Serikali yaruhusu Mabasi ya abiria kusafiri kwa saa 24

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeruhusu Mabasi ya abiria kufanya usafirishaji wa Saa 24, baaada ya kujiridhisha kiusalama, mwamko wa wananchi, huduma za mawasiliano pamoja na miundombinu ya usafirishaji.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Nchi, Jumanne Sagini wakati anaongea na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na kusema kuwa wamefikia maamuzi hayo baada ya Serikali kuimarisha shughuli za uchumi wa wananchi wake wa maeneo ya mjini na Vijijini.

Akiongeza kuwa wamezingatia maoni ya Wadau mbalimbali wakiwemo Wabunge, wamiliki wa mabasi, madereva wa mabasi, wasafiri, Wafanyabiashara na Wananchi kwa ujumla.

Aidha, Serikali imetoa maagizo kwa wadau wote wa usafirishaji kuzingatia Sheria, Kanuni na utaratibu wa leseni zao.

Pia madereva wametakiwa kuthibitishwa na LATRA, ambayo itatoa ratiba za safari kwa saa 24, TANROADS kuhakikisha ubora wa miundombinu, Serikali za Mitaa kuhakikisha zinasimamia usalama wa abiria kwenye huduma wanazosimamia pamoja na Jeshi la Polisi kusimamia Usalama wa watu na mali zao.K
Isiishe tu kwenye mabasi Bali nchi nzima ifanye kazi 24/7 Na tuone nani atasema ajira hakuna.
Hata serikali- mihimili yote iwe 24/7 Na tuone Kama kweli ajira hakuna ...
 
Sijui waliwaza nini katila hili au kwa kuwa wao wanapanda magari ya serikali pamoja na ndugu zao. Hivi unashuka kitonga na kupita zile kina za Iyovi usiku kisa nini?

Tatizo tunalaumu bila kusikiliza walichosema Leo. LATRA wamesema mabasi yatapewa utaratibu wa kusafiri usiku kabla ya kuanza Hilo zoezi. Tusubiri.
 
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeruhusu Mabasi ya abiria kufanya usafirishaji wa Saa 24, baaada ya kujiridhisha kiusalama, mwamko wa wananchi, huduma za mawasiliano pamoja na miundombinu ya usafirishaji.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Nchi, Jumanne Sagini wakati anaongea na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na kusema kuwa wamefikia maamuzi hayo baada ya Serikali kuimarisha shughuli za uchumi wa wananchi wake wa maeneo ya mjini na Vijijini.

Akiongeza kuwa wamezingatia maoni ya Wadau mbalimbali wakiwemo Wabunge, wamiliki wa mabasi, madereva wa mabasi, wasafiri, Wafanyabiashara na Wananchi kwa ujumla.

Aidha, Serikali imetoa maagizo kwa wadau wote wa usafirishaji kuzingatia Sheria, Kanuni na utaratibu wa leseni zao.

Pia madereva wametakiwa kuthibitishwa na LATRA, ambayo itatoa ratiba za safari kwa saa 24, TANROADS kuhakikisha ubora wa miundombinu, Serikali za Mitaa kuhakikisha zinasimamia usalama wa abiria kwenye huduma wanazosimamia pamoja na Jeshi la Polisi kusimamia Usalama wa watu na mali zao.
Jana nmetoka arusha nmepishana na mabasi kadhaa usiku lakini pia nmekutana na barier za police zaid ya 7 usiku. Kuna jamaa tulimuacha njiapanda ya tanga pale akaambiwa ataondoka asubuh sabab gari yake ilikuwa inawaka taa 1
 
huo ni ushamba; iirani Kenya mbona mabasi ni 24 hrs na hakuna tatizo
Hakuna ushamba tunatoa mapendekezo in advance issue sio miundombinu issue madereva unawajua vizuri Juzi nilikua natoka nje ya mji naingia ndani ya mji dereva alikua anapeperusha Gari km kabeba matenga ya nyanya kuna Mama alikua amekaa nyuma alilia kwa sauti kuu 'dereva usidhani umebeba maparachichi' sasa wakiruhusu usiku unadhani nini kinachofuata wakati mchana kweupe wanafanya wanayoyafanya na huyo anafanya hivyo anaendesha Costa hapo hujagusa wenye malori ya Mbao na mizigo mingine, hivi ajali ya mwisho hapo majuzi imeua watu wangapi km kweli wewe ni mfuatiliaji na unajua chanzo Cha ajali?
 
