Serikali yasitisha Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Kuimarisha Bandari za Mtwara, Dar

Serikali yasitisha Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Kuimarisha Bandari za Mtwara, Dar

Status
Not open for further replies.
Swala la Bandari ya

Tanga mpaka wana Nchi walisha lipwa mwaka 2013 ktkt wahame kupisha upanuzi wa Bandari Tanga,ambayo itakua Bandari kubwa na yakisasa kabisa. Hii Bandari ya Bagamoyo kuna ubinafsi humo ndani take it from me,mwambani Tanga ni eneo pana sana linatosha kabisa kua na Bandari ya ukweli kabisa.


yezakuwa uko right.....je kina cha bandari hii kikoje?
 
Mtwara reli imeshaanza kutandikwa kuanzia kule Mbambabay na watu washapewa NOTICE... Safari hii hatutaki upuuzi wa yule lofa wa Msoga.

Ni kazi tu
 
Last edited by a moderator:
Tunakataa mradi wa 10 M usd? , kama tatizo ni location basi upelekwe tanga, sio kusema tumeachana na huu mradi wa bagamoyo tukarabati tanga na mtwara, mbona tunachekesha, nilitegemea awaite wadau/wahisani wa bagamoyo port wafanye survey tanga na mtwara n bagamoyo then wachague wenyewe kimya kimya then waseme kama wamehamisha kwenda sehemu hizo na mradi utaanza mwezi kazaa kama ulivyopangwa , Hakuna nchi duniani kote wanaweza kataa mradi kama huu.
 
I agree with you chief.....but Tanga nako tatizo nadhani ni Kina .....hebu tusubiri wenye data watuambie.....lakini na Bagamoyo je kina kinatosha?
 
Last edited by a moderator:
Hapa sawa. Na aliyetoa amri ya kujengwa bandari hiyo ashitakiwe kwa matumizi mabaya ya ofisi na ubadhirifu wa mali ya umma. fedha nyingi sana ya walipa kodi imeshapotea kwenye ujinga huo.

Naanza kuona sababu za wageni wanafiki kutokukauka kwa Magufuli.
Mradi haukuwa na tija

ina maana haukufanyiwa upembuzi yakinifu kabla? au mambo ya cha juu?
 
Mambo mengi yanagundulika kuwa yalikwenda ndivyo sivyo! Mfano mzuri, upatikanaji wa waendesha mradi wa DART! Si ajabu na hiyo project ya bwagamoyo ilifanyizwa ndivyo sivyo.
 
Habar

Habari ina ukweli kabisa, soma The Citizen, huwa gazeti hili hawaongei mambo ya mitaani.
Serikali Awamu ya Nne inaelekea ilitumia vigezo visivyoeleweka vyema katika sekta nzima ya usafirishaji, hususan bandari.
Bagamoyo haina hata reli ya kuunga bandarini, jipu hilo!

Serikali awamu ya nne ilikuwa na vigezo vizuri sana kuweka banadari hapo, habari inaweza kuwa ina ukweli lakini haijakamilika.
 
Post yako ipo very brief, please tuwekee habari kamili hapa twaweza kujifunza jambo na kuchangia vema kutokana na maelezo kamili yaliyotolewa na msitishaji
 
Kujengwa banadari mpya na ya kisasa kupisha bandari ya dar ambayo haina nafasi ni uharibifu?

Hakika shule mlienda kusomea ujinga.

Hiyo Bandari ya kisasa ilishindwa kujengwa Tanga au Mtwara mpaka tukaanze moja Bagamoyo??

Yaani hiyo Trillion 22 ingegawia 11 kwa 11 zikawekwa Mtwara na Tanga ingekua ni bonge la Investment kuliko hiyo yote kuwekwa Bagamoyo...
 
Ndiyo maana Mkapa na Jk safari zao hazikauki ikulu na benja nae anataka Dr Magufuli amwajiri pumbaffffd
 
Hivi unajua miaka 30 iliyopita pale ulipojengwa uwanja wa ndege Dar es Salaam palikuwa nje ya mji!?
Je, unajua miaka ya 1980s wakati inajengwa barabara ya 'kisasa' Port Access/Mandela Rd ilikuwa inapitia nje ya mji kuelekea bandarini!?
Na je, unadhani hao 'economic immigrants' ndio wataenda Bagamoyo alafu bandari iwafuate au wataifuta bandari huko!?
Ngoja nifuatilie miji mingine kwenye google na jinsi bandari zake zilivyo located. Nadhani hakuna anayepinga kuzidiwa kwa Dar es Salaam bali wanasema kuiboresha pamoja na Tanga na Mtwara ni faida zaidi kiuchumi badala ya Bagamoyo. Lakini tukumbuke Bagamoyo wanajenga wachina sijui na Oman alafu wanaendesha miaka 50 na hakuna anayejua mkataba unasemaje juu ya extension! Hivyo benefits zake ndio wanaozijua na kwa mwananchi wa kawaida ni sawa na mzee wa Isuna anayeishi kwenye tembe huku akiiona barabara ya rami ikipitisha magari ya kifahari kuelekea Mwanza, Kigari nk.
Sasa mnataka tuwaamini kweli watu ambao wameshindwa kufanya planning za miaka 5 tu kuwa wanaweza ya miaka 50 ijayo!?
Hitimisho ni kuwa titizo la Dar es Salaam ni foleni na Dar es Salaam hakuna barabara. Ukiwekeza trillion mbili kwa miaka mitano kwenye miundombinu ya Dar Es salaam unaweza kupata matokeo yasiyotarajiwa na kusahau hii mriadi tata!
 
