Rugemalila yupo kwenye project ya Tanga na sio Bagamoyo na gharama za project ya Tanga ni mara 3 ya project ya Bagamoyo-- na wao ndoto yao ni deep sea port!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Rugemalila yupo kwenye project ya Tanga na sio Bagamoyo na gharama za project ya Tanga ni mara 3 ya project ya Bagamoyo-- na wao ndoto yao ni deep sea port!
Sasa wewe tusaidie kidogo. Kama ushuru wote wa bandari kwa maana mapato yatachukuliwa naTRA Wachina watarejesha vipi fedha zao walizowekeza. Inawezekana binafsi sijajua vizuri. Biashara ya bandari yapo mapato ya aina ngapi. Kwa msaada niambie yapi yatakua ya mchina na yapi yatakuwa ya serikali.Kuna Mdau mmoja hapa nimemuuliza hayo mapato yote ni mapato yapi lakini hajanijibu labda nisaidie wewe kunipa darasa!!
Can I tell you something?! I am afraid ikiwa kweli unalifahamu vizuri hili suala kwa jinsi issue ya kodi ulivyoita vikodi!!
Guys, pesa nyingi bandarini inachukuliwa na TRA na sio TPA!! Na mapato ya TRA yanaongezeka kadri mzigo unaopitia bandarini unavyoongezeka; keeping other factors constant! Pesa inayoingia bandari ni ndogo sana ukilinganisha na inayoenda TRA! Na kv bandari ya Dar hawana eneo kubwa kimapato ndo wanaathirika zaidi na ndio maana sehemu kubwa ya mzigo unahifadhiwa na Privately owned ICDs!
Kule Bagamoyo, hata kama bandari itakuwa funded na Wachina kwa 100%; mapato/kodi za TRA through imports and export Mchina hazigusi kwahiyo ndo maana umenishangaza unaposema vikodi unless kama unamaanisha kodi zitazolipwa na Wachina wenyewe! Ikiwa bandari itakuwa na uwezo wa kupitisha mzigo mara 3 ya sasa, maana ake ni kwamba hata mapato ya TRA yatapanda kwa similar proportionality!
Halafu nitarudia tena kwako!! Bandari 3 au 4 sio nyingi kama mnavyodhani.... kwa sasa zinaweza kuonekana nyingi kv we don't produce so we don't export! Likewise, our purchasing power ni ndogo so we don't import much! Kwahiyo mnaweza kudhani bandari ni nyingi kumbe msingi wake ni bandari kutumiwa na nchi maskini! Leo hii uki-import smart tv milioni moja zitakudodea but assume nchi zinazutumia bandari ya Dar zinakuwa kiuchumi angalau mara tu na hivyo kuongea exports na purchasing power ya imported goods.... hivi bado hapo unaamini Dar port itakuwa abandoned kwa kukosa mzigo?!
Afrika mzima hapana lakini lengo la Mchina ni ku-accomodate East & Central Africa! Don't forget, China ni major exporter to African market!! Sasa basi, kama wewe unaleta bidhaa zako kutoka China au Japan na unazipitishia Mombasa kwenda Rwanda; just do it lakini lengo la Mchina bidhaa zake zote atakazoleta kwa ajili ya East & Central Africa, lengo lake ni kupitishia Bagamoyo badala ya kwenda kupanga foleni Dar au Mombasa! Ana similar project nchini Djibouti kwa ajili ya u kanda ule wa Africa.Hata wewe tatizo la uelewa pia! Unawezaje kujenga Bandari TanZania ikahudumia Afrika nzima? Kivipi unaweza kuniambia? Kwa taarifa yako tu wateja wanaotumia hata Bandari ya Mombasa Kenya huwezi kuwaleta kutumia Bandari yetu ni ngumu sana na hai make economic sense kwao kijiografia sasa iweje Bandari ijengwe Bagamoyo ihudumua Afrika nzima? Unawezaje kumfanya Muethiopia au Msufdani aje kutumia Bandari ya Bagamoyo badala ya Mombasa unaweza kuniambia hilo?
Si umeshaambiwa ipo kisarawe na ina connection za tazara, trl nk? Chige tumeshaliwa sana!Kupisha miundombinu ipi wakati according to the Citizen, wanataka kuonesha gati 1-7; 13 & 14 za bandari ya Dar na kisha kuboresha Mtwara!
Lakini vilevile hakuna anayepinga kuboresha bandari ya Dar lakini huwezi kusitisha mradi mkubwa kama wa Bagamoyo kwa ajili ya Dar ambayo nishasema hapo awali kwamba hata maeneo ya kujenga container depots hamna unless kama wanakusudia kuimaliza Temeke yote na kuibadilisha kuwa eneo la maghala!
Chief nakubaliana na wewe 100%Sisi/watanzania kinachotufanya tusiendelee kwa sababu ni waoga, na hatupendi ushindani, Bandari ya bagamoyo ni wahisani wanajenga ,na baadae watasimamia huo mradi hadi kipindi watakaporudisha pesa zao, hilo ni wazo zuri, cha msingi serikali ikae na hao wawekezaji waangalie jinsi ya kuendesha mradi huo na kwa kipindi gani, pili serikali awe ni player katika mradi huo, Yaani awe na hisa za kutosha katika mradi huo. Kingine serikali itenge pesa za kujenga bandari za mtwara na Tanga, pia to upgrade dar port, ili watu wawe na options nyingi, na itakusanya mapato na yakutosha na pia kuzalisha ajira za kutosha. tunaweza tukawa na hata bandari kumi, reli za kutosha na 5 airports za maana, lengo ni kuwa na revenue of 5 billions USD per month, hapo ndo tutapata maendeleo.
