Mambo kadhaa makubwa.
1. Askari wa usalama barabarani itabidi wafanye kazi masaa 24, point zote za doria kwenye barabara husika, inabidi traffic wawepo muda wote.
2. Kuwe na magari ya traffic police ya road patrol, ambayo kazi yake kubwa itakuwa ni kupiga doria barabara zote zinazotumika na mabasi ya abiria.
3. Makampuni ya mabasi yawe na madereva wa kubadilishana kuepuka madereva kuchoka na kusinzia barabarani.
4. Mabasi yote yafungwe tracking devices kwaajili ya kuwa monitored na mamlaka husika.
5. Mabasi yote yafungwe radio communication equipments na yatumie channel moja ya mawasiliano, hii itawezesha mawasiliano kati ya mabasi yote endapo kutatokea changamoto yoyote maeneo ambayo hamna mawasiliano ya simu. Channel hiyo pia iwe linked na jeshi la polisi. Huu utaratibu unatumika sana Australia na hapa Tanzania kwenye kampuni za utalii.
6. Hospitali zetu zikae standby 24 hours pamoja na magari ya kubeba wagonjwa endapo kutatokea dharura zozote.
7. Basi zote zisafiri na askari mmoja mwenye silaha kubwa, kwaajili ya kukabiliana na majambazi wa barabarani usiku.
Mengine ongezeeni.