Last edited by a moderator:
Tunatakiwa kujenga bandari ya kisasa sio kuboresha wala kukarabati, tunatakiwa tuweke misingi ya maendeleo na plan za muda mrefu zaidi ya miaka 100, siio kila ya baada ya miaka 10 tunakarabati , tuamue moja, sio kuachana na bandari ya bagamoyo eti tunakwenda kukarabati mtwara na tanga, kwa hiyo magufuli aseme bandari ya bagamoyo kuhamishiwa tanga au mtwara na ujenzi wake kuanza ifikapo june. Tunakarabati nini, mabanda ya dar, mtwara na tanga na kuziita bandari?, tunakataa bagamoyo port , bandari ya kisasa tunakibmilia kukarabati?
Poleni sana. Kutumbuliwa majipu kuko kwa aina tofauti tofauti. Kama mna majipu mengine ya aina hii yatapasuliwa moja baada ya jingine. Jiandaeni tu. Maumivu bila shaka ni makali. Na kwa Ushauri tu ile barabara inayoelekea Msoga mjitahidi kuitunza kwa maono yangu ikiharibika haitakarabatiwa kwa vile haifaidishi wengi.
 
The Construction of the 10 billion (about Sh22 trillion) Bagamoyo Port has been suspended, The Citizen has learnt. The government wants to focus instead, on improving the capacity, performance and efficiency of the Mtwara and Dar es Salaam ports.

The Minister for Works, Transport and Communications, Prof. Makame Mbarawa, confirmed yesterday that the construction of what would be the largest port in Africa has been suspended, not shelved to pave way for upgrading berths 13 and 14 as well as developing the Mtwara Port depending on the availability of Funds. The activities would take years to complete, the minister said because the process has to start from finding funding.


Hii yote inatokana na mtu mmoja kutopenda kusugua kichwa chake kwa faida ya watu wake badala yake anawaamini zaidi wapiga deal ndiyo waamue kila jambo kwa manufaa yao binafsi, ni dhahiri kuna mambo mengi sana yanatakiwa kuwa reviewed, na pia matokeo yake yawekwe wazi ili wananchi wote wajue mbinu chafu zinazotumiwa na watu wasio waadilifu katika kulihujumu taifa lao, vinginevyo watanzania na vizazi vyao watakuja umia sana mbele ya safari
 
Hii yote inatokana na mtu mmoja kutopenda kusugua kichwa chake kwa faida ya watu wake badala yake anawaamini zaidi wapiga deal ndiyo waamue kila jambo kwa manufaa yao binafsi, ni dhahiri kuna mambo mengi sana yanatakiwa kuwa reviewed, na pia matokeo yake yawekwe wazi ili wananchi wote wajue mbinu chafu zinazotumiwa na watu wasio waadilifu katika kulihujumu taifa lao, vinginevyo watanzania na vizazi vyao watakuja umia sana mbele ya safari
 
Lowassa aliyasema haya mkasema "anajinyea", kumbe wapo waliokuwa wanajinyea kifikra!

Allen unategemea jambo kutoka kwa watu wa bagamoyo??

Hujui kwanini wazungu wengi walikuwa wanawaua wazaramo kwasababu walikuwa hawana akili
 
Hii habari si nzuri kwa taifa.For short sighted people wataliona hili jambo ni zuri lakini kwa siku za mbeleni tutajikuta hatuwezi kuhimili ushindani katika usafirishaji kwa njia ya maji.

Nikiangalia ujenzi wa Bandari ya Lamu,Kenya,na ujio wa hii habari basi Tanzania kama nchi tujiandae kukosa fursa ambazo wenzetu wemezichungulia na kuzibaini.Kuna mdau hapo juu amezungumzia generation mpya ya meli za mizigo ambazo sidhani kama bandari zetu zitahimili.

Mfano mwengine ni Bagamoyo EPZ ambayo kimsingi imekufa.Unajua ingeweza kutengeneza ajira kiasi haki?Tutaishia import reliant mpaka lini?
 
hata mimi sikuona tija yoyote yaani bandari zetu zimejipanga vizuri sana kwa mtwara ni kwa kusini na na nchi kama malawi zambia wangweza kutumia halafu dar nchi kama uganda,burundi rwanda ingekuwa fursa na tanga tungweza kutumia eneo lote la kasakazini
sasa hii ya Bagamoyo haikua na mashiko tuuacha mji wa kihistoria na tuitangaza mbuga ya saadan kama kivutio adimu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom