Serikali yasitisha Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Kuimarisha Bandari za Mtwara, Dar

Status
Not open for further replies.
Kujengwa banadari mpya na ya kisasa kupisha bandari ya dar ambayo haina nafasi ni uharibifu?

Hakika shule mlienda kusomea ujinga.
Hiyo bandari wachina wanaiendeaha kwa miaka 50 ndo Tanzania mrudishiwe bandari yenu. Pamoja na kuwapa hiyo bandari unayosema ni kubwa maana yake ni kuua bandari zetu zilizopo sasa maana ni kama tutakuwa hatupati kitu lutoka kwenye bandari mpya kwa muda wote huo na wakati bandari zetu zitapumguzwa nguvu.
 
Nadhani wengi hawajapa picha kubwa juu ya hii bandari , hii bandari ni pamoja free zone inakayo kuwa na mabohari na viwanda na vyote hivi vinategemewa kuhudimia zaidi ya nchi 10 na idadi ya watu zaidi ya 200 million, badala ya watu kuenda Dubai na Guanzouw watakuwa chukua bidhaa zao toka Bagamoyo na Tanzania inapata mapato na ajira ! pia bandari itakuwa ni transhipment hub - yaani itakuwa ni kituo ambacho makontena yaendayo nchi mbali mbali yana badili meli.
Bandari za Dar, Mtwara na Tanga ni kama stendi za dala dala hazina mfumo wa business ya karne ya 21 ndio maana wizi na ufisadi umeshamiri.
Bandari ya Bagamoyo itakuwa ni most efficient port in Africa na geared to put Tanzania on key mariner / logistic hubs
 
Mkuu nadhani hapa watu wanajadili mada kitaalamu.. Kila mtu anatoa wazo lake, faida na hasara za huo mradi lakini wewe umekomalia mambo ya Magufuli kuwemo kwenye Cabinet, Hivi una uhakika gani JPM aliukubali huu mradi kwenye cabinet?? Je kama walizozana na mwisho zikapigwa kura??

Ni sawasawa leo tuseme Ukawa walishiriki kuupitisha ule mswada wa mafuta na gesi wakati tuliona wazi waliukataa... Wewe ni mtu mzima, tujadili Je, imefaa kuupiga chini mradi au wamechemsaha, na zitolewe sababu... Wakati wa siasa umeisha tusubiri tu 2020, hata sisi tuna hasira kama wewe...
 
Bandari ya Dar itakuwa supplementary.
Jaribu kutetea vitu unavyovifahamu. Ujenzi unafanywa na wachina na manamiliki bandari kwa miaka 50 ili kurudisha pesa walizojengea. Huoni hii itaua bandari za Dar , Tanga na Mtwara ? Huu mradi haukuwa na maslahi ya taifa na nadhani hii kitu iko Tanzania tu.

Siyo kwamba napinga wazo la kuwa na bandari kubwa ila mizengwe iliyomo kwenye umiliki wa bandari ndio sokubaliani nao. Ingewezekana ku raise pesa za hata za ndani kupitia hata kama UTT na tukajenga wenyewe kama serikali haina.pesa kuliko kuuza nchi.
 
Baada ya kusikia hii habari ya kufuta sijui kusitisha ujenzi wa bandari ya Bagamoyo nimechoka kabisa, hii ambayo ingejengwa kisasa na viwanda zone, yaani tanzania ingekuwa ni african stop ya bizaa zote za china, watu walikuwa hakuna haja ya kwenda tena sijui dubai wala china, vitu vyote vinapatikana tz na tuna ship kwenda nchi zote za africa, tuna sema huu mradi haufai? god, hapa kweli tunashida sana. Tunakosa revenue na ajira hivi hivi halafu kesho unasikia mtu anakwenda dubai na kurudi, si watu wengekuwa wanakwenda bagamoyo tu? raisi wetu cabinet lililopita alikuwepo, mradi kama huu ulihusisha cabinet yote, angesema , sio sisi tumekaa mkao wa kura then tunaambiwa hakuna chakula. let us be serious as he nation , we need this project, hizo mtwara , tanga na Dar zina panuliwa lakini haziwezi kukidhi matakwa ya kibisahra na plna zetu muda mrefu, tusiwe na ka plan just ka leo na kesho.
 
