Serikali yasitisha Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Kuimarisha Bandari za Mtwara, Dar

Serikali yasitisha Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Kuimarisha Bandari za Mtwara, Dar

Status
Not open for further replies.
Si hii project ilikuwa inafadhiliwa sijui na watu wa omani na wachina au wametoka nduki ,labda baada ya JPM kaingia madarakani wameona hautalipa. Lengo lilikuwa kuweza kuchukua meli kubwa ambazo haziwezi ku-dock Dar kama ni hivi tutakuwa nyuma ya port ya Mombasa Lamu na Durban Watanzania katika ubora wetu.
 
This is the win -win project, tanzania inaongeza mapato kwa kukamua kodi na ajira juu, then baada ya miaka 40 tunaachiwa bandari yetu, uogo wetu ndo faillure yetu siku zote. Tunakaa na ardhi kubwa bure lisilo dhalisha. Hapa ilikuwa easy sana, kusanya kodi bagamoyo, dar, mtwara, tanga, ndani ya aka 5 tuko mbali. yaani kama tungekuwa serious na bagamoyo port within 5 yrs tunajenga bagamoyo yetu wenyewe kule mtwara. Kenya chukueni hii project tuacheni sisi tulale, tuendelee kudebate issue za ukawa, majipu, na utanuzi wa bandari.
 
Kuna Mdau mmoja hapa nimemuuliza hayo mapato yote ni mapato yapi lakini hajanijibu labda nisaidie wewe kunipa darasa!!

Can I tell you something?! I am afraid ikiwa kweli unalifahamu vizuri hili suala kwa jinsi issue ya kodi ulivyoita vikodi!!

Guys, pesa nyingi bandarini inachukuliwa na TRA na sio TPA!! Na mapato ya TRA yanaongezeka kadri mzigo unaopitia bandarini unavyoongezeka; keeping other factors constant! Pesa inayoingia bandari ni ndogo sana ukilinganisha na inayoenda TRA! Na kv bandari ya Dar hawana eneo kubwa kimapato ndo wanaathirika zaidi na ndio maana sehemu kubwa ya mzigo unahifadhiwa na Privately owned ICDs!

Kule Bagamoyo, hata kama bandari itakuwa funded na Wachina kwa 100%; mapato/kodi za TRA through imports and export Mchina hazigusi kwahiyo ndo maana umenishangaza unaposema vikodi unless kama unamaanisha kodi zitazolipwa na Wachina wenyewe! Ikiwa bandari itakuwa na uwezo wa kupitisha mzigo mara 3 ya sasa, maana ake ni kwamba hata mapato ya TRA yatapanda kwa similar proportionality!

Halafu nitarudia tena kwako!! Bandari 3 au 4 sio nyingi kama mnavyodhani.... kwa sasa zinaweza kuonekana nyingi kv we don't produce so we don't export! Likewise, our purchasing power ni ndogo so we don't import much! Kwahiyo mnaweza kudhani bandari ni nyingi kumbe msingi wake ni bandari kutumiwa na nchi maskini! Leo hii uki-import smart tv milioni moja zitakudodea but assume nchi zinazutumia bandari ya Dar zinakuwa kiuchumi angalau mara tu na hivyo kuongea exports na purchasing power ya imported goods.... hivi bado hapo unaamini Dar port itakuwa abandoned kwa kukosa mzigo?!
Sasa wewe tusaidie kidogo. Kama ushuru wote wa bandari kwa maana mapato yatachukuliwa naTRA Wachina watarejesha vipi fedha zao walizowekeza. Inawezekana binafsi sijajua vizuri. Biashara ya bandari yapo mapato ya aina ngapi. Kwa msaada niambie yapi yatakua ya mchina na yapi yatakuwa ya serikali.
 
Ahahaha kumbe ndio maana mzee wa SWAGA alijipeleka ikulu juziiiiiii sasa nimejuwa

Ancle Magu please Ignore him, mxieeeeeeew
 
Hata wewe tatizo la uelewa pia! Unawezaje kujenga Bandari TanZania ikahudumia Afrika nzima? Kivipi unaweza kuniambia? Kwa taarifa yako tu wateja wanaotumia hata Bandari ya Mombasa Kenya huwezi kuwaleta kutumia Bandari yetu ni ngumu sana na hai make economic sense kwao kijiografia sasa iweje Bandari ijengwe Bagamoyo ihudumua Afrika nzima? Unawezaje kumfanya Muethiopia au Msufdani aje kutumia Bandari ya Bagamoyo badala ya Mombasa unaweza kuniambia hilo?
Afrika mzima hapana lakini lengo la Mchina ni ku-accomodate East & Central Africa! Don't forget, China ni major exporter to African market!! Sasa basi, kama wewe unaleta bidhaa zako kutoka China au Japan na unazipitishia Mombasa kwenda Rwanda; just do it lakini lengo la Mchina bidhaa zake zote atakazoleta kwa ajili ya East & Central Africa, lengo lake ni kupitishia Bagamoyo badala ya kwenda kupanga foleni Dar au Mombasa! Ana similar project nchini Djibouti kwa ajili ya u kanda ule wa Africa.

