Clemence Baraka
JF-Expert Member
- Sep 4, 2012
- 1,694
- 650
Eeeh! Kwa hiyo atakua tayari keshapokea zile bl 5 za Mo Ibrahim? Heri yake.Usongo tu na bado mpaka sasa Rais bora wa Tanzania hii ni Kikwete na juzi kachukua tuzo ya Rais bora Afrika, unalijuwa hilo?
True bro. He is a smart guy.seems to be a very smart guy. .nakubaliana na suggestions zako 100 percent..reli ujenge ya standard gauge from Tanga ipite arusha mpaka singida I kutana na reli ya dar -mwanza-kigoma same as ile bandari ya Mtwara
Well said.Huu ni mradi mzuri kuuelezea lakini kivitendo una maswali na nadhani JPM kajiuliza hayo maswali na hakupata majibu.
Unaongelea Bagamoyo kutokuwa na foleni lakini ukumbuke pia hakuna barabara za kuiunganisha hiyo bandari hivyo itatakiwa kujengwa reli, barabara za kisasa na mioundombinu mingine.
Dar es salaam wanasema karibia 80% ya mji umejengwa bila kupimwa, kwa maana hiyo wakifanya overhaul na kurudisha master plan ya mji na kujenga 50% tu ya highways/barabara kama inavyotakiwa naamini foleni zitapungua kwa 90%. Kwa maana hiyo hizo foleni za kuanzia uwanja wa taifa unaweza ukashangaa zinapote.
Alafu kuna kitu ambacho wengi hatukisemi hapa, hiyo Bagamoyo wanasema ni 'wawekezaji' lakini kwa upande wa pili wanatukopesha hizo pesa na mikataba yake wengi mnajua ilikuwa na usiri kiasi gani! Maeneo asilia ya bandari ya Dar es Salaam yanajulikana lakini pia yamevamiwa na wnaojiita 'wawekezaji' na kujenga ICDs ambazo zinafanya kazi hizo hizo za bandari! Sasa ukipinga hasara ya mkopo wa kujenga Bagamoyo na kulinganisha na gharama za kuwafidia na kuwahamisha 'majirani' wa bandara ya Dar es Salaam kuanzia Mivinjeni mpaka Mtoni ni wazi itakuwa ni gharama kubwa lakini bado zitakuwa ni kidogo mno kulinganisha na hii mikopo tata yenye masharti ya kuuana.
Ninadhani ni muhimu hiyo bandari iwe mtwara...sio bagamoyo.....Mtwara narurally ina kina kirefu...Pia kwa maana ya Location imekaa strategically zaidi
Bagamoyo was a waste...watu walikuwa wanajali kwao
Eeeh! Kwa hiyo atakua tayari keshapokea zile bl 5 za Mo Ibrahim? Heri yake.
Tena hawa Citizen na Mwananchi ni wataalam wa habari za kuwekea maneno mdomoni
JK asingeweza kung'ang'ania madaraka alishachoka ubongo!Kuna kinga ya rais kutoshtakiwa, bila hivyo Kwa hali jinsi ilivyokuwa wakati wa kuelekea kwenye uchaguzi Mzee wa msoga angeng'ang'ania madarakani
Bado sijaona hoja au mantiki ya kusitisha(kama habari hii sio udaku)
Kama issue ni fedha...basi tukusanye kodi kwa ajili ya ujenzi wa Bagamoyo port ambayo itakuwa ya kisasa kuliko zote katika pwani ya EAC na pia tukusanye fedha kwa ajili ya kuboresha hizo za MTWARA NA TANGA.
Kwa nini basi tujisifu tunakusanya kodi ikiwa tunaogopa kuwekeza??
Nakumbuka Mkapa alijenga uwanja wa Taifa mpya pembeni tu ya uwanja wa Uhuru ambao nao uliboreshwa na sikusikia mtu akisema Uwanja huo ukajengwe Mtwara au Moshi.
Katika mradi mkubwa uliokuwa wa kushangaza kabisa kwa serikali iliyopita basi ilikuwa huo wa bandari ya bagamoyo,hapakuwa na sababu ya msingi kuweka bandari moja umbali wa takribani km 40 tu ndani ya bahari bagamoyo mpaka Dar,pesa iliyotengwa kwa mradi huo ilikuwa kubwa nyingi sana,pesa hiyo inatosha kabisa kufufua bandari ambazo tayari tunazo Mtwara na Tanga,ukitazama Tanga na Mtwara tayari miundo mbinu ilishakuwepo toka miaka hiyo,inatakiwa sasa kuboreshwa tu,
mpaka sasa najiuliza washauri wa huu mradi walitumia vigezo gani kuweka bandari hiyo bagamoyo?
