Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,817
Hoja hapa ni kwamba project kubwa kama bandari huangalii miaka 10-20 ijayo bali unaangalia over 50 years!! Ikiwa unaona Uwanja wa abiria 6M ingekuwa ni white elephant; ni nani kati yetu na Kenya anafaidika kwa kuwa ni gateway? Ule Uwanja wa Jomo Kenyatta umejengwa miaka ya 70... leo hii, Kenya wanaona Jomo Kenyatta haitoshi na wanataka kujenga terminal itakayo-accomodate 20 million passengers annually wakati kwa sasa wanapokea roughly 6 millions!!! Na bila shaka nadhani unafahamu kwamba pamoja na Mombasa kuwa ni bandari kubwa kuliko Dar lakini kv wenzetu wanaangalia 50 years to come; nao wana mega project sawa na ya Bagamoyo ambayo wanataka kujenga Lamb! Kama kumbukumbu zangu zipo sawa, nadhani ule mradi walitaka ku-team up na China lakini China wakaamu kuja Bagamoyo probably kv tayari wana another mega project Djibouti!!
Kwa staili hii Wakenya wana kila sababu ya kutuona maboya....
Kwa kuwa Kenya wanajenga Bandari kubwa Lamu haimanishi kwambo wako sawa, isitoshe sielewi mambo ya Kenya, lkn kwa hapa kwetu huu mradi wa Bandari ya B'moyo ni white elephant na haumake economic sense Serikali ya Magufuli siyo wajinga kuupiga stop na kuhamishia nguvu kule ambako tayari kumeshajengwa na kunahitaji kuboreshwa tu!
Unajua nini? Mimi angalau ningewaelewa watu mnaong'ang'ania huu mradi kama kwa mfano Bandari za Dar, Tanga, na Mtwara zote zingekuwa zinaeffieciency ya mpaka 95% hapo sasa ndiyo mngesema Bandari zetu zimezidiwa tumefanya kila kitu na sasa tunahitaji Bandari kubwa zaidi lkn siyo kweli Bandari ya Dar yenyewe siyo kwa sababu wala ni ndogo bali ni inafanya kazi below its capacity by far , mpka leo hii hata kuhakikisha tu mzigo wa mteja haubiwi na unafika salama bado hatuwezi, ni juzi hapa Rwanda wamelalamika kuibiwa makontena yao na kupata hasara na siyo Rwanda tu Kongo hata Malawi ni kwamba hawana jinsi lkn wameshachoka sasa hapo wala bado sijaongelea mambo ya effieciency ya upakuaji mizigo, uhifadhi, n.k na hiyo ni Dar ,Tanga wala sijagusia MT sasa kama hizi Bandari zilizojengwa na Wakoloni miaka 100 iliyopita tunashindwa kuzifanya ziwe na effiecincy ya angalau 85% tunataka kujenga Bandari yaDola Bilioni 10 hiyo miuijiza itatoka wapi?
Ni sawa una nyumba ya vyumba viwili unashindwa kuisafisha na kukata majani vyoo vinanuka halafu unasema unataka kujenga nyumba mpya ya vyumba 7 ili uishi vizuri na kwa usafi zaidi hakuna atakaye kuamini!