Serikali yashinda rufaa, Wakurugenzi kuendelea kusimamia chaguzi

Watu yawapasa kujua kuwa tuna mahakama za kisheria (courts of law) siyo mahakama za haki (courts of justice ). Kwa hiyo watu watofautishe hilo. Ukitaka court of justice nenda The Hague utaikuta ICJ, au Arusha utaikuta EACJ.

Mahakama ime-propound na ku-uphold what the law "is"? What does the law say? siyo where is justice? What "ought" to be?

Sasa kama upande wa wakatiwa rufaa wameshindwa kuithibitishia mahakama kuwa viapo vinavyoliwa na hao wakurugenzi kuwa ni batili au havipo, mahakama itapindua sheria kirahisi?
 
Serikali ya CCM na Magufuli imewekeza sana kubakia madarakani kuliko kulinda maslahi ya nchi. Kesi za IPTL na mikataba mibovu inayosainiwa na wanaCCM hatushindi. Ila kesi uchwara za ndani serikali inashindishwa kirahisi sana.
AIBU SANA
 
Haki imetendeka na mahakama imetenda haki kabisa...
Wasio ridhishwa na maamuzi ya mahakama wakakate rufaa
 
Kwa utawala huu mahakama kitanda haki ni ndoto. Magufuli ndie anayeamua nano afungwe, nani aachiwe, nano apewe dhamani. Hao majaji sijui mahakama wapo kama mambo tu. Yaani ni waoga, yote yanatokana na kulinda kula zao.
 
Hii ni habari Njema sana kwa watanzania Wote hasa wapenda mabadiliko ya kweli!!!!!
 
Mahakama na siasa.
Ujinga jinga tu asa kama ni hivo mnaoenda piga kura kutafta nini?
Kiongozi atatangazwa tu.
 
Mahakama za Tanzania haziaminiki, tupeleke kesi mahakama ya Africa Mashariki
Unaujua mfumo wa utekelezaji wa hukumu zitokanazo na Mahakama ya Africa Mashariki kwenye kesi zitokazo kwenye nchi mwanachama wa EAC?

White elephant yet.
 
Unaujua mfumo wa utekelezaji wa hukumu zitokanazo na Mahakama ya Africa Mashariki kwenye kesi zitokazo kwenye nchi mwanachama wa EAC?

White elephant yet.
Tikimbilie wapi sasa, mahakama zetu kama ndo hizi? hata common sense ya mtoto mdogo wa darasa la kwanza anajua siyo haki
 
Hakuna kitu kinaitwa uchaguzi Tanzania, ni mfano wa uchaguzi, mahakama imesimamia maamuzi ya CCM kuwarudisha wana CCM kwenye uchaguzi wa vyama vingi yaani CCM wasimamie chaguzi za vyama vingi.

Mahakama nayo ipo chini ya CCM???

Kwani kuna haja gani tena ya kua na chaguzi Tanzania?

Tume ipo chini ya mwenyekiti CCM, mkurugenzi wake CCM. Wasimamizi wake nchini ni CCM.

Uchaguzi Tanzania ni mchezo wa kuigiza
 
Tumekwisha! Ibrahim Juma umeandika historia!
 
Nimeipenda hii mkuu, akiumwa na njaa atamla tu!
Huyo jamaa akiulizwa kati ya fisi na wakurugenzi(binadamu) yupi mwenye utashi? I.e. yaani mwenye Silka au hulka?

Lazima hata ukimwambia judge hiyo scenario ya fisi na mbuzi(ambao ni wanyama (not rational)) ukifananisha na kesi ya wakurugenzi (ambao ni binadamu (rational)) na uchaguzi, kama huyo jaji atafuata kanuni za logic ya syllogism atakuuliza kama nilivyouliza hapo juu.

Huwezi kufanya reasoning ya hivyo kama unajua the mechanism of logic of syllogism and its power in decision(judgment) making (in this case) for judges or magistrates and counsel.

Wakurugenzi wanautashi; na sheria inasisitiza (hata majaji wanajua) kuwa mtu anapoapa anajua maana ya kiapo chake na matokeo ya kiapo hicho, labda kama ni mwehu, mtoto mchanga, au vinginevyo. Hivyo mkurugenzi akiapa kukana uchama anawajibika kwenye kiapo chake.

Next, and this is ridiculous. Ha haaa. Fisi hawezi kuapa maana hana huo uwezo kiasilia. Hivyo hata akiapa (purportedly) kutokula mbuzi na baada ya hiyo purported swearing au affirmation, ukamchanganya na mbuzi zizini lazima tu atawala hao mbuzi bila hata kushangaa. Labda kama awe ni mwehu, mtoto mchanga sana au vinginevyo. Na hatowajibika kwa kiapo chake bali tu kwa kula mbuzi.
 
Kwa hali halisi ilivyo majaji wanaweza kusema eti mtu kala kiapo hivyo anaaminika kwa kula kiapo. Hapo sioni kama kuna haja tena ya umma kuendelea kutulia. Hapa bila nguvu ya umma na taifa letu kuanza upya sioni kama tutatoboa.
 
Unapotosha
Mahakama imetafisiri kuna hatua ya kula kiapo ya kutokuwa na chama kabla ya kuteuliwa kuwa msimamizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…