Serikali yasitisha Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Kuimarisha Bandari za Mtwara, Dar

Serikali yasitisha Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Kuimarisha Bandari za Mtwara, Dar

Status
Not open for further replies.
Ninachojifunza hapa kuna watu wana chuki binafsi kwa mtu fulani. Maana inaonekana kila kitu Kinamuelemea yeye. Ila wanashindwa kuelewa kuwa bila ya yeye jpm asingeingia maaana alikuwa na ushawishi mkubwa wa kumchinja kikubwa tuache unafiki
 
The Construction of the 10 billion (about Sh22 trillion) Bagamoyo Port has been suspended, The Citizen has learnt. The government wants to focus instead, on improving the capacity, performance and efficiency of the Mtwara and Dar es Salaam ports.

The Minister for Works, Transport and Communications, Prof. Makame Mbarawa, confirmed yesterday that the construction of what would be the largest port in Africa has been suspended, not shelved to pave way for upgrading berths 13 and 14 as well as developing the Mtwara Port depending on the availability of Funds. The activities would take years to complete, the minister said because the process has to start from finding funding.


Source: THE CITIZEN
View attachment 315504

Wakati wa kampeni uchaguzi uliopita, wana ccm wengi walipingana na hoja za ukawa kwamba ujenzi wa bandari bagamoyo Hauna tija kwa taifa. Tulijadili kwamba:

Inasemekana Serikali ya Kikwete ilikopa China Tsh Bilioni kumi kwa ajili ya Mradi huo. Ukawa wakaendelea kusema kwamba, haiingii akilini kuanza ujenzi wa bandari mpya wakati zipo nyingine ambazo zinahitaji maboresho na pia kuziunganisha na uchumi wa ndani na nje ya nchi.

Ukawa wakazidi kusema kwamba kama tunaweza kusamehe madeni ya dola 750 kwa mwaka, tunaweza kabisa kwa kipindi kifupi na cha Kati kufanya Miradi yenye matokeo kama hayo kwa fedha zetu wenyewe.

Huo ndio ulikuwa pia mtazamo wa mgombea urais kupitia ukawa, Edward Lowassa. Hivyo akaahidi kwamba serikali yake itaziboresha bandari zilizopo na pia kuzifanya ziweze kutoa huduma bora kabisa sambamba na kuhakikisha kazi zinafanyika kwa masaa 24 mchana na usiku kama ilivyo katika mataifa mengine duniani yaliyofanikiwa kiuchumi.

CCM iliendelea kuhimiza juu ya umuhimu wa ujenzi wa bandari ya bagamoyo hata katika kipindi cha kunadi ilani yake ya uchaguzi (2015-2010) na hata katiak ziara yake ya kampeni mkoa wa Pwani mwezi Oktoba 2015, John Pombe Magufuli aliendelea kuhimiza juu ya msimamo wa chama chake cha CCM kujenga bandari mpya Bagamoyo.

Lakini tofauti na msimamo huo wa awali, inaonekana serikali ya CCM hatimaye imeona mantiki katika hoja za ukawa na kuamua kuzitekeleza. Kwa hilo, Serikali ya ccm inastahili pongezi kubwa.
 
Unazungumzia rekodi gani? Santuri au tija?! Kama ni kuvunja rekodi kwa mipasho, kejeli, ubadhirifu na kutojua anachokifanya sawa!!
 
Hivi kuna babdari ya east Africa ilikuwa ijengwe Kyle mwamboni tanga toka 2006 na watu wakafidiwa, iliishia wapi jamani, muasisi WA hiyo project alikuwa nani
 
On point.
Sifa zikizidi mgema hutia maji,ndio hii sasa!yani Kenya walikuwa wanasali usiku na mchana hoi project ikwame!kukwamisha genetation defining project Kama hii ni uhaini grade one!bandari za aina ya bagamoyo hazijengwi hovyo.na hata zilijengwa,hazijengwi karibu karibu.sasa ikitokea wakenya wakawaconvince wachina wahamishie hii kitu kwao.sie tutabaki na kijibandari cha kichuuzi cha dar ambacho hata kwa mombasa hakifuo dafu.halafu tunataka kushindana,how?

Magufuli will ruin our economy akiendelea hivi.mark my words.dunia ya sasa sio lazima ushinde kila argument, sio lazima utunishie msuli kila MTU/taifa,sio lazima usifiwe kila kona.moderation is important.yataja kutukuta ya Mugabe.tuna raisi anayetutetea na yukp right lakini we keep making suicidal decisions in the name of being correct .