Na endapo angefanikiwa, ndo vile tena Mchina hana magari mazuri compared to Japan vinginevyo biashara ya magari Japan kwa u kanda huu ingekufa rasmi manake Mchina ingekuwa anazoa magari laki 1 toka China na anakuja kuyamwaga Bagamoyo na watu kutoka Rwanda, Zambia, DRC n.k wanafuata mzigo hapa hapa au wanatumiwa kutoka hapa... kwahiyo lengo la Mchina ni kuendesha biashara zake kwa mtindo huo
 
Kupisha miundombinu ipi wakati according to the Citizen, wanataka kuonesha gati 1-7; 13 & 14 za bandari ya Dar na kisha kuboresha Mtwara!

Lakini vilevile hakuna anayepinga kuboresha bandari ya Dar lakini huwezi kusitisha mradi mkubwa kama wa Bagamoyo kwa ajili ya Dar ambayo nishasema hapo awali kwamba hata maeneo ya kujenga container depots hamna unless kama wanakusudia kuimaliza Temeke yote na kuibadilisha kuwa eneo la maghala!
Si umeshaambiwa ipo kisarawe na ina connection za tazara, trl nk? Chige tumeshaliwa sana!
 
Sisi/watanzania kinachotufanya tusiendelee kwa sababu ni waoga, na hatupendi ushindani, Bandari ya bagamoyo ni wahisani wanajenga ,na baadae watasimamia huo mradi hadi kipindi watakaporudisha pesa zao, hilo ni wazo zuri, cha msingi serikali ikae na hao wawekezaji waangalie jinsi ya kuendesha mradi huo na kwa kipindi gani, pili serikali awe ni player katika mradi huo, Yaani awe na hisa za kutosha katika mradi huo. Kingine serikali itenge pesa za kujenga bandari za mtwara na Tanga, pia to upgrade dar port, ili watu wawe na options nyingi, na itakusanya mapato na yakutosha na pia kuzalisha ajira za kutosha. tunaweza tukawa na hata bandari kumi, reli za kutosha na 5 airports za maana, lengo ni kuwa na revenue of 5 billions USD per month, hapo ndo tutapata maendeleo.
Chief nakubaliana na wewe 100%
 
..wakati wa kampeni Dr.Magufuli alisema fedha za ujenzi wa bagamoyo, tanga, mtwara, zipo.

..pia wananchi wameshahamishwa kwenye ardhi zao ili kupisha ujenzi wa bandari.

..na Raisi Kikwete aliamuru wote ambao ardhi yao imechukuliwa kwa ajili ya ujenzi wajengewe nyumba.

..pia Raisi alimfukuza kazi afisa mtathmini wa ardhi kwa madai kwamba anazungusha na kuwanyima wananchi haki zao.

..msikilizeni Dr.Magufuli hapa:

cc MTAZAMO, Magurudumu, Bukyanagandi, Nguruvi3, Ngongo
 
Hatuwezi kufanya issue za ki fuckin namna hiyo aisee!yaani watujengee bandari halafu mapato zaidi ya 50%wachukue wao tena kwa zaidi ya miaka kumi sisi tumekaa tu!safi sana Magufuri

Kuruhusu bandari ya Bagamoyo ni kuua bandari ya Dar,Mtwara na tutapoteza pesa ndefu zaidi,ni heri mradi usitishwe ili tuziendeleze bandari zetu kwa kumiliki mapato yote kuliko akili ya Mstaafu ilivyokuwa.

Safi sana Ancle Magu
 
Ndugu yangu faizaFoxy, kwanza nashukuru sana kwa mawazo yako, walau tunaelekea sehemu nzuri, maana hoja zilizokuwa zinatoka sikuzielewa, maana investment ya 10 B usd sio ya kukataa hivi hivi, Tanzania inahitaji investment za maana sio mchezo mchezo maana tuko kwenye dunia ya ushindani. Lakini swala kama hili magufuli alitakiwa awaambie hii bandari haina uhusiano na issue za kijeshi, na ni opportunity pekee kwa taifa letu. Nakumbuka ujenzi wa TAZARA , Mwl aliwaomba wamarekani waje wasaidie kujenga reli Tanzania wakakataa, ndipo mwl akaenda kuomba wachinese, walipokulbali wamarekani walimpiga vita sana mwl, lakini bahati nzuri mwl na mao ze dong walikuwa ni watu wenye msimamo ,hatimaye reli ile kujengwa. Hapa kuna watu wanabeza investment of 10 B USD, lakini hawajui impacts zake katika uchumi wa tanzania, na hapa kuna nchi nyingi sana zinahofia competitions kati ya tanzania na nchi hizo baada ya Bandari hii kukamilika. My take, ilikuwa ni bora Tanzania, china, Oman na USA wajadili hii issue kabla hajaifuta. Maana tunaoathirika ni sisi.
Nimeshakuambia wachina wa mwalimu si wachina wa leo wa karanga, midoli kariakoo na biashara ya meno ya tembo na faru. Nakuhakikishia hakuna hiyo faida unayofikiria. Kama wana huruma sana watujengee standard gauge railway bila kutaka waendeshe reli kwa miaka arobaini. Hata kama wangeweka sharti hilo faida za reli za moja kwa moja kwa mtanzania wa kawaida akiwemo mfanya biashara na mkulima ni kubwa sana.
 
