Wangeanza kwa baadhi ya route fupi kama Moro - Dar, Arusha - Moshi, Tanga - Dar, Mbeya - Iringa, Lindi - Mtwara, Mwanza - Musoma n.k...
Bado kuna maeneo barabara zake sio rafiki kusafiri usiku, haswa zile ambazo hutumiwa sana na malori...
Serikali kama inatamani kuwe na uchukuzi wa watu kwa masaa 24, ilipaswa iimarishe usafiri wa njia ya reli...
Kipindi cha msimu wa mvua hasa masika, utaratibu huu wa kusafiri masaa 24 usitishwe kwa kuwa kuna baadhi ya njia si salama na hata uono wakati huu huwa hafifu...
Kwa wale wanaopenda kusafiri usiku kwa kutumia magari binafsi, huenda ukawa mwisho wa mimbio sababu kuna uwezekano trafiki wakawa wanakaa barabarani hadi mida ya popo...