Serikali yasitisha Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Kuimarisha Bandari za Mtwara, Dar

Status
Not open for further replies.


Kwa kuwa Kenya wanajenga Bandari kubwa Lamu haimanishi kwambo wako sawa, isitoshe sielewi mambo ya Kenya, lkn kwa hapa kwetu huu mradi wa Bandari ya B'moyo ni white elephant na haumake economic sense Serikali ya Magufuli siyo wajinga kuupiga stop na kuhamishia nguvu kule ambako tayari kumeshajengwa na kunahitaji kuboreshwa tu!

Unajua nini? Mimi angalau ningewaelewa watu mnaong'ang'ania huu mradi kama kwa mfano Bandari za Dar, Tanga, na Mtwara zote zingekuwa zinaeffieciency ya mpaka 95% hapo sasa ndiyo mngesema Bandari zetu zimezidiwa tumefanya kila kitu na sasa tunahitaji Bandari kubwa zaidi lkn siyo kweli Bandari ya Dar yenyewe siyo kwa sababu wala ni ndogo bali ni inafanya kazi below its capacity by far , mpka leo hii hata kuhakikisha tu mzigo wa mteja haubiwi na unafika salama bado hatuwezi, ni juzi hapa Rwanda wamelalamika kuibiwa makontena yao na kupata hasara na siyo Rwanda tu Kongo hata Malawi ni kwamba hawana jinsi lkn wameshachoka sasa hapo wala bado sijaongelea mambo ya effieciency ya upakuaji mizigo, uhifadhi, n.k na hiyo ni Dar ,Tanga wala sijagusia MT sasa kama hizi Bandari zilizojengwa na Wakoloni miaka 100 iliyopita tunashindwa kuzifanya ziwe na effiecincy ya angalau 85% tunataka kujenga Bandari yaDola Bilioni 10 hiyo miuijiza itatoka wapi?

Ni sawa una nyumba ya vyumba viwili unashindwa kuisafisha na kukata majani vyoo vinanuka halafu unasema unataka kujenga nyumba mpya ya vyumba 7 ili uishi vizuri na kwa usafi zaidi hakuna atakaye kuamini!
 
Swali linabaki pale pale na wanalikimbia

Hivi akina Mh Magufuli, Mbarawa, Mwakyembe na wengine hawayakuyaona haya? Je, walipaza sauti lini kupinga haya ?

Je, maamuzi ya miradi mikubwa kama huu yanaongozwa na nini? Wataalamu au wanasiasa?

Pesa zipo kufuatana na video aliyoweka JokaKuu , nini kimebailika kiutaalamu?
 
Lakini Magufuli alikuwemo katika baraza la mawaziri lililokubali 'white elephant'' unataka tuelewe vipi, kwamba wakati huo alikuwaje ili kulinganisha na sasa? Please tuelezeni maana CCM ni ile ile, kamati kuu ni ile ile, magogoni ni wale wale

Hapa tusikwepe , kuna uzembe ambao hatupaswi kufunika kombe.

Wakati mradi unafanyiwa mchakato umegharimu pesa nyingi sana in terms of resource, pesa ambazo zingeweza kujenga kachuo kadogo au kurepea MRI nyingi tu.

Walikuwa kimya, leo mnasema si wajinga wa kukubali white elephant! walikuwa wapi na ujanja wameupata lini

Alinda dalili za uchovu zi wazi. Tuliwambia huwezi kumvisha chui ngozi ya kondoo ukamwaita kondoo mpya!

Nyani Ngabu The Boss wameanza kuelewa
 
Last edited:
Iko siku hapa JF tutakuja zungumzia swala hili tukiwa tumechelewa huku tukichekwa kama Mazombie kila kitu kwetu ni Ushabiki usio na tija
 
Hapo wawekezaji walioingia mikataba watakula fedha ya bure kama hii habari ni ya ukweli.
Watakulaje hela wakati wao ndio walikuwa wanatoa hela? Serikali haijaweka hela zake katika mradi huo.
 