Habar

Habari ina ukweli kabisa, soma The Citizen, huwa gazeti hili hawaongei mambo ya mitaani.
Serikali Awamu ya Nne inaelekea ilitumia vigezo visivyoeleweka vyema katika sekta nzima ya usafirishaji, hususan bandari.
Bagamoyo haina hata reli ya kuunga bandarini, jipu hilo!
reli ipo
 
Watu Wa Ajabu Sana Kwani Akitokea Bagamoyo Maana Yake Bagamoyo MIRADI Isifanyike????
Tuangalie Merits Sio Nani Anatoka Wapi?
Mbona Magufuli Ameanzisha Usanifu wa Daraja Kuvuka Ziwa Victoria BUSISI Akija Rais Mwingine Asitishe??
Mbona JK Alianzisha MIRADI UDOM,MALAGARASI, KIGAMBONI, KILOMBERO Mingi Tu Huko Ni Kwao.
Wanaotizama Kwa Mtazamo Huo Ni WAKABILA TU.
Fedha Hizi Ni Grant Zingejengwa Reli Na Highways Kuelekea Maziwa Makuu Bagamoyo Ni Pori Na Eneo Kubwa DAR Itakuwaje???
Mtaboresha Bandari Msongamano Wa Malori KUINGIA Na Kutoka Port.
Fanyeni Muende Leo Muone Foleni Inaanzia Uwanja wa TAIFA KUINGIA.
Kutoa Unapakia Kutoka Saa 4 Na Zaidi Bagamoyo Tulikuwa Na Option ya Kudesign Tutakavyo.
Nchi Hii Wivu, Cheap Politics Na Uswahili.
Fedha Sio Zetu Wataondoka Wapeleke Kwingine.
Kenya, Uganda Na RWANDA 4 Billion Za Standard Gauge Na 6 Billion Za LAPPSET Wanahangaika Miaka 6 Sasa Nchi 3.
Sisi Tumebahatika SIASA ZA FITNA NA UKABILA Kuliko Mantiki Tunaharibu.
Tutajuta Nipo.
Braza kwani kuboresha hizo bandari unafukiria ni nini?
Miundombinu ndo kitu cha kwanza kwani ni kweli kwamba pamejaa lakini kama kutakua na bandari kavu huko kibaa na miundombinu ya reli ikiwa freshi hamna lori litakalo ingia town rather reli itafanya kazi yake

Pili ujenzi wa bandari ya bagamoyo automatically ungeua bandari ya dar
 
HI kitu nilijua tu kama ingetokea hivyo; niliwahi pia ku- comment kama sio humu basi kwenye mitandao mingine ya kijamii! Kiuhalisia ule mradi ulikua hauna TIJA yoyote kwa nchi. Thanks Magufuli, kwa hili nakuunga mkono pia.
Namuunga MKONO Rais Magufuli 101%,hapa naoana kwa dhati kabisa amedhamiria kuliokoa Taifa hili! Ule mradi haukua na tija kabisa! Maamuzi sahihi kwa wakati sahihi!
 
Ninachotaka kukisema ni kwamba Katiba haimzuii Raisi kuwa mbaya na mwizi
Hayo yanawezekana pale kama ulivyosema wewe mwenyewe kwamba kiwango cha elimu ya Uraia kikiwa kiko chini. Nafurahi kwa mara ya kwanza umekubali kwamba uwekezaji kwenye Elimu ndiyo suluhisho la kuwa na Jamii inayojali Katiba. Lakini pia haiwezekani mtu anaingia kwa Katiba iliyopo halafu asiiheshimu katiba hiyo hiyo kama si kwamba wale wanaoongozwa hawajui watokakako wala waendako!!

Na hili la kuachiana madaraka kwa kweli kama si Mwalimu ambaye akiwa hai alilisimamia sana sijui kama hata hapa kwetu waongeza muda wasingekuwepo. Hapa hoja ya msingi ni kuwa na Jamii inayoweza kuwalazimisha watawala kutii Katiba. Tatizo Afrika ni rahisi watu kuwagawa Kidini, kikabila, kiukoo na mwisho wa siku anayevunja Katiba hujifanya kulinda Kabila, dini, Ukoo, chama, au jinsia yake dhidi ya wale wanaomhimiza kulinda Katiba!
 
Mradi huu bado upo..umesitishwa kwa muda tu. Tatizo waliopewa kazi ya kusaka fedha wanachechemea.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom