Labda tuseme hivi... assume umeagiza gari inapita pale bandaring. 20% ya adjusted value ya hiyo gari inaenda TRA. Sasa kama thamani ya gari ni 1 million; TRA wanachukua laki 2 yao na thamani ya gari hapo inakuwa 1.2 ambapo unakumbana tena Value Added Tax ya 20 or 25% ya hiyo 1.2M.... which means, kama ni 25% ina maana TRA hapo wanachukua laki 3 (mbali na ile laki 2 ya kwanza)! Hiyo laki 3 wanaipandisha juu ya hiyo q.2M na gari yako inakuwa na thamani ya 1.5M halafu wanakutungua excise duty nadhani 20% ya hiyo 1.5 ambayo itakuwa laki 3... which means kwenye ile gari ya 1M TRA watachukua 2+3+3 laki 8! Na ndio maana watu ukiwauliza gharama za ushuru wanakujibu fasta chukua gharama ya gari times 2!Sasa wewe tusaidie kidogo. Kama ushuru wote wa bandari kwa maana mapato yatachukuliwa naTRA Wachina watarejesha vipi fedha zao walizowekeza. Inawezekana binafsi sijajua vizuri. Biashara ya bandari yapo mapato ya aina ngapi. Kwa msaada niambie yapi yatakua ya mchina na yapi yatakuwa ya serikali.
Sasa basi; pesa hiyo always ni ya TRA hata kama bandari ni ya Mchina kwa 100%.
Bandari nao wana ushuru wao na unaofahamika sana ni wharfage na corridor levy. Na hii kitu haifiki hata robo ya ile inayoenda TRA!! So, kwa issue ya Bagamoyo, hiyo wharfage na corridor levy ndo itaenda kwa Mchina ambayo nayo lazima wailipie income tax na kwenda TRA!! Itoshe tu kusema kwamba; maumivu ya TRA ni janga na ndo maana watu wanakwepa kodi lakini ushuru wa bandari kama bandari ni wa kawaida sana!
Mapato mengine kwa Bagamoyo yangetokana na uwepo wa eneo kubwa na wangechukua ushuru wa kutosha wa kuhifadhi mizigo baada ya kupita zile cku ambazo unaruhusiwa kuhifadhi free! Hii privilege kwa Dar inapungua kila cku kutokana na uhaba wa maeneo na wanaonufaika ni wafanyabiashara wenye ICDS!
NOTE: Hizo percentage hapo juu naweza nisiwe correct kwa 100% lakini sitakuwa mbali na ukweli.