JPM si mjinga. Kuna vitu haviwekwi wazi kwenye mikataba na matokeo yake ni watu kuja kuanza kulalamika. We tulia tu utakuka kujua kwa nini huu mradi si priority kama mlivyo aminishwa!
 
Jamani eeeh magufuli yuko sawa.. Na kumbukeni hajafuta kabisa kaweka pending tu.. Wacha tujusanye hela kwanza, tukipata hela huenda tukajenga hiyo bandari kwa hela zetu bila mikopo ya kulazimishwa kukabidhi bandari kwa wachina kwa miaka hamsini
 
Labda ni mgeni kidogo. Kuhusu Bandari tumejadili sana wakati mradi huo ukianza

Kama utakumbuka mradi ulikuwa kujibu mradi wa CoW katika EAC.
Tulisema hivi, kuna hatari ya kuchukua maamuzi ya jazba

Ni lazima kwanza ifanyike study ya kuona faida na hasara za muda mrefu na si kuhamaki.

Katika rekodi, nipo nikisema hivi, bandari ya Dar es Slaam inafanya kazi chini ya kiwango.

Tatizo ni ukosefu wa vifaa na mbinu ikiwemo wizi kutamalaki na kodi zisizovutia wasafiri.

Tukaeleza kwanini eneo muhimu kama bandari liendeshwe na makampuni binafsi yasiyowekeza bali kuleta mitambo ya kukusanya mapato?

Nilisema, yale magati yaliyokuwa yajengwe iligundulika ufisadi kwa kutumia kampuni ile ya China. Hilo ni tatizo kubwa

Tuliendelea, kuna mradi wa bandari ya Mwambani Tanga ambayo ina link na reli ya kaskazini na ya kati.

Bado inaweza kutumika kama bandari ya mizigo ya ndani na ile ya Dar es Slaam ikawa kwa mizigo ya mataifa.
Katika maelezo hayo tulishauri ijengwe bandari kavu ambayo kwasasa ipo kahama.

Msongamano katika bandari ya Dar unaweza kupunguzwa ikiwa wafanyabiashara kutoka Rwanda, Burundi, Uganda au Kongo wataweza kuchukua mizigo yao kutoka bandari kavu katika gharama zinazowavutia.

Hivyo hoja kubwa ilikuwa kuimarisha bandari ya Dar /Tanga /Mtwara zifanye kazi kwa asilimia 100 kwasababu tatizo si ukubwa bali ufanisi.

Ukiende Dubai eneo lao si kubwa kihvyo bali efficiency yake ni superb. Mradi wa Bagamoyo tukashauri uangaliwe kwanza

Kuhusu Magufuli, inawezekana alikataa, hata hivyo alitoka nje katika kampeni na kupigia upatu.
Pitia video zilizowekwa hapa usikie mwenyewe akisema.

Sasa inakuwaje leo anasema mradi huo usitishwe? Alikuwemo na akatumia kama kauli mbiu ya kampeni, miezi michache anageuza kibao.

Hapa ndipo tunahoji kulikoni? Tunajua tunapokwenda au tunaunga tela kwasababu tu !!!!

Hivyo katika mradi huu, Magufuli anaujua kutoka katika Cabinet, na alizungumzia katika kampeni.
Kitu gani unachoona kina kosa kuzungumzia hilo. Hatuwezi kumtwisha JK mzigo mzima ikiwa washirika wake wapo.

Kuhusu sababu za kuahirisha na faida zake au la, hilo halina mashiko kwasasa.

Wameamua kusimamisha! period! Hatuwezi kuwageuza maana hakuna mission wala vision.

Tunachotaka nI watu wajifunze kuelewa kuwa matatizo yetu hayatoki nje, ni yale yale ya miaka 50 na wale waliotufikisha hapa ndio wanatengeneza vision inayosemwa mpya! Vision ya flip flop kucheza na muda kwa matokeo sifuri kama mradi huu unavyoonyesha.
 
