Serikali yasitisha Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Kuimarisha Bandari za Mtwara, Dar

Status
Not open for further replies.
Nyie watu mna vituko sana! Kwamba kwa miaka 40 hatungekuwa na mapato yahusuyo bandari, unazungumzia mapato yapi hasa? Hivi umeshawahi kujiuliza hiyo bandari ingekuwa na uwezo wa kuhudumia mzigo kiasi gani na kodi ingekusanywa kwa kiasi gani? Au ndo unataka kusema na hiyo kodi ingechukuliwa na Wachina?

Halafu kwanini unasema bandari ya Dar es salaam ingesimama na kuhoji ikijengwa Bandari ya Bagamoyo halafu ya Dar ipelekwe wapi!!! Are you serious?! Yaani ndo ushaona tutakuwa ni mibandari mikubwa mikubwa mingi?! Kenya tu hapo, wana mradi mkubwa sana kama ule wa Bagamoyo ambapo wao wanataka kujenga bandari nyingine kubwa zaidi kule Lamu! Kwahiyo unataka kusema bandari ya Mombasa wataipeleka wapi? Hivi we unadhani kuna banadari hapa zaidi tu kwavile kuna umasikini wa kutisha kwahiyo ukifanya massive imports utakosa walaji na kile cha ku-export hatuna.... halafu unadhani bandari ya Dar es salaam inatosha sana! Hivi uliwahi kuona ile picha ya Wachina wakipanga foleni kabla store haijafunguliwa wakisubiria kununua iPhone 6!! Hivi tuwe na angalau 20% ya uchumi wa China bado unaamini bandari ya Dar inatosha sana na kuongeza nyingine "sasa hii tutaipeleka wapi?!" South Afrika hapo, ni kwavile tu na sisi ni masikini wa kutisha lakini uchumi wao ni kawaida sana tena ukikishikiwa na watu wa jamii moja! Population yake wala hawajatuacha sana lakini bado wana bandari 5+!

Kwamba baada ya miaka 40 eti bandari itakuwa imeshachakaa; hivi umeshapata kujiuliza hii bandari ya Dar es salaam ambayo leo tunaitegemea ina miaka mingapi?

FYI, hii habari kama ni kweli basi hili litakuwa kosa kubwa sana kwa serikali ya JPM na watani zetu Wakenya wakisikia hii kitu watafurahi sana na sitagombana tena na Wakenya wakituita Watanzania ni mabogasi manake huwa nakwaruzana nao mara nyingi sana lakini tukiuacha mradi wa Bagamoyo, basi ni kweli tuna kila sifa za kuitwa mabogasi! Hii habari akiipata Bepari Uhuru Kenyatta lazima afungue Champagne asubuhi asubuhi!

Kama kuna terms zisizofaa jibu ni kukaa mezani na sio ku-abandon the whole project! Nimeshasema na hapa nitasema tena-- Dar es salaam haina eneo la kuweza ku-handle bandari yenye uwezo wa ku-handle idadi kubwa ya makontena for the next 50 years. Kule Mtwara kutakuwa bize sana na mimeli ya mafuta.
 
Kumbe lowasa alishanusa harufu mbaya kweli ndio maana wote walihubiri mabadiliko.
Sasa kwa hakika nimemuelewa jpm alipozungusha mikono alimaanisha nini?

Asante Mungu kwa kuniona tz yetu na kutusimamishia viongozi wenye mawazo sawa kupitia vyama tofauti.
 

UKAWA wanahusika na nini katika hili?
 
Na hatua stahiki kwa wakati muafaka

Ni vyema kuwa "imesitisha" na hatujaelezwa sababu. Ingekuwa umefutwa hapo ningesema mengine.

Ndiyo maana nnasema hii habari haijakamilika. Kusitisha kunaweza kuwa na sababu nyingi, labda mwekezaji kachelewa?, Labda mkandaasi kachelewa? Labda mwekezaji hajakamilisha vigezo? Labda kuna redesign?

Sababu za kusitisha mradi huwa ni nyingi sana, mpaka tupate maelezo ya kina, lakini kama unasitisha tu bila sababu za msingi na maelewano na wawekezaji na wakandarasi hapo ni kuwatafutia ulaji wa bure kama ilivyotutokea kwa Dowans na IPTL.

= Magufuli
 
Hilo lilikuwa more than a jipu, Tambaazi kabsaa hongera Magufuli
 
Katika michango mbalimbali humu ndani kuna mapungufu ambayo baadhi yetu tuna-speculate majibu. wakati tunajadili hatufahamu huo mkataba wa kujenga bandari ya Bagamoyo ukoje. Kuna wanaosema ni mkopo na kuna wanaosema ni wawekezaji bila kuhusisha fedha zetu. Wengine wanasema ni mradi wa miaka 50 baada ya hapo unakabidhiwa kwa serikali. Kuna swala la mradi wa Tanga. Bandari ya Tanga sio kupanuliwa bali ni kujengwa upya katika eneo la Mwambani hivyo ujenzi utakuwa hauna tofauti na Bagamoyo, labda ukubwa tu. Huku Tanga bandari ya sasa ina kina kifupi na miaka yote yanatumika matishari (yaani kuhamisha mizigo kutoka kwenye meli iliyoko kina kirefu na kuipeleka bandarini). Bandari ya Bagamoyo itaambatana na eneo la uwekezaji EPZ na wawekezaji wanajua wapi ni sehemu nzuro kuiwekeza, haiwezekani kuwahamishia Mtwara au Tanga maeneo ambayo kiuchumi hayawezi kuwapa faida, badala yake watakwenda kuwekeza kwingine. Mtwara iwepo Bagamoyo isiwepo, ni lazima ijengwe bandari mpya kwa hali ya kiuchumi inavyopanuka kule. Hii bandari ya DSM nina wasiwasi wa eneo la kuipanulia, kinachotakiwa ni kuongeza efficiency kwa hizo meli chache zinazoingia.
Ni muhimu tukafahamu sababu za kusimamisha ujenzi wa bandari ya Bagamoyo na itakuwa inamilikiwa na nani, muwekezaji au serikali. Vinginevyo bandari zote tatu ni muhimu ni swala la kuamua tuanze na upi iklwa tunataka kutumia fedha zetu.
 
mkuu natamani kuijua siri hiyo.funguka kama hutajali
Mkuu vuta subira naamini tutajua mengi muda utasema huu ni mwanzo,
Mradi mkubwa kama huu utakuwa na matatizo makubwa kuliko tunavyofahamu,hadi kuchuliwa kwa uamuzi huu.
 
VIVA magu JPM maana jama alitakaga hiyo bandari kwa maslai ya watu wa kwao bagamoyo bila kuangalia maslai mapana ya taifa na hiyo project sio tuu kuipeka mbele bali ni kuifuta kabisa na kuboresha nandari zilizopo TANGA,DSM na MTWARA
kubolesha miundombinu ya reli na barabara za lami kwa ajili ya kurahisisha usafirishaji wa mizigo
 
Last edited by a moderator:

Read "suspended not shelved", unajuwa maana yake?
 
Uko sahihi mkuu na kama kuna zawadi ambayo jpm anatakiwa kuwaachia watz ni kuweka uwazi ktk.mikataba yote naamini yawezekana hata kwenye gesi si salama.
 
Last edited by a moderator:
....maadam tuna nia ya kushindana ktk biashara ya iliyojaa ushindani, ya bandari ujenzi wa bandari mpya, kubwa, na ya kisasa haukwepeki....
Tuna southern corridor development project. Kuboresha bandari ya mtwari nareli ya kusini hadi kwenda liganga namchuchuma kuzalisha umeme wamakaa ya mawe viwanda vinavyotokana nauwepo wa gas kilimo cha nyanda za juu kusini nakusini ikiwemo korosho nk. Hivi navingine vingi vinatosha kuifanya bandari ya Mtwara kuwa bize kuliko unavyofikiri so huitaji kushindana nalamu kwa ajili ya import but hapa nimuhimu sana kwa ajili ya export for that case uchumi utaweza kuimarika zaid coz bandari itakuwa inaendesha nakuhudumia uchumi wa uzalishaji wa ndani zaidi kuliko uzalishaji wa nje. Pitia doc ya southern corridor dev project uone kwa nini tulipinga ujenz wa Bandar ya bagamoyo. Si kila ushindani wakibiashara nimuhimu wakt mwingine unaweza kuwa nawrong competitor
 
Mkuu vuta subira naamini tutajua mengi muda utasema huu ni mwanzo,
Mradi mkubwa kama huu utakuwa na matatizo makubwa kuliko tunavyofahamu,hadi kuchuliwa kwa uamuzi huu.
na sote tuseme kwamba ushindi mzuri ni ule wa baada ya kipyenga cha mwisho.muda ni hakimu wa haki huwa hauongopi
 
Nchi hii inawatu wanafiki sijapata kuona, waliokuwa wanatuaminisha enzi za utawala wa JK kwamba Bandari ya Bagamoyo ikijengwa itaboost uchumi wetu ameondoka madarakani wameanza habari za Kupanua DSM na MTR. Kweli kwa mfumo uliopo tutaendelea kuganga jaa tu. Nchi haiwezi kuendelea kwa mipango ya kujipendeleza bila kuangalia hali halisi ikoje. Kila awamu itakuja na mbwembwe kibindoni. Duh!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…