Kabla ya kumuhukumu Raisi Magufuli ulipaswa kwanza ujielimishe ni kwa nini Ujenzi umesitishwa, na je Mkataba wa huyo ujenzi unasemaje? Je, Maslahi yetu sisi kama nchi yameangaliwa kwa kiasi gani?
Hawo wafadhili wa huwo mradi walitakiwa kupata nini badala yake?
Kumbuka haijawahi kutokea ktk Historia ya Dunia hii nchi ije kufanya uwekezaji wa Mabilioni kwenye nchi nyingine bure tu, unafikiri wao Wachina hizo fedha hawazihitaji?

Usisahau tumeshaingia mikataba kama hii kwenye dhahabu ambapo sisi tunapata asilimia 3% (gratuity) wakati wawekezaji wanachukuwa zaidi 95% na leo hii kuna Migodi imefungwa kama resolute huko Nzega na ukienda hali ya maisha ya Nzega haijabadilka badala ya kuharibika zaidi kwa kuwa wameachiwa mashimo, hivyo narudia tena usilaumu bure kabla ya kuelewa kwanza, huwezi jua kilichomo kwenye huwo Mkataba kwa maana tuna uzoefu tayari na Mikataba kama hiyo kwenye Dhahabu yetu!
 
Last edited:
cleverbright upooooo?,sikuoni kabisa mkuu,njoo huku,au nifah kakulevya hata habari kama hizi huzifuatilii??

siasa za Tanzania " zinagandisha " akili na hata kukufanya " uwehuke " hivyo siziwezi na sizitaki pia kuzisikia japo nilishiriki fully ( 100% ) katika kuwaleteeni Dr. Magufuli MADARAKANI kwa gharama zozote zile au kwa vyoyote vile ila sasa nimeachana rasmi na siasa za maji taka za kibongo.
 
Kama ni kwa maslahi ya nchi haina shida lakini kama ni majungu ya kuvutia kwangu ni tatizo
 
Mkuu paso sijui kwanini uamuzi wa kusitisha Bandari ya Bagamoyo umeniuma sana tena sana.

Kama nitakuwa mbali na ukweli tafadhali nisahihishwe Bandari ya Bagamoyo fedha zake hazitatoka hazina yetu bali wawekezaji kama sikosei China ambayo ingegharimu 10 bilion u$ zingeingizwa na wawekezaji.Najua kungekuwa na muda mrefu labda 50 years ya kumilikiwa na wawekezaji yamkini mimi na wewe including Kikwete hatutakuwepo lakini watoto na wajukuu wetu wangekuja kufaidi matunda ya maamuzi ya serekali ya awamu ya nne.

Bandari ya Bagamoyo ingetoa majawabu yote ya ushindani na bandari ya Mombasa.Majirani zetu Kenya walikuwa wakiogopa sana ujio wa Bandari ya Bagamoyo ambao ungefungua fursa nyingi za kiuchumi.Uwekezaji wa aina hii unagombewa dunia nzima nashangaa sana mtu mmoja waziri Prof Mbarawa ana uwezo kuondsha mradi mkubwa kiasi hichi na waTanzania wakamchekea kisa eti Bagamoyo nyumbani kwa Vasco watu wanasahau Bagamoyo ipo Tanzania si Uganda au Rwanda.

Sababu za kusitisha ujenzi wa bandari ya Bagamoyo lazima ziwekwe wazi masuala ya kijinga jinga hayana nafasi karne ya 21.Sasa naanza kuamini Dr Magufuli atashindwa mapema iwapo atakuwa anafanya maamuzi ya aina hii.Kama mkataba ulikuwa na kasoro nadhani serekali ingekaa chini na wadau wote na kurekebisha kasoro hizo.Kama Bagamoyo panaonekana si sehemu nzuri basi wengetafuta eneo jingine lakini si kuufyeka mradi.Siku zote Tanzania itabaki nyuma linapokuja suala la ushindani kwakuwa viongozi wetu wengi wanaonekana hawajali sana usatawi wa Tanzania zaidi ya kuwekeana vinyongo.


Hata wewe ndiyo wale wale tu unalalamika na kuhukumu bila kuujua ukweli kwa sababu tu Gazeti limeandika, Je, unazijua sababu hasa za serikali kubadilisha huwo uamuzi?
 
