Serikali yaruhusu Mabasi ya abiria kusafiri kwa saa 24

Serikali yaruhusu Mabasi ya abiria kusafiri kwa saa 24

Safiri usiku ukiwa na shida sana lkn kama hakuna ulazima safiri mchana baadhi ya madereva ni wajinga hasa malory na hizi fuso zilizobeba Mali kuoza kutoka moshi na arusha hawapunguzi taa kuovateki ovyo speed ndio usiseme serekali ilifaa iboreshe vitendea kazi na kuanzisha strong check point ili kuwadhibiti hawa madereva wasio jielewa.
 
Kwa akili za madereva wa tanzania Watu watachinjwa sana andaeni makaburi ya kutosha
 
Mambo kadhaa makubwa.

1. Askari wa usalama barabarani itabidi wafanye kazi masaa 24, point zote za doria kwenye barabara husika, inabidi traffic wawepo muda wote.

2. Kuwe na magari ya traffic police ya road patrol, ambayo kazi yake kubwa itakuwa ni kupiga doria barabara zote zinazotumika na mabasi ya abiria.

3. Makampuni ya mabasi yawe na madereva wa kubadilishana kuepuka madereva kuchoka na kusinzia barabarani.

4. Mabasi yote yafungwe tracking devices kwaajili ya kuwa monitored na mamlaka husika.

5. Mabasi yote yafungwe radio communication equipments na yatumie channel moja ya mawasiliano, hii itawezesha mawasiliano kati ya mabasi yote endapo kutatokea changamoto yoyote maeneo ambayo hamna mawasiliano ya simu. Channel hiyo pia iwe linked na jeshi la polisi. Huu utaratibu unatumika sana Australia na hapa Tanzania kwenye kampuni za utalii.

6. Hospitali zetu zikae standby 24 hours pamoja na magari ya kubeba wagonjwa endapo kutatokea dharura zozote.

7. Basi zote zisafiri na askari mmoja mwenye silaha kubwa, kwaajili ya kukabiliana na majambazi wa barabarani usiku.

Mengine ongezeeni.
 
Hawa madereva wa bongo wakishua kula bangi na konyagi papa vichwa vinawaka.

Naomba kuanzia mwezi ujao uwekww hapa Uzi maalumu wa ajali za Barabarani na vifo usiku.

Bahati mbaya au nzuri watakaokutana na hizi ajali ni watanzania wa kawaida na sio wabunge au mawaziri.

Sasa nyie shangilieni andaeni sanda za kutosha, majeneza na vitanda vya kutosha mahospitalini.
 
Mambo kadhaa makubwa.

1. Askari wa usalama barabarani itabidi wafanye kazi masaa 24, point zote za doria kwenye barabara husika, inabidi traffic wawepo muda wote.

2. Kuwe na magari ya traffic police ya road patrol, ambayo kazi yake kubwa itakuwa ni kupiga doria barabara zote zinazotumika na mabasi ya abiria.

3. Makampuni ya mabasi yawe na madereva wa kubadilishana kuepuka madereva kuchoka na kusinzia barabarani.

4. Mabasi yote yafungwe tracking devices kwaajili ya kuwa monitored na mamlaka husika.

5. Mabasi yote yafungwe radio communication equipments na yatumie channel moja ya mawasiliano, hii itawezesha mawasiliano kati ya mabasi yote endapo kutatokea changamoto yoyote maeneo ambayo hamna mawasiliano ya simu. Channel hiyo pia iwe linked na jeshi la polisi. Huu utaratibu unatumika sana Australia na hapa Tanzania kwenye kampuni za utalii.

6. Hospitali zetu zikae standby 24 hours pamoja na magari ya kubeba wagonjwa endapo kutatokea dharura zozote.

7. Basi zote zisafiri na askari mmoja mwenye silaha kubwa, kwaajili ya kukabiliana na majambazi wa barabarani usiku.

Mengine ongezeeni.
Bongo yakifanyika haya sahau
 
Ila watanzania tupo very negative. Tunawaza mabaya tu. Mbona mabasi yameruhisiwa kusafiri saa tisa usiku na hakuna shida. Tuangalir mambo chanya sio hasi pekee.
Barabara zetu si rafiki wa mwendo kasi, barabara zote za mikoani ni "single road" ( magari yanayopishana yanapita barabara mmoja). Tusipende kupuuza maamuzi ya watangulizi wetu, nini kipya kimefanyika katika barabara za mikoani tangu miaka hiyo ambapo amri hiyo iliwekwa? Barabara zimepanuliwa? Barabara kuwekwa lami si Dawa ya madereva wasiofutwa sheria za barabarani. Magari yamefungwa "speed governor"? Ukitazama takwimu za ajali, zinakuonyesha ajali nyingi za barabarani zinatokana na uzembe wa madereva. Kulikuwa na zuio la kutembeza mabasi usiku na uzembe wa madereva bado ulitendeka, sasa ukiwaruhusu wazembe waendeshe wakati wa giza nene nini kitatokea. Kwenye mambo ya usalama wa binadamu usipende kutizama mambo kichanya chanya. Uhai na uzima wa Binadamu siyo vitu vya kuchezea chezea ili wengine wapate Faida na biashara zaidi.
 
Back
Top Bottom