Serikali yaruhusu Mabasi ya abiria kusafiri kwa saa 24

Serikali yaruhusu Mabasi ya abiria kusafiri kwa saa 24

Wangeanza kwa baadhi ya route fupi kama Moro - Dar, Arusha - Moshi, Tanga - Dar, Mbeya - Iringa, Lindi - Mtwara, Mwanza - Musoma n.k...

Bado kuna maeneo barabara zake sio rafiki kusafiri usiku, haswa zile ambazo hutumiwa sana na malori...

Serikali kama inatamani kuwe na uchukuzi wa watu kwa masaa 24, ilipaswa iimarishe usafiri wa njia ya reli...

Kipindi cha msimu wa mvua hasa masika, utaratibu huu wa kusafiri masaa 24 usitishwe kwa kuwa kuna baadhi ya njia si salama na hata uono wakati huu huwa hafifu...

Kwa wale wanaopenda kusafiri usiku kwa kutumia magari binafsi, huenda ukawa mwisho wa mimbio sababu kuna uwezekano trafiki wakawa wanakaa barabarani hadi mida ya popo...
Tayari Kilimanjaro Express ana route hiyo kitambo, anatoka Dar saa 4 Usiku kwenda Arusha
 
Nyie ambao mnapinga hilo jambo na kuanza kusema mambo ya ajali na vifo hivi hamuwezi kua na mawazo yoyote chanya yakufanya mabadiliko ya mambo kwenye hii nchi hadi tuendelee kuishi kama babu zetu wa miaka mingi iliyopita?.Ni lini tutabadilisha vichwa vyetu ili tukimbizane na dunia badala yakuwaza mabaya tu.Ni lini tutafika level za wenzetu ikiwa ata hili dogo linatushinda.Ni lini miundombinu yetu itakua bora kama hatutaki kuitumia kwenye nyakati ngumu,ni lini madereva wetu watakua smart.
 
Una uhakika miundombinu ya Barabara za UG & Kenya ni sawa sawa na hii miundombinu ya Barabara za Tz?

Una uhakika ustaarabu wa madereva wa UG & KE ndio huo huo wa madereva wa TZ wanaoishi kwa mabifu Kati ya madereva wa malori na wenye mabus Kati ya wenye mabus na bodaboda & bajaj?
Miundombinu ya nchi zote EA haina tofauti na tena kwa barabara za kuunganisha mikoa Tanzania imepiga hatua kubwa kuliko majirani.
 
Miundombinu ya nchi zote EA haina tofauti na tena kwa barabara za kuunganisha mikoa Tanzania imepiga hatua kubwa kuliko majirani.
Yaan unataka kusema Barabara za KE hazina utofauti na Barabara za TZ?

Basi subiria takwimu si zitaandikwa hapa hapa JF tu
 
Mabasi ya Arusha-Kigoma yajiandae kutekwa kwenye msitu wa malagarasi.

Alafu Kampuni za Coast Line na Kiazi Kitamu mnakabidhi Basi kwa dereva mmoja kuendesha umbali mrefu kiasi hicho, tujiandae kuona mengi.
Sheria za kuendesha magari makubwa bado sana huko
Wenzetu kila masaa 4.5 lazima dereva apumzike dakika 45 na akiendesha tena anaweza kupumzika mda kwa dakika 15 halafu tena 30 na kuwa dakika 45 tena
Kwa hiyo anakuwa ameendesha masaa 9 na kipumzika pia
Ila huko ni mwendo wa kukimbiza tu
 
Sipatii picha bus linapita kitonga usiku na sehemu kama hizo

[emoji1787][emoji1787][emoji1787] kuna siku nilipanda IT kutoka Dar, tukafika msamvu dereva akapakia abiria wengine wawili wote wa kiume safari ikaendelea na story nyingi.
Hapo mdada nipo peke yangu. Tulivyofika Mikumi wakatokea abiria wengine wawili nao wanaume tupu. Dereva akaingia tamaa walitaja pesa nyingi akawapakia hivyo hivyo kwa kubanana.
Mimi sikuwa na muda nao si nimekaa zangu mbele kwa dereva.

Shuhuli ilianzia tulivyozianza zile kona za Iyovi wale majamaa yaliyopakiwa Msamvu yakaanza kuongea lugha tusizozielewa. Muda huo dereva yupo speed, mbele katikati tukaona wale wakaka waliokuwa wanaongea kilugha wamechomoa MAPANGA yamenolewa kote kote yanang’aa.
Wanamwambia dereva paki gari pembeni, dereva anatetemeka panga liko shingoni mimi muda sielewi kitu nilikumbuka kusema Mungu nisaidie.

Lakini cha kushangaza wale wakaka wengine wao wametulia, nikaangalia kwenye kioo mmoja wa wale majamaa wengine anamuonyesha ishara dereva lakini sijaielewa.
Dereva akapaki gari tukashuka wote, wale majambazi wanaitaka gari na walishachorewa ramani na watu wao. Kabla hawajachukua gari tukashangaa wale wakaka wengine wanachomoa silaha za kazi [emoji23][emoji23][emoji23] woiiiih!!
Nikasema hii movie ya Damme leo naiona live.

Wakawaambia nyie wangese aliewaambia gari inaibiwa kijinga namna hii nani? Haya tupa mapanga chini kabla hatujamwaga ubongo wenu. Wakatupa zile panga yule mwenzie akazichukua, tukaambiwa we sister na suka ingiieni kwenye gari. Wale majambazi wa mapanga wakaomba basi bro tusameheane usiku saa hizi porini hapa tupeni lift mkatuache hata Ruaha Mbuyuni [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Wale majambazi wa bunduki mmoja akamuuliza dereva, “Oya suka hawa maboya wamekulipa nauli yako?” Dereva akasema hawajanilipa, akaulizwa unawadai shingapi? Akajibu, tulikubaliana elfu 60,000 wote wawili. Wakaambiwa leteni pesa hizo wakatoa lakini kwa manung’uniko. Akaambiwa oya mwanangu suka chukua pesa zako. Na nyie maboya mnabaki hapa mtajua wenyewe mnatoka vipi.

Safari ikaendelea ila hatujui hawa kina Van Damme na mwenzie Dolph tunamalizana nao vipi??
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom