Serikali yashinda rufaa, Wakurugenzi kuendelea kusimamia chaguzi

Serikali yashinda rufaa, Wakurugenzi kuendelea kusimamia chaguzi

Halafu mnalazimisha watu kujiandikisha. Labda siku ya uchaguzi mtufuate majumbani. Kwa mtindo huu wa Mahakama zetu haki imekuwa ndiyo hivyo tena labda Mola atende miujiza.
 
Hivi ikiwa watu wanakula kiapo mahakamani cha kusema ukweli, na bado wanakana mashtaka ambayo kimsingi ni ya kweli, itakuwa kwa hawa wa kukana uanachama! Sijui ngoja tusubiri tuone. Matokeo ya uchaguzi yatasema.
 
Hapo ndio rasmi hatutapiga kura bali itabidi tutafute njia mbadala ya kupata viongozi nje ya box la kura. Mahakama imeshindwa wajibu wake, hivyo umma utatumia nguvu yake kuhakikisha haki yake haipotei.
Hautapiga ww na familia yako,usiwasemee wengine
 
Kuna haja ya kukinukisha aisee hii nchi imeingiliwa.
 
Ina maana Singa Singa akila kiapo cha kukana makosa yake atashinda kesi pia! Jee baada ya uchaguzi watakula kiapo tena kurejesha uwanachama wao au kiapo kinabakia vile vile. Kiapo hakibadilishi uhalisia. Mimi nikila kiapo kuwa ni Mmarekani jee mahakama itakubali kuwa mimi ni Mmarekani?

Hapa ni patamu sana tena sana. Hicho kiapo kina limitation! Kwa sababu sijawahi kumuona au kusikia DED anatenguwa kiapo na kurejea kuwa mwanachama tena!

Na kama hawa wasimamizi wa uchaguzi watakuja kugombea nafasi kwenye chama siku za mbele, jee wanaweza kupingwa on the basis kwamba waliukana uwanachama wao na hawaku reverse kiapo baada ya uchaguzi!
 
Kosa lililofanywa na waliofungua hii kesi na mawakili wao, walifungua kwa lengo la kupambana na CCM na si mfumo. Hata waliposhinda kesi Mahakama Kuu walishangilia kwa kuishinda CCM.
Wangelenga ktk mfumo kungekuwa na kujenga hoja ya kuwapo uwezekano wa kuwapata wasimamizi wa uchaguzi wasio wanachama wala wapenzi wa vyama katika mfumo huu wa vyama vingi.

Walisahau kuwa kiapo ni utaratibu unaowezesha muapaji kuwajibika kwa makosa aliyofanya kwa kutozingatia kiapo. Kuna wabunge, mawaziri, madiwani, wenyeviti wa serikali za mitaa toka upinzani hawatiliwi mashaka kufanya kazi chini ya serikali ya chama kilichopo madarakani sababu wameapishwa kabla ya kuanza kazi na kuenenda kinyume chake ni uhaini.

Lakini pia walijikita zaidi na mistari ya katiba wakiacha SHERIA na KANUNI nyingine za Uchaguzi zinazoelekeza nini kifanyike ktk utendaji wa tume ya uchaguzi.
 
Nawashangaa sana viongozi wa vyama vya upinzani kuendelea kuota ndoto za mchana eti kuna siku watashinda.

Kiongozi wa chama cha upinzani anayehamasisha watu kuoiga kura bafala ya kuhamasisha watu kudai katiba mpya, kwangu mimi, huyo ni mbabaishaji ambaye kauli yake haistahili kupewa uzito wowote na watu wanaoitakia mema nchi yetu.

Tidai katiba mpya kwaajili ya Tanzania mpya.
 
Hatupingi mipango ya Mungu wala kuikosoa. Lakini tunaweza kumuuliza Mungu kwa nini kizazi cha kina Kapt Hatty Macghee, Lt. Eugene Maganga, Kapt.Komando, Kapt Hanspoppe, nk nk hakukiacha na kukileta wakati huu? Kama wale waliweza kukaa na kuhoji falsafa za Mwalimu ambazo alikuwa amekwisha jijengea jina kubwa sio TZ na Afrika tuu, bali duniani kote jee wangeshindwa sasa kuhoji na kuchukua hatua?
Utawala huu wa sasa hauwezi kutolewa kwa kutumia mbinu za kizazi cha kina Mbowe, Zitto, Mbatia,Heche, Chakaza, Retired, Salary Slip nk maana kwao masikio yametoboka haya maneno matupu yanaingia huku na kutokea huku. Bali kizazi kile hawakuwa wanaandaa maneno matupu bali na viboko ukiwa sugu kusikia.
Niliwahi kusema Mbowe ni Sehemu ya CCM tangu utoto.
Hakuna Mageuzi yatakayoletwa chini ya watu kama Mbowe.
Ubunifu ziro.


