Serikali yaruhusu Mabasi ya abiria kusafiri kwa saa 24

Serikali yaruhusu Mabasi ya abiria kusafiri kwa saa 24

Wale madereva wa malori wenye bifu na madereva wa mabus ambao wakiona bus inamuovertake alaf mbele kuna gari inakuja na yeye anaongeza mwendo waache hizo mambo ili ajali za uso kwa uso zisiwe nyingi maana usiku ndo hatari zaidi
Watakufa wengi kwa mabifu ya madereva plus uzembe
 
Miaka ya 80 safari zilikuwa zikifanywa usiku na mchana. Safari zikianza saa 12 jioni, usiku mzima uko safarini unafika asubuhi yake. Kenya pia safari zao zinaanza kati ya saa 12 jioni safari ya usiku mzima. Kwa Tanzania nakumbuka safari za Dar es salaam -Songea mabasi ya Kamata yalianza saa 12 jioni..... Arusha/Moshi-Dar es salaam pia zilianza saa 12 jioni.
Nchi jirani ya Kenya safari kutoka Rodwar kwenda Kitale zilianza saa nne usiku ! Nairobi-Dar es salaam hivyo hivyo. Sijui ni kwa nini nchi iliugua kiharusi hadi kuzuia safari za usiku kwa miaka yote hiyo?. 😳
 
Wangeanza kwa baadhi ya route fupi kama Moro - Dar, Arusha - Moshi, Tanga - Dar, Mbeya - Iringa, Lindi - Mtwara, Mwanza - Musoma n.k...

Bado kuna maeneo barabara zake sio rafiki kusafiri usiku, haswa zile ambazo hutumiwa sana na malori...

Serikali kama inatamani kuwe na uchukuzi wa watu kwa masaa 24, ilipaswa iimarishe usafiri wa njia ya reli...

Kipindi cha msimu wa mvua hasa masika, utaratibu huu wa kusafiri masaa 24 usitishwe kwa kuwa kuna baadhi ya njia si salama na hata uono wakati huu huwa hafifu...

Kwa wale wanaopenda kusafiri usiku kwa kutumia magari binafsi, huenda ukawa mwisho wa mimbio sababu kuna uwezekano trafiki wakawa wanakaa barabarani hadi mida ya popo...
Hizo route fupi ulizotaja sidhani hata kama wanahitaji hizi safari za usiku, hapa walengwa ni mikoa ya mbali (Dar - Kigoma, Dar - Mwanza, Dar - Kagera, Dom - Mwanza n.k)
Wazo ni zuri sana, muhimu ni tutoe maoni ya kuboresha na si kusitisha.
 
Mabasi ya Arusha-Kigoma yajiandae kutekwa kwenye msitu wa malagarasi.

Alafu Kampuni za Coast Line na Kiazi Kitamu mnakabidhi Basi kwa dereva mmoja kuendesha umbali mrefu kiasi hicho, tujiandae kuona mengi.
Mabasi ambayo kwa ratiba ya sasa yangepita kwenye misitu usiku yataweka ratiba itakayoyawezesha kupit maeneo hayo mchana.
Mfano iwapo lilikuwa linatoka Arusha alfajiri na kufika Malagarasi saa 5 usiku, sasa yatatoka Arusha jioni au usiku ili yafike Malagarasi asubuhi.
Hii ina.maana kuwa kila kampuni itapanga ratiba inayokwenda kwa.mazingira yanayowasaidia Abiria na kampuni husika.
 
Mabasi ambayo kwa ratiba ya sasa yangepita kwenye misitu usiku yataweka ratiba itakayoyawezesha kupit maeneo hayo mchana.
Mfano iwapo lilikuwa linatoka Arusha alfajiri na kufika Malagarasi saa 5 usiku, sasa yatatoka Arusha jioni au usiku ili yafike Malagarasi asubuhi.
Hii ina.maana kuwa kila kampuni itapanga ratiba inayokwenda kwa.mazingira yanayowasaidia Abiria na kampuni husika.
Very reasonable practice
 
Kwani wanaosafiri mchana hawawezi kupata ajali? Mbona Majirani (Kenya & UG) wanasafiri 24hrs na bado wana matukio machache ya ajali kuliko sisi wasafiri mchana!?
Safisha ubongo huo utoke nje ya box.
Una uhakika miundombinu ya Barabara za UG & Kenya ni sawa sawa na hii miundombinu ya Barabara za Tz?

Una uhakika ustaarabu wa madereva wa UG & KE ndio huo huo wa madereva wa TZ wanaoishi kwa mabifu Kati ya madereva wa malori na wenye mabus Kati ya wenye mabus na bodaboda & bajaj?
 
Back
Top Bottom