Mzee wa kupambania
JF-Expert Member
- Aug 14, 2022
- 21,111
- 53,092
Madavoo wa mabasi wataziweza fujo za madavoo wa malori usiku barabarani?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Lindi sijui Katqvi huko basi zitembee masaa 24 kwa lipi haswa?
Huo ni Ushamba na Woga wa Maendeleo, nchi nyingi tu za Africa Mabus yanasafiri saa 24..Kuruhusu usafiri kwa saa 24 ni kutengeneza bomu ajali zitakuwa nyingi
Wachawi hamkosekani
Kisababishi kikubwa cha ajali barabarani ni malori. Malori yamekuwa mengi sana, halafu yapo yanayoenda mwendo wa konokono lakini mengine yanaenda mwendo panya, breki za ghafla. Changamoto wanayoipata madreva wa magari ya abiria ni kulazimika Ku overtake msululu wa malori mara wakati huo huo akiyakadria yanayokuja face to face.Hii nzuri sana kwa kwa jamii inayojali UHAI, UTU na ubinadamu.
Ila kwa akili za madreva wetu ukichanganya na ubovu wa miundombinu na Mabasi tutegemee BOMU la kupoteza ndugu, marafiki, wapendwa wetu au sisi wenyewe!
Kiufupi kali ni kifo akuna cha mpango wa Mungu au kurogana.
Mliopewa mamlaka tumieni akili zaidi kuliko hisia
Shauri zaoooKuruhusu usafiri kwa saa 24 ni kutengeneza bomu ajali zitakuwa nyingi
Yakiwakuta hakuna kuwaonea hurumaMadereva wa Tz mchana kweupe wanashindwa kufuata mwongozo wa taa za barabarani mpaka awepo askari wa usalama barabarani (trafiki), kweli watafuata sheria za barabarani usiku wa giza, hapa tunajipangia kuongeza takwimu za ajali mbaya za barabarani.
Ngoja wawaingize abiria mtaroniMadereva wa Tanzania ni wateja wakubwa wa visungura yaani vikishawakolea wanaruka ruka tu barabarani
Tomato sourceChanzo cha habari tafadhali!
Kafara zinatafutwa.
Hapo nimeelewa MkuuNi basi gani linashindana kuua watu?. Hao watakuwa sio wafanya biashara. LATRA walitoa majaribio kwa mabasi kusafiri saa tisa usiku na majaribio yalienda vizuri. Ally's na Katarama walipokiuka maagizo walifungiwa kusafiri saa tisa mpaka waliporuhuswa Tena. Sio kwamba unasafiri tu usiku, Kuna masharti unapewa.
Duuh pole aseeh...... Mm nipo ndani akn nilivosoma hii km ndo tumevamiwa[emoji1787][emoji1787][emoji1787] kuna siku nilipanda IT kutoka Dar, tukafika msamvu dereva akapakia abiria wengine wawili wote wa kiume safari ikaendelea na story nyingi.
Hapo mdada nipo peke yangu. Tulivyofika Mikumi wakatokea abiria wengine wawili nao wanaume tupu. Dereva akaingia tamaa walitaja pesa nyingi akawapakia hivyo hivyo kwa kubanana.
Mimi sikuwa na muda nao si nimekaa zangu mbele kwa dereva.
Shuhuli ilianzia tulivyozianza zile kona za Iyovi wale majamaa yaliyopakiwa Msamvu yakaanza kuongea lugha tusizozielewa. Muda huo dereva yupo speed, mbele katikati tukaona wale wakaka waliokuwa wanaongea kilugha wamechomoa MAPANGA yamenolewa kote kote yanang’aa.
Wanamwambia dereva paki gari pembeni, dereva anatetemeka panga liko shingoni mimi muda sielewi kitu nilikumbuka kusema Mungu nisaidie.
Lakini cha kushangaza wale wakaka wengine wao wametulia, nikaangalia kwenye kioo mmoja wa wale majamaa wengine anamuonyesha ishara dereva lakini sijaielewa.
Dereva akapaki gari tukashuka wote, wale majambazi wanaitaka gari na walishachorewa ramani na watu wao. Kabla hawajachukua gari tukashangaa wale wakaka wengine wanachomoa silaha za kazi [emoji23][emoji23][emoji23] woiiiih!!
Nikasema hii movie ya Damme leo naiona live.
Wakawaambia nyie wangese aliewaambia gari inaibiwa kijinga namna hii nani? Haya tupa mapanga chini kabla hatujamwaga ubongo wenu. Wakatupa zile panga yule mwenzie akazichukua, tukaambiwa we sister na suka ingiieni kwenye gari. Wale majambazi wa mapanga wakaomba basi bro tusameheane usiku saa hizi porini hapa tupeni lift mkatuache hata Ruaha Mbuyuni [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Wale majambazi wa bunduki mmoja akamuuliza dereva, “Oya suka hawa maboya wamekulipa nauli yako?” Dereva akasema hawajanilipa, akaulizwa unawadai shingapi? Akajibu, tulikubaliana elfu 60,000 wote wawili. Wakaambiwa leteni pesa hizo wakatoa lakini kwa manung’uniko. Akaambiwa oya mwanangu suka chukua pesa zako. Na nyie maboya mnabaki hapa mtajua wenyewe mnatoka vipi.
Safari ikaendelea ila hatujui hawa kina Van Damme na mwenzie Dolph tunamalizana nao vipi??
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hivi unajua mjinga mmoja barabarani anaweza kusababisha ajali hata kwa mtu mwenye akili zake timamu.Kisababishi kikubwa cha ajali barabarani ni malori. Malori yamekuwa mengi sana, halafu yapo yanayoenda mwendo wa konokono lakini mengine yanaenda mwendo panya, breki za ghafla. Changamoto wanayoipata madreva wa magari ya abiria ni kulazimika Ku overtake msululu wa malori mara wakati huo huo akiyakadria yanayokuja face to face.
Giza la usiku linaleta hatari ya kuyaparamia malori yaliyoegeshwa barabarani bila kuweka alama stahiki.
Hii sgr ikamilike tu, RAIA tutumie train, tuyaache malori yatambe barabarani.
Swala siyo kuendesha usiko bali ni muda ambao Dereva anakaa kwenye usukani. Rwanda Inalingana na mkoa wa Mororgoro ampao kutoka mpakani mpaka mpakani ni mwendo wa saa moja tu, siyo sawa na kusafiri Dar hadi Bukoba kwa masaa takriban 30.Mbona hapo Rwanda huwa tunasafiri usiku, kwanini iwe shida kwa Tanzania. Hapo Kenya tangu 1990 wanasafiri usiku mpaka Leo. Nadhani tuangalie uhitaji kuliko madhara. Halafu sio kila basi litasafiri usiku, ni baadhi tu.
Hivi unajua mjinga mmoja barabarani anaweza kusababisha ajali hata kwa mtu mwenye akili zake timamu.
Ndiyo maana nikasema safari za usiku wataua watu wengi sana chanzo inaweza kuwa hayo malori speed au barabara mbovu jumlisha magari mabovu.
uhai ukitoka harudi