Jiongeze ndugu hiyo ni Lugha ya Dipromasia kutuliza mihemko ya mkwere na Genge lake....unadhani ikikaa miaka zaidi ya 50 bila kujengwa utasema haijawa Cancelled au Wameandika na muda
Yawezekana, lakini sidhani kama JPM atamwangusha JK. Labda!!!
 
bandari ya bagamoyo iliwekwa kwa maslahi binafsi ya jk na sio kwa maslahi ya umma..
 
Asanteeeeee Magufuli... atleast MUNGU amekuongoza kuokoa nchi yetu... kwani WACHINA wangemaliza kila kitu..!!
 
Wanasheria naombeni ufsfanuzi hapo, hivi hao wachina wamesitishiwa mkataba kweli? kwahiyo tz itaadhibiwa kwa kubreach contract?
 
Tatizo lako hutaki kuelewa! Kwahiyo unataka kusema efficiency ya bandari ya Dar ikifikia 100% ndo cargo storage haitakuwa tatizo?

Narudia, Bandari ya Dar hata ikiongeza efficiency kwa 100000000000% not mentioning hiyo 100%, watakachofanikiwa ni improvement ya logistics. Kwamba, meli ikifunga nanga, mzigo utapakuliwa na kuwa cleared on time na kwa outward cargo, nayo itakuwa hivyo hivyo! Kwamba, kazi waliyokuwa wanafanya kwa siku 5, kukiwa na efficiency itafanyika kwa dakika 5!!

Hoja hapa ni kwamba bandari ya Dar es salaam haina uwezo wa ku-handle mzigo mkubwa. Kwamba, sawa una supersonic efficiency; inward na outward cargo imeongezeka; sasa na hiyo supersonic efficiency yako itakusaidia nini wakati hauna facilities za kutosha za kuhifadhi mzigo? Ingawaje kuna ICD za watu binafsi, lakini mzigo unapofika mteja ana haki ya kuhifadhiwa mzigo wake kwa siku 7 bila kulipa chochote... kwahiyo, hata kukiwa na ICDs za watu binagsi kila mtaa, bado bandari wana wajibu wa kuhifadhi mzigo wa mteja at least kwa siku 7... kama ndani ya hizo cku 7 itabidi kupelekwa privately owned ICDs, basi wapeleke wenyewe bandari kwa gharama zao!!
Hii yote ni kwa sababu kule bandarini hakuna maghala ya kutosha ya kuhifadhia mizigo! Kwahiyo, efficiency ita-speed up logistics lakini tatizo la msingi litabaki pale pale!

Bandari ya Tanga, nimewahi kupita pale siku moja... sina hakika kama nilichokuwa nimekiona ndicho kilichopo au ile siku maji yalikupwa! Kwa macho yangu nilishuhudia tishari zinatoa mzigo melini na kuleta gatini! Kama hivyo ndo hali yenyewe, basi maanake ni kwamba kuna shallow water.... kama kuna mtu wa Tanga humu anisaidie. But all in all, hivi pale Tanga kuna bandari ya kuboresha pale kama sio kujenga upya!!

Kwamba Kenya kutaka kujenga bandari nyingine haimanishi ndo wapo sawa... hebu jiulize kidogo! Kenya ina raslimali watu na raslimali fedha! Imetumia raslimali zote mbili kufanya feasibility study na wakaona umuhimu wa kujenga bandari kubwa zaidi kutokana na projections zao!! Yaani bado unaamini wewe usiyefahamu hata wanapokea containers ngapi kwa mwezi unaweza kuwa sawa kuliko wao? Sasa wakati nyie mnadhani ndo wataalamu zaidi wa kuzifahamu white elephant projects, Wakenya na Wamarekani kwa kuwa hawana akili hawa hapa: Kwahiyo hapa Wachina hawana akili, Kenya hawana akili, US Companies nao maboya tu lakini nyinyi tena ambao hata shipping business yenyewe hamuifahamu lakini ndo mna uwezo mkubwa wa kufahamu viable and white elephant project kwenye ports investments!!!! Sasa ikiwa $ 10 Billion mnaona ni li-project likubwa kwelikweli; what abaout hao ambao target yao ni $26 Billion?