Wakati wenzetu wananunua suruali mpya sisi tunaziba viraka.Angalia kenya wanavyochakarika port ya mombasa ilikuwa bora Africa mashariki laakini sasa wanashusha modern port lamu sisi tunaenda kuziba viraka vya kurasini na maajengo mtwara.Tusipokuwa na viongozi wenye upeo na wanaoweza kujua dunia inaenda vipi tutabaki kulalamika shilingi inashuka.Magufuli usidanganywe wenzako hawakuwa wajinga kupanga mipango ya kimaendeleo kwa kwenda na wakati port ya Bagamoyo ni uamuzi sahihi wake up man
 

Mkuu wangu hii NCHI inaongozwa kwa mihemko ya MTU yyt anaeingia Ikulu haina mipango inayoeleweka.....
 
Huu ujinga unafanyika Tanzania tuu watu wanafanya maamuzi ya kukurupuka sana
 
Hayo maneno kwenye rangi nyekundu yahusika! Ukitaka mtanzania (soma mdanganyika) asihoji chochote kuhusu mradi wa kijinga na usio na manufaa mwambie huu mradi ni mkubwa kuliko yote Afrika Mashariki au Afrika au Duniaani! Umemmaliza! Ataridhika na kuzuuza roho yake. Wala hawezi kujiuliza ''hata kama ni mradi mkubwa so what! Una faida gani kwetu!'' Pasco na hawa wanasiasa uchwara wanajua zaidi ndio maana hawaishi kubwagiza na haya maneno...
 
Walikuwa kwenye baraza la mawaziri na hawakuwahi kupinga ili hata kuweka kumbukumbu. Hii nchi ni hatari sana. Kila rais anayeingia anaingia na vituko vyake. Sasa huo mkataba ukivunjwa itakuwaje?
 
Uwe uamuzi sahihi au la, alikuwemo ndani wakati maamuzi yanapitishwa

Tusimsukumie mzigo mtu mwingine, ni hawa hawa walikuwa katika harakati tena wakipiga kampeni za kutaja mradi.

#Hapa kazi tu, hapamauza uza tu
 
Walikuwa kwenye baraza la mawaziri na hawakuwahi kupinga ili hata kuweka kumbukumbu. Hii nchi ni hatari sana. Kila rais anayeingia anaingia na vituko vyake. Sasa huo mkataba ukivunjwa itakuwaje?
Hapa tunaimba nyimbo tu wenzetu wanachanja mbuga. JK ana la kusema kuwa mradi huo ulikuwa na faida

Magufuli alikuwemo, sasa anasema hapana. Huyu ndiye wa kutueleza nini kimebadilika alichokuwa hakioni wakati huo?

Kila siku tunalishwa 'kashata' mpya, tunaimba tu hatufikirii. Hatuna maono na nchi yetu

Tusubiri tangazo siku moja, mtu ataamka asubuhi na kusema akina baba wahasiwe, population imekuwa kubwa!

Mungu pishilia mbali , twaweza fyekwa tu.
 
Kiroho saaaaaaafi na kwaaaaaaaaaaaaaaaaaatuuuuuuuuuuuuuuuuu......! Nampongeza Waziri wa Kazi, Uchukuzi na mawasiliano kwa kutumia Weledi wake katika mambo ya kitaifa kama haya.
 
EDDO alipokuwa anapinga hilo swala wengi walimkejeli sana
 
Shikamoo yako baba maghufuli!! Kweli wewe jembe na ni mzalendo wa kweli endelea vivyo hivyo wasiopenda wale malimao
 
Ombeni kwani ni mshauri wa rais?acheni kumharibia mzee wa watu,kwanza walimtoa UN ambako huko hamna uswahili lkn akivoletwa huku ndo akakutana na habati ya mkwere ss hata ungekuwa ww ungefanyaje?
 
Nilisikia mkataba huu unawapa wawekezaji wa China kuendesha hiyo bandari kwa muda wa miaka 50 mpaka watakaporudisha pesa zao na hapo Tanzania ndo itapewa bandari yake.
 
It's about time!! The only port worth of spending that kind of dough is Mtwara because the benefits are known, and return to investment is quicker and realistic. Instead of developing Bagamoyo port they should have strengthened the road/rail to Bagamoyo and strengthened the Dar port. Even Tanga has better development merit than Bagamoyo! Bravo the new government.
 
Yaan we acha tu.. Bila KATIBA MPYA YA WARIOBA hii nchi akija rais mwingine yatarudi hayahaya tunayoyalalamikia..
Pigania Katiba Mpya kwa maslahi mpana na ya mbele ya nchi..
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…