Mkuu nadhani hapa watu wanajadili mada kitaalamu.. Kila mtu anatoa wazo lake, faida na hasara za huo mradi lakini wewe umekomalia mambo ya Magufuli kuwemo kwenye Cabinet, Hivi una uhakika gani JPM aliukubali huu mradi kwenye cabinet?? Je kama walizozana na mwisho zikapigwa kura??
Ni sawasawa leo tuseme Ukawa walishiriki kuupitisha ule mswada wa mafuta na gesi wakati tuliona wazi waliukataa... Wewe ni mtu mzima, tujadili Je, imefaa kuupiga chini mradi au wamechemsaha, na zitolewe sababu... Wakati wa siasa umeisha tusubiri tu 2020, hata sisi tuna hasira kama wewe...
Labda ni mgeni kidogo. Kuhusu Bandari tumejadili sana wakati mradi huo ukianza
Kama utakumbuka mradi ulikuwa kujibu mradi wa CoW katika EAC.
Tulisema hivi, kuna hatari ya kuchukua maamuzi ya jazba
Ni lazima kwanza ifanyike study ya kuona faida na hasara za muda mrefu na si kuhamaki.
Katika rekodi, nipo nikisema hivi, bandari ya Dar es Slaam inafanya kazi chini ya kiwango.
Tatizo ni ukosefu wa vifaa na mbinu ikiwemo wizi kutamalaki na kodi zisizovutia wasafiri.
Tukaeleza kwanini eneo muhimu kama bandari liendeshwe na makampuni binafsi yasiyowekeza bali kuleta mitambo ya kukusanya mapato?
Nilisema, yale magati yaliyokuwa yajengwe iligundulika ufisadi kwa kutumia kampuni ile ya China. Hilo ni tatizo kubwa
Tuliendelea, kuna mradi wa bandari ya Mwambani Tanga ambayo ina link na reli ya kaskazini na ya kati.
Bado inaweza kutumika kama bandari ya mizigo ya ndani na ile ya Dar es Slaam ikawa kwa mizigo ya mataifa.
Katika maelezo hayo tulishauri ijengwe bandari kavu ambayo kwasasa ipo kahama.
Msongamano katika bandari ya Dar unaweza kupunguzwa ikiwa wafanyabiashara kutoka Rwanda, Burundi, Uganda au Kongo wataweza kuchukua mizigo yao kutoka bandari kavu katika gharama zinazowavutia.
Hivyo hoja kubwa ilikuwa kuimarisha bandari ya Dar /Tanga /Mtwara zifanye kazi kwa asilimia 100 kwasababu tatizo si ukubwa bali ufanisi.
Ukiende Dubai eneo lao si kubwa kihvyo bali efficiency yake ni superb. Mradi wa Bagamoyo tukashauri uangaliwe kwanza
Kuhusu Magufuli, inawezekana alikataa, hata hivyo alitoka nje katika kampeni na kupigia upatu.
Pitia video zilizowekwa hapa usikie mwenyewe akisema.
Sasa inakuwaje leo anasema mradi huo usitishwe? Alikuwemo na akatumia kama kauli mbiu ya kampeni, miezi michache anageuza kibao.
Hapa ndipo tunahoji kulikoni? Tunajua tunapokwenda au tunaunga tela kwasababu tu !!!!
Hivyo katika mradi huu, Magufuli anaujua kutoka katika Cabinet, na alizungumzia katika kampeni.
Kitu gani unachoona kina kosa kuzungumzia hilo. Hatuwezi kumtwisha JK mzigo mzima ikiwa washirika wake wapo.
Kuhusu sababu za kuahirisha na faida zake au la, hilo halina mashiko kwasasa.
Wameamua kusimamisha! period! Hatuwezi kuwageuza maana hakuna mission wala vision.
Tunachotaka nI watu wajifunze kuelewa kuwa matatizo yetu hayatoki nje, ni yale yale ya miaka 50 na wale waliotufikisha hapa ndio wanatengeneza vision inayosemwa mpya! Vision ya flip flop kucheza na muda kwa matokeo sifuri kama mradi huu unavyoonyesha.