Wengine wanaohangaika kutafuta mikopo kwa ajili ya bandari hawa hapa:

In what appears to be a possible clash with Brazilian mining giant Vale, the government of Mozambique plans to secure funding from China to build a deepwater port in Nacala, in the Nampula province. Vale has announced plans to invest US$5 billion in the construction of a deepwater port in Nacala

Wengine wakati wanelezea strategy za China kujitanua, wanaandika:
China’s strategy is to have key points on the Silk Road space such as Bagamoyo become the key sites for the transcontinental exchange of manufactured goods and commodities between the Asian and African economies along the Maritime Silk Road. Chinese policy-makers are convinced that the benefits of China’s infrastructure-driven development model can also be transferred to Africa. Pamoja na yote hayo, bado mnaona Wachina ni wapumbavu wa kutaka kuwekeza Bagamoyo?! Yaani kv Kikwete hatumpendi, ndo basi tena tunaona huu mradi ni kwa manufaa ya Kikwete... yaani Mchina akatafute mkopo wa $ 10 Billion kwa ajili ya kumnufaisha Kikwete!!!

Tatizo la Watanzania, hata vitu ambavyo hatuna utaalamu navyo tunataka kuvitolea maoni na ku-criticize na tunafanya hivyo bila ku-research wala kuuliza wenye utalaamu na suala husika!!! Yaani unakuta mtu anaibuka from nowhere na kuongea bila woga kwamba pale kina kifupi... muulize kifupi futi ngapi hana jibu... kumbe alikariri Jiografia ya shule ya msingi kwamba Mtwara ndo bandari yenye kina kirefu basi ndo tayari anajiona mtalaamu wa kufahamu wapi panafaa kujengwa bandari na wapi hapafai!!!! Muulize ili kujenga bandari kina kinatakiwa kuwa futi ngapi, hana
jibu lakini bado anataka kuwa-criticize watalaamu ambao wameshafanya study!
 
Last edited by a moderator:
Kupanga ni kuchagua. Uchumi mkubwa katika nchi hii kwa sasa uko kusini hususani mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma na Njombe. Bandari kubwa Bagamoyo ya nini wakati umbali kutoka bandari kubwa iliyopo Dar es Salaam kwenda Bagamoyo ni kilomita 40 tu. Pure wastage of public resouces.
 
...ndio mana bado tunasema serikali iliyoondoka ilijaa unafiki mtupu kwenye mipango yake...na JPM anazidi kujidhihirisha kuwa more realistic kwenye mipango yake...maana haingii akilini blah blah kibao zilizopigwa na serikali ya mkwere kuhusu ujenzi wa bandari ya bagamoyo....not knowing kumbe hawakuwa na funds kwa ujenzi ule!!....yaani waliingia mikataba bila uhakika wa funding!....this is amazing....na zile bla blah sijui za oman funds??wakishirikiana sijui na wachina (exim banks or whatever!!)....yaani wabongo kweli wamedanganywa awamu iliyopita....Mi najiuliza bado kwanini watambe na jenzi hizi wakati pesa hawakuwa nazo????.

......ndio maana hata ma meli na mibehewa walinunua mafeki (used)...na hata ujenzi wa ile standard gauge railway nao lazima watakua walituzuga tu....Hivi jamani tusemezane...ni mipango gani ilipangwa na serikali ya mkwere ikatekelezeka????i mean lets be realistic....je mtu humu sasa atuambie mpango mmoja tu wa utawala wa mkwere uliotekelezeka....maana hata kwenye elimu yale madaraja ya viwango vya chini sasa Prof. Ndalichakom anataka kufumua.....hata yale ma mipango ya BRN nayo yamefia baharini...hujasema bado kilimo kwanza...sijui operation tokomeza....ujenzi wa magati ya bandari hakuna.....sasa nini kilipangwa kikatekelezeka kwa asilimia 100???....maana hata ujenzi wa udom ni mipango ya Mkapa....daraja lam kigamboni halijaisha.....na hata huo mradi wa DART wa mabasi ya kasi ndio hivyo wamekula sijui hela na mabasi hawajalipia bandarini......sasa tusemeje wajameni???...maana hata wezi waliokwiba escrow hawajashughulikiwa.....
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…