nadhani wahandisi wa huu mradi wanattakiwa washtakiwe wote kwa ujinga na upuuzi na ushauri wa hovyo kabisa
Tatizo ni mkataba uliongiwa ambao ungeuwa bandari ya DSM, pia mkataba unapoisha tungepewa bandari kama chuma chakavu, so hili ni tatizo sana....kungekuwa na goodwill isingevunjwa lakini 10% ndo imesumbua, Magu sio Kwamba anakurupuka Bali amekuwa well informed, ukiiboresha bandari ya Mtwara hicho unachosema kitatokea, haiwezekani ndani ya wizara moja kuwe na competition yani ndani ya 130km uwe na bandari wakati hii iliyopo haijaboreshwa, only MP Lusinde can prove this projectBandari ya Bagamoyo ni muhimu sana, kama ikijengwa itakuwa ya kisasa zaidi na ambayo ingewezeka kushindana na bandari za dubai na SA-Durban na zinginezo. Kwa kifupi hata nchi hizo zinatolea macho bandari hii ya Bagamoyo kujengwa Tanzania. Kwa mazingira na mahali/location ilipo bandari ya Dar es salaam hata wakijaribu kuupgrade li kuongeza capacity bado haiwezi kutoa ushindani mzuri. Bandari ya dar es salaam haina eneo kubwa, imejibana mahali ilipo, hakuna nafasi ya kutosha, haina hat auwezo wa meli kubwa kutua pale, kama mizigo ikiongezeka jam ni kubwa sana pale na kuathiri wakazi wa mji wa dar. Magufuli kuachana na mradi bandari ya Bagamoyo sio busara, tusifanye vitu kwa kuangalia nchi jirani za kenya, eti kwa kuwa wao wana upgrade sijui mombasa au lamu basi nasisi just to upgrade bandari yetu, ngoja niwaambieni nchi hiyo jirani kama ingelipata bahati ya mradi huo kuwa kwenye nchi yao wasingeaacha, halafu kwa nini tunacompare na nchi masikini kama sisi? kama tunataka tuendelee kwa nini tusiangalie wenzetu dubai au SA bandari zao ziko vipi? ,kuna ubaya gani tukiwa na largest port in Africa? tuache issue za kuwa za kuwa inajengwa wapi, Bagamoyo ni Tanzania, tatizo liko wapi? ,tunaweza tukajenga bandari ya Bagamoyo na tuka upgrade ya dar es salaam, pia zikajengwa hizo bandari za mtwara na tanga, kuna ubaya gani tukiwa na bandari hata kumi? , nchi ya china ina zaidi ya badnari 1000 na zote zinafanya kazi vizuri, leo hii tanzania tunalzimisha miaka zaidi ya 50 kuwa na bandari zile zile, zenye uwezo ulele mbovu na hazina tija, na wakati huo tunalalamikia maendeleo , maendeleo gani hayo? tupende kuwa na largest projects tanzania, mabazo zitatuingizia mapato kwa kasi na haraka. If u want to be the best u must beat the bests, sasa kama tunataka tuwe economic imara nashauri tanzania /watanzania kuacha kujilinganisha na chi kama kenya, uganda, burundi sijui rwanda,..........., tutabaki pale pale, let us beat SA, tutakuwa tumeipiga Africa yote, haya mawazo ya kukataa projects kubwa na nzuri tanzania yanatoka wapi?
Kwa nini hauna tija mkuu?HI kitu nilijua tu kama ingetokea hivyo; niliwahi pia ku- comment kama sio humu basi kwenye mitandao mingine ya kijamii! Kiuhalisia ule mradi ulikua hauna TIJA yoyote kwa nchi. Thanks Magufuli, kwa hili nakuunga mkono pia.
Nasma Comments huku nikijifariji na SIGNATURE YANGU..................Kwa nini hauna tija mkuu?
Watanzania tuna safari ndefu sana-- siumi maneno, this's MISTAKE! Nitarudia tena na tena, hapa serikali ya Magufuri itakuwa inakosea sana! Bandari ni zaidi ya meli kufunga gati bali container terminals! Bandari zote duniani zinapimwa kwa uwezo wake wa kuhudumia makoentena. Dar es salaam hakuna eneo linaloweza kutufikisha miaka 50 ijayo! Sisi watu wa Kurasini tunaifahamu vizuri hii! Kurasini ya miaka ya 80 sio ya miaka ya 90 na Kurasini ya miaka ya 90 sio ya miaka 2000! Kurasini yote imeisha kwa ajili ya Bandari na sooner or later watahamia Mtoni manake hata Mivinjeni nayo imebaki historia!
Pamoja na Kurasini na Mivinjeni ku-RIP lakini bado bandari ya Dar es salaam haipokei mzigo mwingi wa angalau kulinganisha na Mombasa. Pamoja na Mombasa kupokea mzigo mwingi kuliko sisi lakini nao wameshaona bandari ya Mombasa haitawafikisha miaka 50 ijayo na ndo maana wanaanzisha grand project kule Lamu! Kama lengo la serikali ni kuipanua zaidi bandari ya Dar es salaam basi wafanye declaration kabisa kwamba Temeke yote iwe ni eneo la bandari ya Dar es salaam!!
Kwamba waimarishe bandari ya Mtwara hii ni mistake nyingine! Unless kama tunadanganywa kuhusu gas boom huko Lindi na Mtwara lakini kama ni kweli basi itakuwa taabu sana siku za usoni kuifanya bandari ya Mtwara kuwa multi-purpose... yaani ku-accommodate gas and petroleum shipping lines together with other cargo shipping lines. Sehemu nyingi duniani, bandari zinazo-accomodate meli za mafuta zinakuwa na separate habors coz' ile mimeli ni mikubwa mno!
At least ningewaelewa kama wangesema mradi wanauhamishia Tanga lakini Dar es salaam au Mtwara... hili ni kosa la kiufundi!