Ni kama hakuna Wapinza ni kwa sasa Bali watu Jasiri kama Fatima Karume ,Lisu ,Askofu Dr. Bagonza, Bernard Membe n.k.

Kwa hiyo ni vyema vyama vingi vikafutwa ili vijekuanza kwa mbinu itakayotikana na jamii yenyewe wakati huo China na Korea itakua ina mfumo mzuri wa vyama vingi na sisi tutakua tunapigana kutafuta vyama vingi.Mana kizazi kijacho hakitakua salama chini ya Watawala wasiojali haki na Uhuru wa Mawazo.

Mbowe ,Lipumba,Cheyo,Mrema n.k. Wamengangania vyama mpaka vimekufa.
Mabadiliko yaanzie ndani ya vyama kwanza.
Haki na uhuru wa kuchagua uanze kuonekana ndani ya vyama. Vinginevyo tusubiri hao wenye vyama watakapoozeeka na kushindwa kutembe kabisa ndio watoe ruhusa ya kuchaguliwa wengine
 
Kwa kufanya hivo wanazidi kuimalisha upinzani usiokuwa na mtu wa kuwaongoza.
 
Ipo haja ya kuingia msituni,kukata gogo. Kama unaungana na mawazo haya " gonga likes"
 
Tofauti ya mfumo na CCM ni nini?

Ni nani aliye-design huo mfumo,
Kosa lililofanywa na waliofungua hii kesi na mawakili wao, walifungua kwa lengo la kupambana na CCM na si mfumo. Hata waliposhinda kesi Mahakama Kuu walishangilia kwa kuishinda CCM.
Wangelenga ktk mfumo kungekuwa na kujenga hoja ya kuwapo uwezekano wa kuwapata wasimamizi wa uchaguzi wasio wanachama wala wapenzi wa vyama katika mfumo huu wa vyama vingi.

Walisahau kuwa kiapo ni utaratibu unaowezesha muapaji kuwajibika kwa makosa aliyofanya kwa kutozingatia kiapo. Kuna wabunge, mawaziri, madiwani, wenyeviti wa serikali za mitaa toka upinzani hawatiliwi mashaka kufanya kazi chini ya serikali ya chama kilichopo madarakani sababu wameapishwa kabla ya kuanza kazi na kuenenda kinyume chake ni uhaini.

Lakini pia walijikita zaidi na mistari ya katiba wakiacha SHERIA na KANUNI nyingine za Uchaguzi zinazoelekeza nini kifanyike ktk utendaji wa tume ya uchaguzi.
 
Safi Sana !kiapo kinakubalika kisheria, haohao wakurugenzi mbona waliwapekeka wapinzani bungeni Sasa hivi iwe nongwa kwa nini! Acheni deko upinzani tafteni agenda zenye maana wananchi wawaelewe zaidi ya hapo chaguzi zote mtakuwa watu wa kulialia kila siku
Hv huwaga mnajitoa ufahamu au hao wabunge unaosema walipelekwa na wakurugenzi uliona lkn mpaka utangazwaji wake ulikuaje ni kwa mbinde mfano shinyanga mbele ya macho yangu marehemu shilembi mgombea wa cdm kaongoza vituo vyote watu wanaenda wanajua yeye ndo anatangazwa mkurugenz kajivutavuta mpaka saa nane usiku akaja kupindua meza hapo hapo kura za majumuisho zote zimehasibiwa na watu wakasaini kabsa mshindi ni jamaa wa cdm ile mkurugenz kutoka nje kushika mike anatangaza akapindua et maselle kashinda kwa kura moja ndo maana hatutaki ma DED wawe wasimamizi na afadhal jk alikuwa mstaarabu kidogo huyu wa sasa je
 
Back
Top Bottom