Serikali yaruhusu Mabasi ya abiria kusafiri kwa saa 24

Serikali yaruhusu Mabasi ya abiria kusafiri kwa saa 24

Duuh, tuna safari ndefu sana kama watu wenyewe ndo kama wewe. Hilo kosa liko wapi!? Wanaoruhusu usafiri 24hr wanapitia changamoto zipi ambazo unahisi zitatukuta nasi? Kenya and Uganda wana utaratibu huo wa 24hrs na bado sisi tuliokuwa tunasafiri mchana tuliwazidi kwa matukio ya ajali.
Halafu sasa hapo Kenya hata tochi hakuna, na kwa gari za abiria speed limit ni 100Kmh., unatembea kutoka Nairobi to Mombasa bila hata shida., ila jamaa wanazingatia sana sheria, hutaona dereva amezidi speed 100. Shida ni hawa Madereva wetu wasipoona police barabarani wanashangilia, hapo mnaweza kudhani mnapaa.
 
Safari za usiku zinahitaji utulivu sana wa akili. Kuna watu wa malori huko barabarani muda wa kuanzia saba-hadi kumi alfajiri wengi wao huwa na fatigue hivyo kupunguza umakini.
Binafsi sipendi safari za kuzidi sita usiku.
Kwa uendeshaji wetu napenda barabara yenye askari wengi wa barabarani
 
Safari za usiku zilisimamishwa na Lyatonga akiwa waziri mambo ya ndani kwa kukurupuka bila tafiti, kabla ya hapo mabasi yote ya mikoani yalikuwa yanaanza Safari saa 12 jioni, wapo wanaoona mchana ajali za mabasi hasa kupasuka matairi ni kubwa kuliko usiku,
Changamoto ya usiku ni usingizi wa madreva, Jambo ambalo ni uzembe
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] kuna siku nilipanda IT kutoka Dar, tukafika msamvu dereva akapakia abiria wengine wawili wote wa kiume safari ikaendelea na story nyingi.
Hapo mdada nipo peke yangu. Tulivyofika Mikumi wakatokea abiria wengine wawili nao wanaume tupu. Dereva akaingia tamaa walitaja pesa nyingi akawapakia hivyo hivyo kwa kubanana.
Mimi sikuwa na muda nao si nimekaa zangu mbele kwa dereva.

Shuhuli ilianzia tulivyozianza zile kona za Iyovi wale majamaa yaliyopakiwa Msamvu yakaanza lugha tusizozielewa. Muda huo dereva yupo speed, mbele katikati tukaona wale wakaka waliokuwa wanaongea kilugha wamechomoa MAPANGA yamenolewa kote kote yanang’aa.
Wanamwambia dereva paki gari pembeni, dereva anatetemeka panga liko shingoni mimi muda sielewi kitu nilikumbuka kusema Mungu nisaidie.

Lakini cha kushangaza wale wakaka wengine wao wametulia, nikaangalia kwenye kioo mmoja wa wale majamaa wengine anamuonyesha ishara dereva lakini sijaielewa.
Dereva akapaki gari tukashuka wote, wale majambazi wanaitaka gari na walishachorewa ramani na watu wao. Kabla hawajachukua gari tukashangaa wale wakaka wengine wanachomoa silaha za kazi [emoji23][emoji23][emoji23] woiiiih!!
Nikasema hii movie ya Damme leo naiona live.

Wakawaambia nyie wangese aliewaambia gari inaibiwa kijinga namna hii nani? Haya tupa mapanga chini kabla hatujamwaga ubongo wenu. Wakatupa zile panga yule mwenzie akazichukua, tukaambiwa we sister na suka ingiieni kwenye gari. Wale majambazi wa mapanga wakaomba basi bro tusameheane usiku saa hizi porini hapa tupeni lift mkatuache hata Ruaha Mbuyuni [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Wale majambazi wa bunduki mmoja akamuuliza dereva, “Oya suka hawa maboya wamekulipa nauli yako?” Dereva akasema hawajanilipa, akaulizwa unawadai shingapi? Akajibu, tulikubaliana elfu 60,000 wote wawili. Wakaambiwa leteni pesa hizo wakatoa lakini kwa manung’uniko. Akaambiwa oya mwanangu suka chukua pesa zako. Na nyie maboya mnabaki hapa mtajua wenyewe mnatoka vipi.

Safari ikaendelea ila hatujui hawa kina Van Damme na mwenzie Dolph tunamalizana nao vipi??
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
We inabidi nikukutanishe na jb una kitu maana picha umelimaliza kibabe kama mel gibson 😄
 
Hongera kwa uamuzi huu!

Fikiria ATM isingekuwa saa 24!!!

Tumechelewa sana,ni vyema uchumi uzunguke kwa saa 24.(kama ATM za benki)

Mauzo ya mafuta saa 24,wanaouza chakula na shughuli mbalimbali watakuwa wapo saa 24.uchumi na ajira itaongezeka.

Usafiri usiku ni sawa na mwenye kiwanda awe na uzalishaji wa bidhaa mara 2 kwani bidhaa zitazalishwa mchana na usiku.

Mataifa yaliyotuzidi kiuchumi wana itaratibu huu wa shughuli za uchumi kuwa saa 24

Wananchi wakubali na waelewe utaratibu ulikuwepo na maisha yaliendelea kama kawaida!!
 
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeruhusu Mabasi ya abiria kufanya usafirishaji wa Saa 24, baaada ya kujiridhisha kiusalama, mwamko wa wananchi, huduma za mawasiliano pamoja na miundombinu ya usafirishaji.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Nchi, Jumanne Sagini wakati anaongea na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na kusema kuwa wamefikia maamuzi hayo baada ya Serikali kuimarisha shughuli za uchumi wa wananchi wake wa maeneo ya mjini na Vijijini.

Akiongeza kuwa wamezingatia maoni ya Wadau mbalimbali wakiwemo Wabunge, wamiliki wa mabasi, madereva wa mabasi, wasafiri, Wafanyabiashara na Wananchi kwa ujumla.

Aidha, Serikali imetoa maagizo kwa wadau wote wa usafirishaji kuzingatia Sheria, Kanuni na utaratibu wa leseni zao.

Pia madereva wametakiwa kuthibitishwa na LATRA, ambayo itatoa ratiba za safari kwa saa 24, TANROADS kuhakikisha ubora wa miundombinu, Serikali za Mitaa kuhakikisha zinasimamia usalama wa abiria kwenye huduma wanazosimamia pamoja na Jeshi la Polisi kusimamia Usalama wa watu na mali zao.
Mungu atunusuru
 
Madereva wa Tz mchana kweupe wanashindwa kufuata mwongozo wa taa za barabarani mpaka awepo askari wa usalama barabarani (trafiki), kweli watafuata sheria za barabarani usiku wa giza, hapa tunajipangia kuongeza takwimu za ajali mbaya za barabarani.
Umemsikia Mkurugenzi wa LATRA?. Wamesema watatoka utaratibu wa jinsi ya kusafiri.
 
Back
Top Bottom