Hivi jk kalifanyia nn hili taifa?maana naona yeye ndo anayeisoma namba kuliko mtu yoyote nchi hii
 
Tunatakiwa kujenga bandari ya kisasa sio kuboresha wala kukarabati, tunatakiwa tuweke misingi ya maendeleo na plan za muda mrefu zaidi ya miaka 100, siio kila ya baada ya miaka 10 tunakarabati , tuamue moja, sio kuachana na bandari ya bagamoyo eti tunakwenda kukarabati mtwara na tanga, kwa hiyo magufuli aseme bandari ya bagamoyo kuhamishiwa tanga au mtwara na ujenzi wake kuanza ifikapo june. Tunakarabati nini, mabanda ya dar, mtwara na tanga na kuziita bandari?, tunakataa bagamoyo port , bandari ya kisasa tunakibmilia kukarabati?
Nadhani kuna tofauti kubwa sana ya misamiati hii miwili ya Ukarabati na Upanuzi..!! Kinachofanyika ni upanuzi wa bandari za dar,mtwara na tanga
 
Mkuu hebu vua miwani tazama Ramani ya Africa, siku hizi kuna ushindani mkubwa sana ktk kutafuta wateja, DRC wamevutwa sana na Beira na Cape Town kuliko Dar hawawezi kwanza Mtwara, pia kuna mazungumzo alikua a nafanya Moses Katumbi kufufua reli kati Katanga na Angola ambapol ni jirani sana kwao, ila Kabila ametibua na Moses kahama chama.

Zambia kumbuka waliacha hata kutumia Tazara kusafirisha shaba angalia shida wanayopata Tazara, Chiluba alizidiwa au alihongwa na wafanyabiashara mpaka leo reli zao hazitumiki vizuri kusafirisha mizigo hawawezi kwenda Mtwara, zaidi ni kwa matumizi ya ndani.

Bagamoyo ni muhimu sana kwa Rwanda, Burundi na DRC ambayo Tanzania inaingia mara 3 kwa ukubwa, kwa kupitisha mizigo, Kasanga via Murilo kwa ajiri ya Lubumbash Katanga, Kasai zote 2, na Kinshasa, na Kigoma kwa ajiri ya Congo mashariki majimbo ya Kivu kusini na kaskazini.[/QhapanaNyie ndio mliokaa kwenye kahawa maamua bagamoyo sio? Kama ulivosema tuangalie Raman ya Africa na wewe angalia Raman ya Africa zoom. Mombasa port af weka upande wa satellite iangalie jinsi wakenya walivoongeza berth za Mombasa na uàngalie Bandar yao ilivo ndan zaid hata ya Tanzania.
Wanasema Iyo bagamoyo mega port itakuwa na uwezo Mara 20 ya sasa.sasa swal ni je tanzania na majiran zetu tuna demand capacity kubwa kwa mda huu kiasi hicho cha kuitaj Bandar mpya?jibu ni hapana.
Kumbe inaezekana tukiongeza magate ya meli kwa dar es salaam.na jaribu kuchek satellite dar port bado ina nafas kubwa ya kuongeza bandar
 
Ni dili tuu hizi,watu wanarudi kinyume na kwenda kuchukua 80% zao kwa makampuni waliyo saini nao mikataba,Jambo hili ni planned kabisa.
Mkuu,kama ulikuwepo kwenye akili yangu.Nami nafikiri vivyo hivyo.
Kama kweli JPM yupo serious katika hili,basi ahakikishe wahusika wote wanachunguzwa na ikibainika kuna ufisadi,basi wachukuliwe hatua kali.
Inawezekana watu walipiga deal liwe hivi huku wao wakineemeka kwa mikataba kusitishwa,sasa ni wakati wa mamlaka husika kuwachunguza wote waliohusika na kuingia mikataba ya huu mradi.
 
kuondoa Concentration Dar es salaam....Mikoa ya kusini inabidi tutengeneze hub upande huo pia
Sijajua tunafanyaje kuimarisha miundo mbinu yetu hasa Reli na viwanja vya ndege. Najua kuna wafanya biashara wengi pamoja na kutumia Bandari pia huwa wanataka kufanya mambo yao kwa kasi. Kwa mfano mtu anatoka Kongo wakati Bandari iko Mtwara ya Mzigo anaoupeleka Kusini mwa Msumbiji sidhani kama atataka kupanda Basi toka Dar es salaam kwenda Mtwara!
 
Habar

Habari ina ukweli kabisa, soma The Citizen, huwa gazeti hili hawaongei mambo ya mitaani.
Serikali Awamu ya Nne inaelekea ilitumia vigezo visivyoeleweka vyema katika sekta nzima ya usafirishaji, hususan bandari.
Bagamoyo haina hata reli ya kuunga bandarini, jipu hilo!
Watu wanao mlahumu JK siwaelewi kabisa!! Upanuzi/ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ungeliketea tija Taifa letu na majirani - kina cha Bandari ya Bagamoyo ni kirefu zaidi huitaji miundo mbinu ya gharama kubwa kuijenga/kupanua - kwa uelewa wangu Wachina ndio wangegharimia karibu kila kitu,halafu wanakodi kwa miaka ishirini na tano kama sikosei, sasa hapo Serikali atapataje hasara au kufikiria bandari hiyo haitufai wakati wenzetu wako mbioni kujenga bandari kubwa Malindi ambayo ingeshindana na ya Bagamoyo, sio vizuri kubeza beza miradi ambayo ingeweza kutuletea manufaa makubwa as a Nation - sio kila kitu alichopenekeza JK kina walakini - hatujui alitumia mbinu gani kuwashurutisha Wachina kuja kuwekeza kwenye bandari - hii ilikuwa ni moja ya project kubwa ambayo tulipaswa kujivunia na kumshukuru JK kwa kutumia PR yake nzuri kuwashurutisha wawekezaji, mradi huu mkiuua basi ntajua Watanzania kumbe hatujui vipa umbele vyetu ni vipi. Washindani wetu watafurahi sana sana kutokana na sisi kupoteza a golden chance kwa kuendekeza malumbam yasiyo na tija, tukifanya ujinga wachina hawaturudi tena.
 
Hapo wawekezaji walioingia mikataba watakula fedha ya bure kama hii habari ni ya ukweli.

Wawekezaji akina nani kama siyo nyienyie na vikampuni vyenu uchwara mlivyoviandaa kupiga dili?naona mna plan nzuri sana ya wizi.
 
Bandari ya Bagamoyo serikali inatoa kiasi gani cha pesa? tusifuate mambo ya wanasiasa, Tanzania hata nchi baadhi ya africa haina uwezo wa kujenga bandari ya 10 B usd, huu mradi ni wawekezaji, yaani serikali ya china na Oman. Tukumbuke wawekezaji wana conditions zao, kama wawekezaji wamekuja Tanzania wakasema tunataka kujenga bandari ya kisasa, na eneo tunalotaka ni Bagamoyo kuna kosa? saa kama serikali wana mipango yao ya kutanua bandari zingine za tanga na mtwara na dar sidhani kama wanakuwa affected na ujenzi wa bandari ya Bagamoyo. Ilikuwa ni jukumu la serikali kuwashawishi hao wawekezaji kuwa inafaa hii bandari ijengwe sehemu zile ambako wao wanaona sio kukataa mradi, na ikiwa muwekezaji anaona bado option nzuri ni bagamoyo basi aendelee na plan hiyo. Hapa tunasema kuna halafu ya rushwa, rushwa ipi? hivi huu mradi tanzania anahusika kama nani? nijuavyo tanzania sisi tumetoa eneo la bagamoyo, lakini pesa ni za wahisani(china/oman), ambapo serikali itakuja kunufaika na mapato pia ajira kwa vijana. Lakini kama serikali wao plan yao ni kupanua hizo zingine waendelee, wajenge kule tanga, mtwara na wapanue dar wao wenyewe , at the same time bagamoyo ujenzi unaweza endelea kwani watoa pesa ni wengine, hat akama serikali inatoa pesa basi ni kiasi kidogo ambacho hakiwezi kuzuia ujenzi wa bandari zingine usiendelee. Tukiwa na bandari hizo zote zitatoa options kwa watu watumie bandari ipi, hivyo ufanisi /mapato kwa serikali utakuwa mkubwa. Nashangaa tunasema huu mradi uligubikwa na usiri ,sijui wizi, mara ohhh sio priority yetu, sasa unataka tuwaambie wahisani acheni kujenga bagamoyo kwani sio pririoty yetu? au ajenge na sisi tuendelee na plan zetu? mimi sioni logic hapo, serikali ya iendelee na upanuzi na wawekezaji wandelee na mradi huo.
 
Watu wanao mlahumu JK siwaelewi kabisa!! Upanuzi/ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ungeliketea tija Taifa letu na majirani - kina cha Bandari ya Bagamoyo ni kirefu zaidi huitaji miundo mbinu ya gharama kubwa kuijenga/kupanua - kwa uelewa wangu Wachina ndio wangegharimia karibu kila kitu,halafu wanakodi kwa miaka ishirini na tano kama sikosei, sasa hapo Serikali atapataje hasara au kufikiria bandari hiyo haitufai wakati wenzetu wako mbioni kujenga bandari kubwa Malindi ambayo ingeshindana na ya Bagamoyo, sio vizuri kubeza beza miradi ambayo ingeweza kutuletea manufaa makubwa as a Nation - sio kila kitu alichopenekeza JK kina walakini - hatujui alitumia mbinu gani kuwashurutisha Wachina kuja kuwekeza kwenye bandari - hii ilikuwa ni moja ya project kubwa ambayo tulipaswa kujivunia na kumshukuru JK kwa kutumia PR yake nzuri kuwashurutisha wawekezaji, mradi huu mkiuua basi ntajua Watanzania kumbe hatujui vipa umbele vyetu ni vipi. Washindani wetu watafurahi sana sana kutokana na sisi kupoteza a golden chance kwa kuendekeza malumbam yasiyo na tija, tukifanya ujinga wachina hawaturudi tena.

Sawa mkuu ila tunauhitaji mkubwa sana wa bandari mtwara kwa sasa kuliko bagamoyo.pia kama tutaboresha kwanza bandari ya dar na ika perfom to the maximum itatupa tija sana wakati wa ujenzi wa bandari ya bagamoyo.

gudbye mkwere
 
Hapo wawekezaji walioingia mikataba watakula fedha ya bure kama hii habari ni ya ukweli.

Bora wale fedha ya bure maana walishazoea.....hata TRL nao ilikuwaje? Awamu ya nne ilikimbilia nini kusaini mkataba dakika za mwisho?

Kama hata mkataba wa mabasi yaendayo kasi ni magumashi ndio iwe mradi mkubwa kama huo tena dakika za majeruhi? There are ways we become heros or zeros
 
Mradi wa Bagamoyo haukuwa na tija yoyote zaidi ya matakwa ya mtawala asiyeambilika.
Priority ya bandari za Tanzania ni:-
1. Dar 2. Tanga 3. Mtwara then zinafuata nyingine
Bandari ya Dar haijawa exploied to the maximum na tatizo la kuondoa na kuhifadhi containers lina ufumbuzi ambao haujafanyiwa kazi kwa makusudi ya watawala na wenza wao wafanyabiashara wanaotaka kuchuma fedha bila kufikiria.
World Bank walifadhili study ya kutengeneza master plan ya bandari zote Tanzania na solution zote zipo.
Tatizo kubwa la Dar Port ni miundombinu ya kuingia na kutoka lakini ufumbuzi wake ni kujenga dry port Kisarawe ambapo kuna eneo la kutosha kati ya reli ya kati na Tazara. Containers zote ta transit zingepelekwa Kisarawe kwa kutumia reli hizo mbili ambayo ingeondoa tayari msongamano barabarani. Mizigo yote ya transit ingekuwa cleared kutokea Kisarawe ambayo ingeunganishwa na road network nje ya Dar.
Terminal na storage za mafuta zingejengwa nje ya Dar pia na kuunganishwa kwa pipeline hivyo tusingeona fuel tankers ndani ya mji.
Ukijumlisha matatizo yote ya nchi hii unarudi pale pale kwenye habari ya KATIBA.
Sasa hivi kila kiongozi anafanya mambo anavyojisikia na hakuna anayeweza kumgusa.
Tatizo pia ni kwamba nchi haina strategic planning ingawa tunaaminishwa kuwa kuna tume ya mipango na mipango inapangwa kumbe hakuna kitu, ni bure kabisa!
Nchi inatakiwa iwe na long term plans kama 30-50 years katika nyanja zote za kiuchumi na kijamii ambazo zinatekelezwa katika shorter terms za 5 years. Ndivyo nchi ambazo zipo serious zinafanya na sio huu utumbo unaondelea hapa.
Kama Rais Magufuli kweli ana vision na nchi hii kwanza ashughulikie swala la katiba wakati anaendelea na hizi emergency measures anazofanya sasa. Then ndiyo afikirie stategic planning ya kuikwamua na kuindeleza hii nchi. Vinginevyo anapoteza nguvu na muda bure.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom