Serikali yasitisha Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Kuimarisha Bandari za Mtwara, Dar

Status
Not open for further replies.
Labda tuseme hivi... assume umeagiza gari inapita pale bandaring. 20% ya adjusted value ya hiyo gari inaenda TRA. Sasa kama thamani ya gari ni 1 million; TRA wanachukua laki 2 yao na thamani ya gari hapo inakuwa 1.2 ambapo unakumbana tena Value Added Tax ya 20 or 25% ya hiyo 1.2M.... which means, kama ni 25% ina maana TRA hapo wanachukua laki 3 (mbali na ile laki 2 ya kwanza)! Hiyo laki 3 wanaipandisha juu ya hiyo q.2M na gari yako inakuwa na thamani ya 1.5M halafu wanakutungua excise duty nadhani 20% ya hiyo 1.5 ambayo itakuwa laki 3... which means kwenye ile gari ya 1M TRA watachukua 2+3+3 laki 8! Na ndio maana watu ukiwauliza gharama za ushuru wanakujibu fasta chukua gharama ya gari times 2!

Sasa basi; pesa hiyo always ni ya TRA hata kama bandari ni ya Mchina kwa 100%.

Bandari nao wana ushuru wao na unaofahamika sana ni wharfage na corridor levy. Na hii kitu haifiki hata robo ya ile inayoenda TRA!! So, kwa issue ya Bagamoyo, hiyo wharfage na corridor levy ndo itaenda kwa Mchina ambayo nayo lazima wailipie income tax na kwenda TRA!! Itoshe tu kusema kwamba; maumivu ya TRA ni janga na ndo maana watu wanakwepa kodi lakini ushuru wa bandari kama bandari ni wa kawaida sana!

Mapato mengine kwa Bagamoyo yangetokana na uwepo wa eneo kubwa na wangechukua ushuru wa kutosha wa kuhifadhi mizigo baada ya kupita zile cku ambazo unaruhusiwa kuhifadhi free! Hii privilege kwa Dar inapungua kila cku kutokana na uhaba wa maeneo na wanaonufaika ni wafanyabiashara wenye ICDS!

NOTE: Hizo percentage hapo juu naweza nisiwe correct kwa 100% lakini sitakuwa mbali na ukweli.
 
HI kitu nilijua tu kama ingetokea hivyo; niliwahi pia ku- comment kama sio humu basi kwenye mitandao mingine ya kijamii! Kiuhalisia ule mradi ulikua hauna TIJA yoyote kwa nchi. Thanks Magufuli, kwa hili nakuunga mkono pia.
HI kitu nilijua tu kama ingetokea hivyo; niliwahi pia ku- comment kama sio humu basi kwenye mitandao mingine ya kijamii! Kiuhalisia ule mradi ulikua hauna TIJA yoyote kwa nchi. Thanks Magufuli, kwa hili nakuunga mkono pia.
 
Ungebahatika ukawa rais mzalendo ukakuta aliyekutangulia ametoa robo ya nchi hii kwa mwekezaji moja utaona sawa tu na hutakua na chembe ya shaka kama kufanya hivyo kutaiacha nchi yako salama?
 
Mradi wa pili ni wa bomba la gesi. Kutoka moyoni, zile gharama zingetumika kujenga ULTRA HIGH TENSION line kutoka Mtwara naamini kwa dhati kabisa tungebakiza Change. Bomba la gesi pamoja na nia njema(if at all so), limegharim gharama kubwa ambazo kadri ya hali ya Umeme iliyopo kwa sasa hairidhishi na matrillion yale yaliyotumika na hali ya umeme nchini hazi-TALLY/endani. Ila ndo hivyo ishatokea lakini kipekee naamini tuliERROR somewhere hasa kwa uhaba tulionao wa Rasilimali fedha, mradi unaonekana siyo FEASIBLE!
 
Kwa hili nisipompongeza Magufuli nitakuwa mnafiki mkubwa, pia nitakuwa mnafiki mkubwa kama sitajisuta nafsini mwangu kama mtanzania/mwananchi nimekuwa mnafiki kwa hili. Hivi sikuwa na kanafasi cha kusemea? Hivi wananchi tungeungana kupaza sauti zetu kweli isingesikika? Hivi waandishi wangepaza sauti kupitia kalamu zao zisinge sikika?. Hii ndiyo Tanzania hata siku tunaweza kuuzwa tukaishia kuongelea tumboni tu "jamani tunauzwa hata mwisho tumeuzwa bado tutasemea tumboni tu tumeuzwa"
 
Safi sana JPM barabara ya Msata Bagamoyo inawatosha
 
"The project has been suspended and not cancelled" ... Sijui mmeelewa ama mnakurupuka kuchangia kwa mihemko?!
 
Duh! We jamaa wewe!! Yaani kv capacity ya uchumi wetu ni import and export value ya $X billions basi ndo tunatakiwa kujenga Bandari yenye uwezo wa ku-cater hiyo workload!!! Then what? Uchumi ukipanda unapanua; ukipanda unapanua tena na tena... yaani ujenzi wa bandani unaangalia miaka 5-10 wakati project kubwa kama za bandari zinatakiwa kuangalia at least miaka 50 ijayo!

Si ushawahi kufika pale Airport Terminal II? Historia ya ule Uwanja umefunguliwa early 1980's na wakati huo lilikuwa linaonekana bonge la liji-terminal lakini in less than 30 years Terminal II ikaelemewa...
 
Hii bandari ndo ingekuwa bandari maarufu ya wapiga dili ulimwenguni!! Si hivo tu, hata hivyo bandari ya Dar es salaam ingekwishiney!!
 


Sasa hauoni kama tungejenga Terminal III ya kuchukuwa abiria milioni 6 /mwaka, mwaka 1980 ingekuwa ni white elephant project? Ambapo leo hii ni lazima tungeuvunja tu kwa maana kwanza ungekuwa umechakaa na usingekuwa wa kisasa kulingana na teknolojia iliyopo? Halafu kama wakati huwo watu waliokuwa wanatumia uwanja wetu walikuwa chini ya Milioni huoni kwamba jengo la kuchukuwa milioni 6 lingekuwa ni hasara kubwa?
Haya ndiyo mambo yanayotushinda Afrika, ni wapi tutumie fedha na miradi ya aina gani tuanzishe!

Ndiyo maana kwenye uchumi kuna projections hiyo project ni white elephant ni feasible zaidi kama tukiwekeza kwenye Bandari ya Tanga, Mtwara, kwenye maziwa yetu Kigoma, Mwanza, Musoma, Bukoba Ziwa Nyasa kote huko kunahitaji Bandari na hii ina make economic sense klk kutumia mabilioni kujenga Bandari Bagamoyo wakati 100 km kuna Bandari tayari ya Dar!

Hakuna mtu anayeelewa uchumi ambaye anaweza kuukubali mradi kama huu, hauna tija kabisa!
 
Bandari ya bagamoyo ilikua ni ubinafsi tu... Hatuwezi kuingia mkopo wa trilioni 22kujenga bandari bagamoyo wakati bandari ya dar hatujaiutilize hata kwa 50% ya uwezo wake, lakini pia tulikua na mpango wa utanuzi wa bandari ya dar, tuendelee na upanuzi na sio kujenga ingine just 40kms from dar port, mtwara na tanga nazo zinahitaji kuboreshwa ili ziweze kupiga kazi ipasavyo..

Nini kifanyike: tuendelee na upanuzi wa dar port, tufufue reli yetu kwa kiwango cha kimataifa tutapiga hatua
 
Hawa walisitisha huu mradi wafunguke zaidi walichokuta huko ndani ni kitu gani?
Hadi kufikia uamuzi huu?
 

98%= A+
 
Sasa Ultra High Tension Line si ingetumika kusafirishia umeme na co gas?! Au kuna UHT Line zinazotumika kusafirisha gas?! Kama unacholenga ni kusafirisha umeme basi ulazima wa bomba la gesi ungebaki pale na sooner or later tungejenga tu wakati tumeshagharamika kwenye UHT Line. Nasema lazima tungeingia gharama nyingine za bomba la gesi coz" suala la kusafirisha raw gas toka Kusini hadI Dar es salaam haliepukiki unless kama tunge-opt gas yote iwe exported.
Lakini kwa upande mwingine; kwa hapa tulipofikia; kukiwa na additional supply ya gas kutoka Mtwara; hatutaingia gharama nyingine kv miundombinu ya usafiri shati (bomba) tayari ipo. Umeme bado majanga coz' gas inayotoka Mtwara hivi ni kidogo kwa kuwa uchimbaji wa deep sea kwenye gas nyingi haujaanza
 
Last edited by a moderator:
Leo ndo nimekiri kuwa tanzania hatuwezi kuanzisha na kusimamia miradi mikubwa , ni wazuri sana kwa kubuni, likija swala la implementation tunakimbia. Leo tumeanza issue za kusema mara ohhh we need standard gauge reason behind kenya wanajenga standard gauge, huu mradi wa reli upo, na juzi kati tulisikia mzee six anasema wameweka jiwe na msingi, kwa hiyo ni wawekezaji wawili tofauti. Inabidi tuondokane na tabia hii ya kuogopa ogopa, we can have all simultaneously, uchumi wa kati hauji kwa maneno tu na kukumbatia miradi kama ya upanuzi, sijui upgrade, kujenga mabanda /containers za kufanyia clearance Tanga/Mtwara. Tunaridhika kabisa na tunakaa hapa tunahesabu ohh tuna bandari tatu, ziko wapi hizo bandari tatu tanzania? its jokes.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…