Serikali yaruhusu Mabasi ya abiria kusafiri kwa saa 24

Serikali yaruhusu Mabasi ya abiria kusafiri kwa saa 24

Ngoja tusubri route za wenye mabasi kwa safari za usiku.
 
Miundombinu ya nchi zote EA haina tofauti na tena kwa barabara za kuunganisha mikoa Tanzania imepiga hatua kubwa kuliko majirani.
Sure,katika hili serikali imejitahidi sana kwenye miundombinu...sio siku nyingi Kigomq nao wataunganishwa na mtandao wa barabara za lami bado kilometa chache sana..ifike hatua sio tunapinga kila kitu.
 
Sio kila basi litasafiri usiku. Ni Kama Mwanza to Dar. Ni mabasi matati tu Ally's, Katarama na Happy Nation wameruhusiwa kusafiri saa tisa usiku. Halafu safari za usiku mbona zimeanza zamani.
Ndiyo, coz ata kwetu yanatoka saa 9 na kuingia dar saa 2.
 
Kuna mdau alileta uzi hapa juzi kuwa aliona basi bovu sana la kampuni ya simba likiwa barabarani limebeba abiria ! Ndo asahau kuliona tena !
Latra wasipokuwa makini mabasi mengi mabovu yatarudi barabarani kwa ratiba ya usiku tu.
 
Hivi unajua mjinga mmoja barabarani anaweza kusababisha ajali hata kwa mtu mwenye akili zake timamu.

Ndiyo maana nikasema safari za usiku wataua watu wengi sana chanzo inaweza kuwa hayo malori speed au barabara mbovu jumlisha magari mabovu.

uhai ukitoka harudi
Huwezi kutatua changamoto ulizo nazo kwa kuzikwepa kwamba hazipo.Kwasababu kufa kupo pale pale.sasa kipi bora kati ya wewe mwenye akili timamu kutumia akili zako kuboresha mambo yawe vizuri kwa vizazi vingi vijavyo au usubiri ukisha kufa kizazi chako kije kufanya kwa namna mbaya?.
 
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeruhusu Mabasi ya abiria kufanya usafirishaji wa Saa 24, baaada ya kujiridhisha kiusalama, mwamko wa wananchi, huduma za mawasiliano pamoja na miundombinu ya usafirishaji.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Nchi, Jumanne Sagini wakati anaongea na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na kusema kuwa wamefikia maamuzi hayo baada ya Serikali kuimarisha shughuli za uchumi wa wananchi wake wa maeneo ya mjini na Vijijini.

Akiongeza kuwa wamezingatia maoni ya Wadau mbalimbali wakiwemo Wabunge, wamiliki wa mabasi, madereva wa mabasi, wasafiri, Wafanyabiashara na Wananchi kwa ujumla.

Aidha, Serikali imetoa maagizo kwa wadau wote wa usafirishaji kuzingatia Sheria, Kanuni na utaratibu wa leseni zao.

Pia madereva wametakiwa kuthibitishwa na LATRA, ambayo itatoa ratiba za safari kwa saa 24, TANROADS kuhakikisha ubora wa miundombinu, Serikali za Mitaa kuhakikisha zinasimamia usalama wa abiria kwenye huduma wanazosimamia pamoja na Jeshi la Polisi kusimamia Usalama wa watu na mali zao.
Itakuza uchumi sana ,mshindwe wenyewe.

Cha muhimu vigezo na masharti vizingatiwe , kampuni kubwa tuu Zenye Mabasi mengi na salama ndio zipewe leseni.

Wale wa Kuunga unga wasalie kusafiri mchana tuu.

Very sorry Kwa Kampuni njaa maana huenda zikawa eliminated kwenye soko Kwa sababu Abiria ana uhuru wa kusafiri mda na wakati wowote.
 
Watoa kafara utawajua tu kwa mbinu zao! Uchaguzi mkuu unakaribia wanataka kutoa sadaka ya damu wasingizie mabasi kusafiri usiku, na kama sio kweli nisemayo watupe criteria walizotumia kufikia kurejesha usafiri walioupiga marufuku wao wenyewe miaka hiyo, watwambie wameaddress vipi sababu zilizopelekea marufuku hiyo na control measures zitakazokuwepo sasa.

Habari ya madereva kusajiliwa LATRA sio kusajili mikono na miguu na ubongo wa dereva mhusika kufanya doria na check point barabarani hakuwezeshi kuwa na magari yote kwa muda wote hivyo uhuru na utashi wa dereva uko palepale na mabwana afande ndio watanifaika zaidi na rushwa kubwakubwa kutoka kwa madereva walevi.
 
Duuh pole aseeh...... Mm nipo ndani akn nilivosoma hii km ndo tumevamiwa
Ahsante ndugu, yaani nilikoma kupanda IT usiku. Ni risk sana mnaweza kufa kizembe.

Mbele tulikuta ajali IT nyingine ilikuwa inaenda Malawi dereva na abiria wawili walikufa palepale kapona mdada.
Basi na lile wenge la kuuponea kufa akaanza kuropoka,
Katoka Dar hajamuaga mume wake alikuwa anaenda Iringa kwenye graduation ya mchepuko wake, na mumewe kasafiri nje ya nchi akaanza kulia kinyachu pale hadi huruma. 🤣🤣🤣
Anasema, “Gwe Kyala umalaya huu mimi basi Ee joba, ningekufa hii aibu familia yangu wangeficha wapi sura zao??”
 
Ahsante ndugu, yaani nilikoma kupanda IT usiku. Ni risk sana mnaweza kufa kizembe.

Mbele tulikuta ajali IT nyingine ilikuwa inaenda Malawi dereva na abiria wawili walikufa palepale kapona mdada.
Basi na lile wenge la kuuponea kufa akaanza kuropoka,
Katoka Dar hajamuaga mume wake alikuwa anaenda Iringa kwenye graduation ya mchepuko wake, na mumewe kasafiri nje ya nchi akaanza kulia kinyachu pale hadi huruma. [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Anasema, “Gwe Kyala umalaya huu mimi basi Ee joba, ningekufa hii aibu familia yangu wangeficha wapi sura zao??”
Yaani safar za usiku ni ile tuu unakuta huezi kukwepa kwa baadhi ya Mambo yanayotusubri Ila sio nzuri kabisaa.....

Bora ata sis Dar Moshi chapu tuu tukivuka apo wami bas tena njia haina maporii na kdg imenyooka lkn usiku siwez kuapia Ila sipend kusafr kwa kutumia malori na usku [emoji16]
 
Yaani safar za usiku ni ile tuu unakuta huezi kukwepa kwa baadhi ya Mambo yanayotusubri Ila sio nzuri kabisaa.....

Bora ata sis Dar Moshi chapu tuu tukivuka apo wami bas tena njia haina maporii na kdg imenyooka lkn usiku siwez kuapia Ila sipend kusafr kwa kutumia malori na usku [emoji16]
Mimi pamoja na yote lakini sijakoma nikisikia dili la pesa nasali najikabidhi kwa Sir God mwendoo 🤣🤣
 
Back
Top Bottom