Serikali yasitisha Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Kuimarisha Bandari za Mtwara, Dar

Status
Not open for further replies.
Kwanini hakupotoshwa kwenye Wezi wa Makontena
Kwa kuwa ametumia vyombo sahihi vya ushauri....
Mkuu hoja ni utata wa mkataba?
 
Bandari za Mtwara na Tanga zikiimarishwa itapunguza mzigo kwa bandari ya Dar kwa kiwango kikubwa ....pia plan ya kujenga bandari kavu kubwa sana Chalinze pamoja na reli kutoka Bandarini Dar hadi hapo Bandari kavu Chalinze itaondoa kero ya foleni maana mizigo yote ya mikoani na nchi jirani itapelekwa kwa reli Chalinze ...ni mpango mzuri sana ukitekelezwa ...
 



Acha kukurupuka Meli kubwa kwa mizigo gani? Hizi white elephants projects ndiyo zinazorudisha Afrika nyuma tunapoteza fedha nyingi kwenye miradi mikubwa ambayo haina tija, kwa uwezo wa Uchumi na wa nchi zilizotuzunguka Bandari zetu tatu kama tukiziboresha na kutengeneza Miundo ya kuunganisha na Mikoani pia na nchi jirani zinatosha kabisa kukidhi soko la letu na la nchi zinazotuzunguka na wala hatuhitaji Mega ports ya mega ships kwa maana hakuna cha kushafirisha!
 
Huo Mkopo wa kujenga bandari ya Bagamoyo utakuwa na 10% za watu ....ni kilio sasa ...
 
Nampongeza Raisi Pombe Magufuli kwa kuliona hili la bandari,sasa namshauri azidi kubana matumizi kwa kupunguza majimbo (Wabunge)hadi kufikia wabunge 200 tu
 
KIONA MBALI!!
BANDARI YA MTWARA IWE MODERNISED KUTOKANA NA KINA CHAKE/ ILI SUPER GIANT SHIP ZIELEKEZWE HAPO/
N.B
****
IWE SPECIAL KWA GIANT SHIP!!
FEDHA HIZO ZA BANDARI YA BAGAMOYO ZIELEKEZWE KATIKA STANDARD GEJI RAILWAY,TUOKOE MABARABARA YETU.
ii
 
Katika moja ya project useless kutokea tz hii ni namba moja.alitaka awalipe fadhila watu wa kwao kwa kuwawekea bandari.
 
I salute the President Hon. Dr. John Joseph Pombe Magufuli, if this post is true infos then this man of the people for now has come to serve tanzanians on the right time! This is the critical decision and I kudos my president.
 
 
Huu mkataba basi utakuwa na walakini mkubwa! Sisi tuliambiwa kuwa tutoe tu ardhi maana wachina wataugharamia 100% kwenye ishu ya funds!
Sasa wakati wakiusitisha Pia waweke wazi vigezo walivyotumia kuuvunja!

Pia ni bora wakafikiria kwenda kujenga bandari mpya ya Tanga kuliko kufikiria kuiboresha bandari ya Dar yenye makosa mengi kiufundi!

Ni vigumu sana Bandari ya Dar kwa hali ilivyo sasa kuweza kuleta ufanisi! Ni lazima kujenga bandari mpya!!!

Kama serikali ya Magufuli ndiyo imewaza huu ujinga wa kuiboresha 'vijibandari' vya Dar Na Mtwara Na kupiga teke wazo la kujenga bandari mpya basi nazidi kuwapa "zero" kwenye falsafa yao ya utendaji! UJENZI WA BANDARI MPYA KUBWA NA YA KISASA haukwepeki!! Hii nchi mbona tunaifanyia majaribio sana?????

Wazo la ujenzi wa Bandari ya Tanga na iwe connected Na reli ya kisasa pamoja na usafiri wa uhakika uwe palepale!!!
Na ile plan ya mji wa kisasa wa Bagamoyo vepee??
 
