Serikali yasitisha Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Kuimarisha Bandari za Mtwara, Dar

Status
Not open for further replies.
Mmmmhhhhh Kila zama na kitabu chake Mzee wa Lupaso aliondoka na mtwara corridor yake na sasa Mzee wa Msoga Ana ondoka na Bandari ya Bagamoyo
 
Alafu wachina ndio wangeiendesha bandaribkwa kitu kama miaka50 ivi.¡¡¡¡¡kweli kahawa zinadhohofisha uwezo wa kufikiri
 
Hamna lolote ndugu yangu. Hiyo bandari ni white elephant na ingetugharimu sana. Haina kipaumbele chochote ukilinganisha na kuboresha bandari ya dar, tanga na mtwara. Ingepaisha deni la taifa mpaka tuchanganyikiwe. Kama ni viwanda bado vinaweza kujengwa huko bagamoyo.
 
bandar ya dar iko hovyoo,..local sana,,.wanaangaika na bandar mpya,...jk hovyoooooooo sana,.....ashitakiwee kwa matumiz mabaya
Kuna kinga ya rais kutoshtakiwa, bila hivyo Kwa hali jinsi ilivyokuwa wakati wa kuelekea kwenye uchaguzi Mzee wa msoga angeng'ang'ania madarakani
 
bagamoyo kina kifup toka enzi ya mjeruman alishaona ndio mana akahamishia bandari dar, cost za kuchimba chini ni kubwa sana ili kina kiwe kikubwa meli kubwa zipite pili shippers walishasema haitakua na faida yoyote maana bandari ya dar inaitaj improvement tu finally the project is dead and we can all be happy now!!!
 
Magufuli anafanya maamuzi bila kujali nani atafurahi au kununa .... Miaka kumi iliyopita ni kama system nzima ilipigwa ganzi ...
 
...hayo mapesa / watupatie nusu tu,kama kweli walikuwa na nia njema tuimarishe bandari ya dar!,tuipanue ya tanga na mtwara!
yakhee!
 

weka maslahi yako pembeni, umeambiwa bandari za Dar na Mtwara zinaimarishwa.....over
 
This is beyond my comprehension yaani bandari ambayo kwa sasa inatumiwa na mataifa jirani Congo, Rwanda, Burundi na mataifa mengine ya chini mwa Tanzania iwe katikati ya jiji.

Kwa sasa tu magari inabidi ya pakie usiku ambapo ni time consuming kwa wateja wengine kulaza magari ambayo yangekuwa yanawatengezea hela, port ya Bagamoyo si ndio ideal ipo nje ya mji kidogo na eneo linaweza wekewa mazingira tu suit entry and exit ya kumudu foleni za baadae ata mji ukikuwa na tena kuna investor ambaye yuko tayari, ajira ambazo zingepatikana kwa wadau maana dar is congested surely bagamoyo ingekuwa sababu ya kulitanua jij la Dar ambalo kwa sasa lipokea malaki ya economic migrants kila mwaka.

Kuna vitu vingine maamuzi anayaelewa anaenua mwenyewe lakini sio duniani nzima hili ni moja wapo ina maana awaoni location wise tu bandari ya Dar sio sawa kwa volume inazobeba sehemu na sio sahihi kwa jiji leo.
 
Last edited:
Huu ni mradi mzuri kuuelezea lakini kivitendo una maswali na nadhani JPM kajiuliza hayo maswali na hakupata majibu.
Unaongelea Bagamoyo kutokuwa na foleni lakini ukumbuke pia hakuna barabara za kuiunganisha hiyo bandari hivyo itatakiwa kujengwa reli, barabara za kisasa na mioundombinu mingine.
Dar es salaam wanasema karibia 80% ya mji umejengwa bila kupimwa, kwa maana hiyo wakifanya overhaul na kurudisha master plan ya mji na kujenga 50% tu ya highways/barabara kama inavyotakiwa naamini foleni zitapungua kwa 90%. Kwa maana hiyo hizo foleni za kuanzia uwanja wa taifa unaweza ukashangaa zinapote.
Alafu kuna kitu ambacho wengi hatukisemi hapa, hiyo Bagamoyo wanasema ni 'wawekezaji' lakini kwa upande wa pili wanatukopesha hizo pesa na mikataba yake wengi mnajua ilikuwa na usiri kiasi gani! Maeneo asilia ya bandari ya Dar es Salaam yanajulikana lakini pia yamevamiwa na wnaojiita 'wawekezaji' na kujenga ICDs ambazo zinafanya kazi hizo hizo za bandari! Sasa ukipinga hasara ya mkopo wa kujenga Bagamoyo na kulinganisha na gharama za kuwafidia na kuwahamisha 'majirani' wa bandara ya Dar es Salaam kuanzia Mivinjeni mpaka Mtoni ni wazi itakuwa ni gharama kubwa lakini bado zitakuwa ni kidogo mno kulinganisha na hii mikopo tata yenye masharti ya kuuana.
 
we mtu unafikiri. safi sana.
 
Kuna aliyesema mtwara inafaa kwa hilo na ina kina kirefu cha maji.
 
Kama tuboresha bandari ya mtwara, vipi bandari ya dangote
 



Kwa sababu ni linaandikwa kwa kiingereza? The Citizen ni Mwnanchi Kampuni ile ile falsafa ile, ila kwa kuwa wameandika Kiingereza basi unaamaini lkn kama Mwananchi wangeandika usingeamini, kweli sisi Waafrika ni zaidi ya utujuavyo!
 
Bandari ya mwaa kivyake na ile kivyake.

Habari imekaaa kiudaku zaidi na siwezi kuishadidia mpaka nione tamko rasmi la serikali.

Strategically Bagamoyo Port ni better kuliko Dar.
Na tukishajenga bagamoyo bandari ya dar ipelekwe wapi?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…