wala ziada ambapo maudhui yake yanakizana na mila, desturi na utamaduni wa Mtanzania na yanahatarisha ukuaji wa Wanafunzi ikiwemo vinavyofundisha mapenzi ya jinsia moja.

Vitabu vilivyopingwa marufuku kutumika na kuwepo shuleni ni Diary of a Wimpy Kid, Diary of a Wimpy Kid -Rodrick Rules, Diary of Wimpy Kid - The Last Straw, Diary of Wimpy Kid-Dog Days, Diary of a Wimpy Kid The Ugly Truth, Diary of a Wimpy Kid -Cabin Fever.

Vingine ni Diary of a Wimpy Kid - The Third Wheel na Diary of a Wimpy Kid - Hard Luck, Diary of a Wimpy Kid - The Long Haul, Diary of a Wimpy Kid -Old School, Diary of a Wimpy Kid -Double Down, Diary of a Wimpy Kid-The Gateway, Diary, Diary of a Wimpy Kid-Diper Overlode.

Vitabu vingine vilivyopigwa marufuku kutumika shuleni ni Is for TANSGENDER ( you know best who you are!), Is for LGBTQIA ( find the words that make you you) na Sex Education a Guide to life.

FF91C59F-82EC-44EB-AD7A-9F1B7ED1D7E1.jpeg

Prof.Mkenda amesema, uwepo wa vitabu hivyo pia unahatarisha malezi bora ya watoto na kwa shule ambayo itabainika kuendelea kutumia vitabu hivyo mara baada ya katazo la Serikali itachukuliwa hatua mbalimbali za kinidhamu na kisheria ikiwemo kufutiwa usajili wake.

“Nahimiza wazazi mkague mabegi ya wanafunzi kuhakikisha vitabu hivi havitumiki nyumbani; ukaguzi na ufuatiliaji huu ni endelevu ili kubaini kama vitabu kama hivi hipo katika shule tuweze kichukua hatua,".Profesa Mkenda”

Prof. Mkenda ametoa rai kwa watanzania kupiga namba 0262160270 ya mezani na 0737 962965 ya mkononi ili kutoa taarifa ya uwepo wa vitabu hivyo shuleni na kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa shule yoyote itakayokutwa na vitabu hivyo ikiwemo kufutiwa usajili
 
Hivyo vitambu vitakuwa
IST
ISM
HOPAC
St C
DIA

Nimejaribu google ila sijaona sehemu kama kina maudhui tajwa.

Kama kuna mzazi ana ushahidi aweke hapa tuone, sio wa karatasi moja bali achukue video
 
Serikali ya Tanzania imeingia mkenge kukubali fake news ya "Diary of a Wimpy Kid" kilichobadilishwa na wahafidhina na kusambazwa Whatsapp?

Kama ni hivyo, Wizara ya Elimu itakuwa kichekesho kikubwa sana.

Kuna siku page moja ya moja ya hivi kitabu ilikuwa inasambazwa Wwhatsapp, ina maandishi ya kushawishi watoto kufanya ngono.

Sasa mwenzetu mmoja akashangaa sana, kwa sababu mtoto wake anavipenda sana hivi vitabu (yupo Uingereza).

Akakichukua kile kitabu, akatafuta ule ukurasa, akakuta ukurasa wa kwenye kitabu na ukurasa ulele unaosambazwa Wwhatsapp ni vitu viwili tofauti.

Tukajua hizi ni kampeni za fake news.

Sasa najiuliza sana, kama habari hizi ni kweli, je, wizara imefanya uhakiki kwenye vitabu?

Au imetumia maandishi yaliyoonekana Whatsapp na kukurupuka?
 
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda leo February 13, 2023 kwa Mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 59 cha sheria ya Elimu Sura 353 amepiga marufuku matumizi ya vitabu 16 vya ziada katika Shule za umma na binafsi nchini.

Vitabu vya 16 vilivyopigwa marufuku vimekutwa katika baadhi ya Shule si kama vitabu vya kiada wala ziada ambapo maudhui yake yanakizana na mila, desturi na utamaduni wa Mtanzania na yanahatarisha ukuaji wa Wanafunzi ikiwemo vinavyofundisha mapenzi ya jinsia moja.

Vitabu vilivyopingwa marufuku kutumika na kuwepo shuleni ni Diary of a Wimpy Kid, Diary of a Wimpy Kid -Rodrick Rules, Diary of Wimpy Kid - The Last Straw, Diary of Wimpy Kid-Dog Days, Diary of a Wimpy Kid The Ugly Truth, Diary of a Wimpy Kid -Cabin Fever.

Vingine ni Diary of a Wimpy Kid - The Third Wheel na Diary of a Wimpy Kid - Hard Luck, Diary of a Wimpy Kid - The Long Haul, Diary of a Wimpy Kid -Old School, Diary of a Wimpy Kid -Double Down, Diary of a Wimpy Kid-The Gateway, Diary, Diary of a Wimpy Kid-Diper Overlode.

Vitabu vingine vilivyopigwa marufuku kutumika shuleni ni Is for TANSGENDER ( you know best who you are!), Is for LGBTQIA ( find the words that make you you) na Sex Education a Guide to life.
 
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda leo February 13, 2023 kwa Mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 59 cha sheria ya Elimu Sura 353 amepiga marufuku matumizi ya vitabu 16 vya ziada katika Shule za umma na binafsi nchini...
Marufuku iende sambamba na kumtia kizuizini aliyeviruhusu ili nidhamu irejee
 
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda leo February 13, 2023 kwa Mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 59 cha sheria ya Elimu Sura 353 amepiga marufuku matumizi ya vitabu 16 vya ziada katika Shule za umma na binafsi nchini.

Vitabu 17 vimepigwa marufuku nchini​

Icho kitabu cha Dairy of Wimpy Kid kina movie yake. sijapata mda wa kuangalia sijajua ina maudhui gani
 
Back
Top Bottom