Last edited:
Ng'wanene ngalo
 
Kwani haimoi kwenye masterplan ,naona mradi huo kama uliwahusu wawekezaji ambao wangelitoa kiasi kikubwa cha fedha au kama kulikuwepo na wafadhili basi sioni sababu ya kuusimamisha ,au wanadhani wafadhili watatoa hela kupeleka katika sehemu wasizokuwa na interest nazo , ,eti kuendeleza bandari ya feri na ile ya Ntwala ,imekula kwao nchi kibao zinatafuta wawekezaji na wafadhili wa miradi mikubwa ,utakuja kusikia tu ule mradi uliokuwa ujengwe bagamoyo sasa unajengwa kando ya kisiwa cha Mombasa au utajengwa maputo,hapa mnasubiri uendelezaji wa soko ya samaki feri na wakulima wa kolosho !
 
Kulikua na tetesi kwamba mwekezaji wa bandari hiyo alikua aiendeshe kwa miaka 40 arudishe gharama zake ndio akabidhi. Kwa vyovyote miaka 40 hatungekua na mapato yahusuyo bandari kwa kuwa bandari ya dar ingebidi isimame ili bagamoyo ifanye kazi. Na kwa vyovyote baada ya miaka 40 tungekabidhiwa bandari iliyochakaa na ingebidi serikali itumie gharama kubwa kuirudisha katika hali yake. Wataalamu wanasema hilo ni 'disaster'.
 
Kwa sababu Bagamoyo ndio karibu zaidi na kitovu cha biashara cha Afrika Mashariki, Dar Es Salaam.

Na hizo nyingine zote si vibaya kuwepo zenye ubora.
Dada acha ushabiki.unafahamu kwamba upande wa kaskazin yaan tanga Kilimanjaro arusha na musomo.karibu robo ya watanzania wanatimia zaid Mombasa.sabab tanga imekufa na wao wako karibu na Mombasa.sasa unaonaje tuboreshe tanga ili watanzania wenzetu wasicross border kama wakenya wanavofanya?.(karibu 100% ya wakenya wanatimia Bandar zao ila watanzania ni kama 70s%)
 
Bandari ya Bagamoyo ni muhimu sana, kama ikijengwa itakuwa ya kisasa zaidi na ambayo ingewezeka kushindana na bandari za dubai na SA-Durban na zinginezo. Kwa kifupi hata nchi hizo zinatolea macho bandari hii ya Bagamoyo kujengwa Tanzania. Kwa mazingira na mahali/location ilipo bandari ya Dar es salaam hata wakijaribu kuupgrade li kuongeza capacity bado haiwezi kutoa ushindani mzuri. Bandari ya dar es salaam haina eneo kubwa, imejibana mahali ilipo, hakuna nafasi ya kutosha, haina hat auwezo wa meli kubwa kutua pale, kama mizigo ikiongezeka jam ni kubwa sana pale na kuathiri wakazi wa mji wa dar. Magufuli kuachana na mradi bandari ya Bagamoyo sio busara, tusifanye vitu kwa kuangalia nchi jirani za kenya, eti kwa kuwa wao wana upgrade sijui mombasa au lamu basi nasisi just to upgrade bandari yetu, ngoja niwaambieni nchi hiyo jirani kama ingelipata bahati ya mradi huo kuwa kwenye nchi yao wasingeaacha, halafu kwa nini tunacompare na nchi masikini kama sisi? kama tunataka tuendelee kwa nini tusiangalie wenzetu dubai au SA bandari zao ziko vipi? ,kuna ubaya gani tukiwa na largest port in Africa? tuache issue za kuwa za kuwa inajengwa wapi, Bagamoyo ni Tanzania, tatizo liko wapi? ,tunaweza tukajenga bandari ya Bagamoyo na tuka upgrade ya dar es salaam, pia zikajengwa hizo bandari za mtwara na tanga, kuna ubaya gani tukiwa na bandari hata kumi? , nchi ya china ina zaidi ya badnari 1000 na zote zinafanya kazi vizuri, leo hii tanzania tunalzimisha miaka zaidi ya 50 kuwa na bandari zile zile, zenye uwezo ulele mbovu na hazina tija, na wakati huo tunalalamikia maendeleo , maendeleo gani hayo? tupende kuwa na largest projects tanzania, mabazo zitatuingizia mapato kwa kasi na haraka. If u want to be the best u must beat the bests, sasa kama tunataka tuwe economic imara nashauri tanzania /watanzania kuacha kujilinganisha na chi kama kenya, uganda, burundi sijui rwanda,..........., tutabaki pale pale, let us beat SA, tutakuwa tumeipiga Africa yote, haya mawazo ya kukataa projects kubwa na nzuri tanzania yanatoka wapi?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…