Mkuu
paso sijui kwanini uamuzi wa kusitisha Bandari ya Bagamoyo umeniuma sana tena sana.
Kama nitakuwa mbali na ukweli tafadhali nisahihishwe Bandari ya Bagamoyo fedha zake hazitatoka hazina yetu bali wawekezaji kama sikosei China ambayo ingegharimu 10 bilion u$ zingeingizwa na wawekezaji.Najua kungekuwa na muda mrefu labda 50 years ya kumilikiwa na wawekezaji yamkini mimi na wewe including Kikwete hatutakuwepo lakini watoto na wajukuu wetu wangekuja kufaidi matunda ya maamuzi ya serekali ya awamu ya nne.
Bandari ya Bagamoyo ingetoa majawabu yote ya ushindani na bandari ya Mombasa.Majirani zetu Kenya walikuwa wakiogopa sana ujio wa Bandari ya Bagamoyo ambao ungefungua fursa nyingi za kiuchumi.Uwekezaji wa aina hii unagombewa dunia nzima nashangaa sana mtu mmoja waziri Prof Mbarawa ana uwezo kuondsha mradi mkubwa kiasi hichi na waTanzania wakamchekea kisa eti Bagamoyo nyumbani kwa Vasco watu wanasahau Bagamoyo ipo Tanzania si Uganda au Rwanda.
Sababu za kusitisha ujenzi wa bandari ya Bagamoyo lazima ziwekwe wazi masuala ya kijinga jinga hayana nafasi karne ya 21.Sasa naanza kuamini Dr Magufuli atashindwa mapema iwapo atakuwa anafanya maamuzi ya aina hii.Kama mkataba ulikuwa na kasoro nadhani serekali ingekaa chini na wadau wote na kurekebisha kasoro hizo.Kama Bagamoyo panaonekana si sehemu nzuri basi wengetafuta eneo jingine lakini si kuufyeka mradi.Siku zote Tanzania itabaki nyuma linapokuja suala la ushindani kwakuwa viongozi wetu wengi wanaonekana hawajali sana usatawi wa Tanzania zaidi ya kuwekeana vinyongo.