Bei ya ardhi Bagamoyo itashuka sasa
Nimeshakuambia wachina wa mwalimu si wachina wa leo wa karanga, midoli kariakoo na biashara ya meno ya tembo na faru. Nakuhakikishia hakuna hiyo faida unayofikiria. Kama wana huruma sana watujengee standard gauge railway bila kutaka waendeshe reli kwa miaka arobaini. Hata kama wangeweka sharti hilo faida za reli za moja kwa moja kwa mtanzania wa kawaida akiwemo mfanya biashara na mkulima ni kubwa sana.Ndugu yangu faizaFoxy, kwanza nashukuru sana kwa mawazo yako, walau tunaelekea sehemu nzuri, maana hoja zilizokuwa zinatoka sikuzielewa, maana investment ya 10 B usd sio ya kukataa hivi hivi, Tanzania inahitaji investment za maana sio mchezo mchezo maana tuko kwenye dunia ya ushindani. Lakini swala kama hili magufuli alitakiwa awaambie hii bandari haina uhusiano na issue za kijeshi, na ni opportunity pekee kwa taifa letu. Nakumbuka ujenzi wa TAZARA , Mwl aliwaomba wamarekani waje wasaidie kujenga reli Tanzania wakakataa, ndipo mwl akaenda kuomba wachinese, walipokulbali wamarekani walimpiga vita sana mwl, lakini bahati nzuri mwl na mao ze dong walikuwa ni watu wenye msimamo ,hatimaye reli ile kujengwa. Hapa kuna watu wanabeza investment of 10 B USD, lakini hawajui impacts zake katika uchumi wa tanzania, na hapa kuna nchi nyingi sana zinahofia competitions kati ya tanzania na nchi hizo baada ya Bandari hii kukamilika. My take, ilikuwa ni bora Tanzania, china, Oman na USA wajadili hii issue kabla hajaifuta. Maana tunaoathirika ni sisi.
reli ipoHabar
Habari ina ukweli kabisa, soma The Citizen, huwa gazeti hili hawaongei mambo ya mitaani.
Serikali Awamu ya Nne inaelekea ilitumia vigezo visivyoeleweka vyema katika sekta nzima ya usafirishaji, hususan bandari.
Bagamoyo haina hata reli ya kuunga bandarini, jipu hilo!
Braza kwani kuboresha hizo bandari unafukiria ni nini?Watu Wa Ajabu Sana Kwani Akitokea Bagamoyo Maana Yake Bagamoyo MIRADI Isifanyike????
Tuangalie Merits Sio Nani Anatoka Wapi?
Mbona Magufuli Ameanzisha Usanifu wa Daraja Kuvuka Ziwa Victoria BUSISI Akija Rais Mwingine Asitishe??
Mbona JK Alianzisha MIRADI UDOM,MALAGARASI, KIGAMBONI, KILOMBERO Mingi Tu Huko Ni Kwao.
Wanaotizama Kwa Mtazamo Huo Ni WAKABILA TU.
Fedha Hizi Ni Grant Zingejengwa Reli Na Highways Kuelekea Maziwa Makuu Bagamoyo Ni Pori Na Eneo Kubwa DAR Itakuwaje???
Mtaboresha Bandari Msongamano Wa Malori KUINGIA Na Kutoka Port.
Fanyeni Muende Leo Muone Foleni Inaanzia Uwanja wa TAIFA KUINGIA.
Kutoa Unapakia Kutoka Saa 4 Na Zaidi Bagamoyo Tulikuwa Na Option ya Kudesign Tutakavyo.
Nchi Hii Wivu, Cheap Politics Na Uswahili.
Fedha Sio Zetu Wataondoka Wapeleke Kwingine.
Kenya, Uganda Na RWANDA 4 Billion Za Standard Gauge Na 6 Billion Za LAPPSET Wanahangaika Miaka 6 Sasa Nchi 3.
Sisi Tumebahatika SIASA ZA FITNA NA UKABILA Kuliko Mantiki Tunaharibu.
Tutajuta Nipo.
Namuunga MKONO Rais Magufuli 101%,hapa naoana kwa dhati kabisa amedhamiria kuliokoa Taifa hili! Ule mradi haukua na tija kabisa! Maamuzi sahihi kwa wakati sahihi!HI kitu nilijua tu kama ingetokea hivyo; niliwahi pia ku- comment kama sio humu basi kwenye mitandao mingine ya kijamii! Kiuhalisia ule mradi ulikua hauna TIJA yoyote kwa nchi. Thanks Magufuli, kwa hili nakuunga mkono pia.
Kufanya long term plans zako kutegemea plan za serikali zilizo kwenye makaratasi bado ni kamari ya hali ya juu!Bei ya ardhi Bagamoyo itashuka sasa
Hayo yanawezekana pale kama ulivyosema wewe mwenyewe kwamba kiwango cha elimu ya Uraia kikiwa kiko chini. Nafurahi kwa mara ya kwanza umekubali kwamba uwekezaji kwenye Elimu ndiyo suluhisho la kuwa na Jamii inayojali Katiba. Lakini pia haiwezekani mtu anaingia kwa Katiba iliyopo halafu asiiheshimu katiba hiyo hiyo kama si kwamba wale wanaoongozwa hawajui watokakako wala waendako!!Ninachotaka kukisema ni kwamba Katiba haimzuii Raisi kuwa mbaya na mwizi