Serikali yasitisha Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Kuimarisha Bandari za Mtwara, Dar

Status
Not open for further replies.
Si hii project ilikuwa inafadhiliwa sijui na watu wa omani na wachina au wametoka nduki ,labda baada ya JPM kaingia madarakani wameona hautalipa. Lengo lilikuwa kuweza kuchukua meli kubwa ambazo haziwezi ku-dock Dar kama ni hivi tutakuwa nyuma ya port ya Mombasa Lamu na Durban Watanzania katika ubora wetu.
 
This is the win -win project, tanzania inaongeza mapato kwa kukamua kodi na ajira juu, then baada ya miaka 40 tunaachiwa bandari yetu, uogo wetu ndo faillure yetu siku zote. Tunakaa na ardhi kubwa bure lisilo dhalisha. Hapa ilikuwa easy sana, kusanya kodi bagamoyo, dar, mtwara, tanga, ndani ya aka 5 tuko mbali. yaani kama tungekuwa serious na bagamoyo port within 5 yrs tunajenga bagamoyo yetu wenyewe kule mtwara. Kenya chukueni hii project tuacheni sisi tulale, tuendelee kudebate issue za ukawa, majipu, na utanuzi wa bandari.
 
Sasa wewe tusaidie kidogo. Kama ushuru wote wa bandari kwa maana mapato yatachukuliwa naTRA Wachina watarejesha vipi fedha zao walizowekeza. Inawezekana binafsi sijajua vizuri. Biashara ya bandari yapo mapato ya aina ngapi. Kwa msaada niambie yapi yatakua ya mchina na yapi yatakuwa ya serikali.
 
Ahahaha kumbe ndio maana mzee wa SWAGA alijipeleka ikulu juziiiiiii sasa nimejuwa

Ancle Magu please Ignore him, mxieeeeeeew
 
Afrika mzima hapana lakini lengo la Mchina ni ku-accomodate East & Central Africa! Don't forget, China ni major exporter to African market!! Sasa basi, kama wewe unaleta bidhaa zako kutoka China au Japan na unazipitishia Mombasa kwenda Rwanda; just do it lakini lengo la Mchina bidhaa zake zote atakazoleta kwa ajili ya East & Central Africa, lengo lake ni kupitishia Bagamoyo badala ya kwenda kupanga foleni Dar au Mombasa! Ana similar project nchini Djibouti kwa ajili ya u kanda ule wa Africa.

Na endapo angefanikiwa, ndo vile tena Mchina hana magari mazuri compared to Japan vinginevyo biashara ya magari Japan kwa u kanda huu ingekufa rasmi manake Mchina ingekuwa anazoa magari laki 1 toka China na anakuja kuyamwaga Bagamoyo na watu kutoka Rwanda, Zambia, DRC n.k wanafuata mzigo hapa hapa au wanatumiwa kutoka hapa... kwahiyo lengo la Mchina ni kuendesha biashara zake kwa mtindo huo
 
Si umeshaambiwa ipo kisarawe na ina connection za tazara, trl nk? Chige tumeshaliwa sana!
 
Chief nakubaliana na wewe 100%
 
..wakati wa kampeni Dr.Magufuli alisema fedha za ujenzi wa bagamoyo, tanga, mtwara, zipo.

..pia wananchi wameshahamishwa kwenye ardhi zao ili kupisha ujenzi wa bandari.

..na Raisi Kikwete aliamuru wote ambao ardhi yao imechukuliwa kwa ajili ya ujenzi wajengewe nyumba.

..pia Raisi alimfukuza kazi afisa mtathmini wa ardhi kwa madai kwamba anazungusha na kuwanyima wananchi haki zao.

..msikilizeni Dr.Magufuli hapa:
cc MTAZAMO, Magurudumu, Bukyanagandi, Nguruvi3, Ngongo
 
Hatuwezi kufanya issue za ki fuckin namna hiyo aisee!yaani watujengee bandari halafu mapato zaidi ya 50%wachukue wao tena kwa zaidi ya miaka kumi sisi tumekaa tu!safi sana Magufuri

Kuruhusu bandari ya Bagamoyo ni kuua bandari ya Dar,Mtwara na tutapoteza pesa ndefu zaidi,ni heri mradi usitishwe ili tuziendeleze bandari zetu kwa kumiliki mapato yote kuliko akili ya Mstaafu ilivyokuwa.

Safi sana Ancle Magu
 
Nimeshakuambia wachina wa mwalimu si wachina wa leo wa karanga, midoli kariakoo na biashara ya meno ya tembo na faru. Nakuhakikishia hakuna hiyo faida unayofikiria. Kama wana huruma sana watujengee standard gauge railway bila kutaka waendeshe reli kwa miaka arobaini. Hata kama wangeweka sharti hilo faida za reli za moja kwa moja kwa mtanzania wa kawaida akiwemo mfanya biashara na mkulima ni kubwa sana.
 
reli ipo
 
Braza kwani kuboresha hizo bandari unafukiria ni nini?
Miundombinu ndo kitu cha kwanza kwani ni kweli kwamba pamejaa lakini kama kutakua na bandari kavu huko kibaa na miundombinu ya reli ikiwa freshi hamna lori litakalo ingia town rather reli itafanya kazi yake

Pili ujenzi wa bandari ya bagamoyo automatically ungeua bandari ya dar
 
HI kitu nilijua tu kama ingetokea hivyo; niliwahi pia ku- comment kama sio humu basi kwenye mitandao mingine ya kijamii! Kiuhalisia ule mradi ulikua hauna TIJA yoyote kwa nchi. Thanks Magufuli, kwa hili nakuunga mkono pia.
Namuunga MKONO Rais Magufuli 101%,hapa naoana kwa dhati kabisa amedhamiria kuliokoa Taifa hili! Ule mradi haukua na tija kabisa! Maamuzi sahihi kwa wakati sahihi!
 
Haya akaimarishe bandari ya Ukerewe...ndio kitakachofuata
 
Ninachotaka kukisema ni kwamba Katiba haimzuii Raisi kuwa mbaya na mwizi
Hayo yanawezekana pale kama ulivyosema wewe mwenyewe kwamba kiwango cha elimu ya Uraia kikiwa kiko chini. Nafurahi kwa mara ya kwanza umekubali kwamba uwekezaji kwenye Elimu ndiyo suluhisho la kuwa na Jamii inayojali Katiba. Lakini pia haiwezekani mtu anaingia kwa Katiba iliyopo halafu asiiheshimu katiba hiyo hiyo kama si kwamba wale wanaoongozwa hawajui watokakako wala waendako!!

Na hili la kuachiana madaraka kwa kweli kama si Mwalimu ambaye akiwa hai alilisimamia sana sijui kama hata hapa kwetu waongeza muda wasingekuwepo. Hapa hoja ya msingi ni kuwa na Jamii inayoweza kuwalazimisha watawala kutii Katiba. Tatizo Afrika ni rahisi watu kuwagawa Kidini, kikabila, kiukoo na mwisho wa siku anayevunja Katiba hujifanya kulinda Kabila, dini, Ukoo, chama, au jinsia yake dhidi ya wale wanaomhimiza kulinda Katiba!
 
Mradi huu bado upo..umesitishwa kwa muda tu. Tatizo waliopewa kazi ya kusaka fedha wanachechemea.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…