mtigalubawa
Member
- Jan 5, 2016
- 19
- 0
The Construction of the 10 billion (about Sh22 trillion) Bagamoyo Port has been suspended, The Citizen has learnt. The government wants to focus instead, on improving the capacity, performance and efficiency of the Mtwara and Dar es Salaam ports.
The Minister for Works, Transport and Communications, Prof. Makame Mbarawa, confirmed yesterday that the construction of what would be the largest port in Africa has been suspended, not shelved to pave way for upgrading berths 13 and 14 as well as developing the Mtwara Port depending on the availability of Funds. The activities would take years to complete, the minister said because the process has to start from finding funding.
Source: THE CITIZEN
View attachment 315504
On point.
Sifa zikizidi mgema hutia maji,ndio hii sasa!yani Kenya walikuwa wanasali usiku na mchana hoi project ikwame!kukwamisha genetation defining project Kama hii ni uhaini grade one!bandari za aina ya bagamoyo hazijengwi hovyo.na hata zilijengwa,hazijengwi karibu karibu.sasa ikitokea wakenya wakawaconvince wachina wahamishie hii kitu kwao.sie tutabaki na kijibandari cha kichuuzi cha dar ambacho hata kwa mombasa hakifuo dafu.halafu tunataka kushindana,how?
Magufuli will ruin our economy akiendelea hivi.mark my words.dunia ya sasa sio lazima ushinde kila argument, sio lazima utunishie msuli kila MTU/taifa,sio lazima usifiwe kila kona.moderation is important.yataja kutukuta ya Mugabe.tuna raisi anayetutetea na yukp right lakini we keep making suicidal decisions in the name of being correct .
cleverbright upooooo?,sikuoni kabisa mkuu,njoo huku,au nifah kakulevya hata habari kama hizi huzifuatilii??
Mkuu paso sijui kwanini uamuzi wa kusitisha Bandari ya Bagamoyo umeniuma sana tena sana.
Kama nitakuwa mbali na ukweli tafadhali nisahihishwe Bandari ya Bagamoyo fedha zake hazitatoka hazina yetu bali wawekezaji kama sikosei China ambayo ingegharimu 10 bilion u$ zingeingizwa na wawekezaji.Najua kungekuwa na muda mrefu labda 50 years ya kumilikiwa na wawekezaji yamkini mimi na wewe including Kikwete hatutakuwepo lakini watoto na wajukuu wetu wangekuja kufaidi matunda ya maamuzi ya serekali ya awamu ya nne.
Bandari ya Bagamoyo ingetoa majawabu yote ya ushindani na bandari ya Mombasa.Majirani zetu Kenya walikuwa wakiogopa sana ujio wa Bandari ya Bagamoyo ambao ungefungua fursa nyingi za kiuchumi.Uwekezaji wa aina hii unagombewa dunia nzima nashangaa sana mtu mmoja waziri Prof Mbarawa ana uwezo kuondsha mradi mkubwa kiasi hichi na waTanzania wakamchekea kisa eti Bagamoyo nyumbani kwa Vasco watu wanasahau Bagamoyo ipo Tanzania si Uganda au Rwanda.
Sababu za kusitisha ujenzi wa bandari ya Bagamoyo lazima ziwekwe wazi masuala ya kijinga jinga hayana nafasi karne ya 21.Sasa naanza kuamini Dr Magufuli atashindwa mapema iwapo atakuwa anafanya maamuzi ya aina hii.Kama mkataba ulikuwa na kasoro nadhani serekali ingekaa chini na wadau wote na kurekebisha kasoro hizo.Kama Bagamoyo panaonekana si sehemu nzuri basi wengetafuta eneo jingine lakini si kuufyeka mradi.Siku zote Tanzania itabaki nyuma linapokuja suala la ushindani kwakuwa viongozi wetu wengi wanaonekana hawajali sana usatawi wa Tanzania zaidi ya kuwekeana vinyongo.
Nadhani kuna tofauti kubwa sana ya misamiati hii miwili ya Ukarabati na Upanuzi..!! Kinachofanyika ni upanuzi wa bandari za dar,mtwara na tangaTunatakiwa kujenga bandari ya kisasa sio kuboresha wala kukarabati, tunatakiwa tuweke misingi ya maendeleo na plan za muda mrefu zaidi ya miaka 100, siio kila ya baada ya miaka 10 tunakarabati , tuamue moja, sio kuachana na bandari ya bagamoyo eti tunakwenda kukarabati mtwara na tanga, kwa hiyo magufuli aseme bandari ya bagamoyo kuhamishiwa tanga au mtwara na ujenzi wake kuanza ifikapo june. Tunakarabati nini, mabanda ya dar, mtwara na tanga na kuziita bandari?, tunakataa bagamoyo port , bandari ya kisasa tunakibmilia kukarabati?
Mkuu hebu vua miwani tazama Ramani ya Africa, siku hizi kuna ushindani mkubwa sana ktk kutafuta wateja, DRC wamevutwa sana na Beira na Cape Town kuliko Dar hawawezi kwanza Mtwara, pia kuna mazungumzo alikua a nafanya Moses Katumbi kufufua reli kati Katanga na Angola ambapol ni jirani sana kwao, ila Kabila ametibua na Moses kahama chama.
Zambia kumbuka waliacha hata kutumia Tazara kusafirisha shaba angalia shida wanayopata Tazara, Chiluba alizidiwa au alihongwa na wafanyabiashara mpaka leo reli zao hazitumiki vizuri kusafirisha mizigo hawawezi kwenda Mtwara, zaidi ni kwa matumizi ya ndani.
Bagamoyo ni muhimu sana kwa Rwanda, Burundi na DRC ambayo Tanzania inaingia mara 3 kwa ukubwa, kwa kupitisha mizigo, Kasanga via Murilo kwa ajiri ya Lubumbash Katanga, Kasai zote 2, na Kinshasa, na Kigoma kwa ajiri ya Congo mashariki majimbo ya Kivu kusini na kaskazini.[/QhapanaNyie ndio mliokaa kwenye kahawa maamua bagamoyo sio? Kama ulivosema tuangalie Raman ya Africa na wewe angalia Raman ya Africa zoom. Mombasa port af weka upande wa satellite iangalie jinsi wakenya walivoongeza berth za Mombasa na uàngalie Bandar yao ilivo ndan zaid hata ya Tanzania.
Wanasema Iyo bagamoyo mega port itakuwa na uwezo Mara 20 ya sasa.sasa swal ni je tanzania na majiran zetu tuna demand capacity kubwa kwa mda huu kiasi hicho cha kuitaj Bandar mpya?jibu ni hapana.
Kumbe inaezekana tukiongeza magate ya meli kwa dar es salaam.na jaribu kuchek satellite dar port bado ina nafas kubwa ya kuongeza bandar
Mkuu,kama ulikuwepo kwenye akili yangu.Nami nafikiri vivyo hivyo.Ni dili tuu hizi,watu wanarudi kinyume na kwenda kuchukua 80% zao kwa makampuni waliyo saini nao mikataba,Jambo hili ni planned kabisa.
Acha hao wawekezaji wale hiyo fwedha ya bure; Heri nusu shari kuliko shari kamili...,Hapo wawekezaji walioingia mikataba watakula fedha ya bure kama hii habari ni ya ukweli.
Sijajua tunafanyaje kuimarisha miundo mbinu yetu hasa Reli na viwanja vya ndege. Najua kuna wafanya biashara wengi pamoja na kutumia Bandari pia huwa wanataka kufanya mambo yao kwa kasi. Kwa mfano mtu anatoka Kongo wakati Bandari iko Mtwara ya Mzigo anaoupeleka Kusini mwa Msumbiji sidhani kama atataka kupanda Basi toka Dar es salaam kwenda Mtwara!kuondoa Concentration Dar es salaam....Mikoa ya kusini inabidi tutengeneze hub upande huo pia
Watu wanao mlahumu JK siwaelewi kabisa!! Upanuzi/ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ungeliketea tija Taifa letu na majirani - kina cha Bandari ya Bagamoyo ni kirefu zaidi huitaji miundo mbinu ya gharama kubwa kuijenga/kupanua - kwa uelewa wangu Wachina ndio wangegharimia karibu kila kitu,halafu wanakodi kwa miaka ishirini na tano kama sikosei, sasa hapo Serikali atapataje hasara au kufikiria bandari hiyo haitufai wakati wenzetu wako mbioni kujenga bandari kubwa Malindi ambayo ingeshindana na ya Bagamoyo, sio vizuri kubeza beza miradi ambayo ingeweza kutuletea manufaa makubwa as a Nation - sio kila kitu alichopenekeza JK kina walakini - hatujui alitumia mbinu gani kuwashurutisha Wachina kuja kuwekeza kwenye bandari - hii ilikuwa ni moja ya project kubwa ambayo tulipaswa kujivunia na kumshukuru JK kwa kutumia PR yake nzuri kuwashurutisha wawekezaji, mradi huu mkiuua basi ntajua Watanzania kumbe hatujui vipa umbele vyetu ni vipi. Washindani wetu watafurahi sana sana kutokana na sisi kupoteza a golden chance kwa kuendekeza malumbam yasiyo na tija, tukifanya ujinga wachina hawaturudi tena.Habar
Habari ina ukweli kabisa, soma The Citizen, huwa gazeti hili hawaongei mambo ya mitaani.
Serikali Awamu ya Nne inaelekea ilitumia vigezo visivyoeleweka vyema katika sekta nzima ya usafirishaji, hususan bandari.
Bagamoyo haina hata reli ya kuunga bandarini, jipu hilo!
Hapo wawekezaji walioingia mikataba watakula fedha ya bure kama hii habari ni ya ukweli.
Watu wanao mlahumu JK siwaelewi kabisa!! Upanuzi/ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ungeliketea tija Taifa letu na majirani - kina cha Bandari ya Bagamoyo ni kirefu zaidi huitaji miundo mbinu ya gharama kubwa kuijenga/kupanua - kwa uelewa wangu Wachina ndio wangegharimia karibu kila kitu,halafu wanakodi kwa miaka ishirini na tano kama sikosei, sasa hapo Serikali atapataje hasara au kufikiria bandari hiyo haitufai wakati wenzetu wako mbioni kujenga bandari kubwa Malindi ambayo ingeshindana na ya Bagamoyo, sio vizuri kubeza beza miradi ambayo ingeweza kutuletea manufaa makubwa as a Nation - sio kila kitu alichopenekeza JK kina walakini - hatujui alitumia mbinu gani kuwashurutisha Wachina kuja kuwekeza kwenye bandari - hii ilikuwa ni moja ya project kubwa ambayo tulipaswa kujivunia na kumshukuru JK kwa kutumia PR yake nzuri kuwashurutisha wawekezaji, mradi huu mkiuua basi ntajua Watanzania kumbe hatujui vipa umbele vyetu ni vipi. Washindani wetu watafurahi sana sana kutokana na sisi kupoteza a golden chance kwa kuendekeza malumbam yasiyo na tija, tukifanya ujinga wachina hawaturudi tena.
Hapo wawekezaji walioingia mikataba watakula fedha ya bure kama hii habari ni ya ukweli.