Isiishe tu kwenye mabasi Bali nchi nzima ifanye kazi 24/7 Na tuone nani atasema ajira hakuna.
Hata serikali- mihimili yote iwe 24/7 Na tuone Kama kweli ajira hakuna ...

Maendeleo huwa yanaanza polepole. Usafiri wa usiku utazalisha ajira nyingi.
 
Hakuna ushamba tunatoa mapendekezo in advance issue sio miundombinu issue madereva unawajua vizuri Juzi nilikua natoka nje ya mji naingia ndani ya mji dereva alikua anapeperusha Gari km kabeba matenga ya nyanya kuna Mama alikua amekaa nyuma alilia kwa sauti kuu 'dereva usidhani umebeba maparachichi' sasa wakiruhusu usiku unadhani nini kinachofuata wakati mchana kweupe wanafanya wanayoyafanya na huyo anafanya hivyo anaendesha Costa hapo hujagusa wenye malori ya Mbao na mizigo mingine, hivi ajali ya mwisho hapo majuzi imeua watu wangapi km kweli wewe ni mfuatiliaji na unajua chanzo Cha ajali?

Wameruhusu mabasi saa tisa usiku na ajali hazikuwepo muda huo, hivyo wameruhusu baada ya kuona majaribio yameenda vizuri.
 
Hakuna ushamba tunatoa mapendekezo in advance issue sio miundombinu issue madereva unawajua vizuri Juzi nilikua natoka nje ya mji naingia ndani ya mji dereva alikua anapeperusha Gari km kabeba matenga ya nyanya kuna Mama alikua amekaa nyuma alilia kwa sauti kuu 'dereva usidhani umebeba maparachichi' sasa wakiruhusu usiku unadhani nini kinachofuata wakati mchana kweupe wanafanya wanayoyafanya na huyo anafanya hivyo anaendesha Costa hapo hujagusa wenye malori ya Mbao na mizigo mingine, hivi ajali ya mwisho hapo majuzi imeua watu wangapi km kweli wewe ni mfuatiliaji na unajua chanzo Cha ajali?
Hujanipata point yangu; kwa nini wenzetu wanaliweza hili mfano hapo Kenya.
 
Kama naona mashindano ya kuuwa watu uso kwa uso
Kama wataacha speed kali huku wala rushwa nao wakasema basi tunalinda roho za watu badala ya matumbo mbona itakuwa poa sana

Ni basi gani linashindana kuua watu?. Hao watakuwa sio wafanya biashara. LATRA walitoa majaribio kwa mabasi kusafiri saa tisa usiku na majaribio yalienda vizuri. Ally's na Katarama walipokiuka maagizo walifungiwa kusafiri saa tisa mpaka waliporuhuswa Tena. Sio kwamba unasafiri tu usiku, Kuna masharti unapewa.
 
Mabasi ambayo kwa ratiba ya sasa yangepita kwenye misitu usiku yataweka ratiba itakayoyawezesha kupit maeneo hayo mchana.
Mfano iwapo lilikuwa linatoka Arusha alfajiri na kufika Malagarasi saa 5 usiku, sasa yatatoka Arusha jioni au usiku ili yafike Malagarasi asubuhi.
Hii ina.maana kuwa kila kampuni itapanga ratiba inayokwenda kwa.mazingira yanayowasaidia Abiria na kampuni husika.

Safi Sana. Haya ndio maelezo yanayotekelezeka. Sio kuwaza ajali tu.
 
Back
Top Bottom