Serikali yasitisha Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Kuimarisha Bandari za Mtwara, Dar

Serikali yasitisha Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Kuimarisha Bandari za Mtwara, Dar

Status
Not open for further replies.
Hicho ndio kilimpeleka JK ikulu juzi, thanx Magufuli

Na maamuzi ya Magufuli juu ya kufuta mkataba huo ndiyo yalimfanya Mkapa na Warioba jana waende kwa Magufuli kwa furaha kubwa na bashasha kumpongeza kwa jinsi anavyoingoza serikali yake (ikiwemo kutokubali kuelekezwa na Mkwere)
 
Last edited:
Nakatishwa tamaa sana ninapoona hoja dhaifu kutoka kwa wasomi kama nyinyi,sasa hao wasiobahatika kwenda shule sijui wako ktk hali gani kiupeo?Dr Magufuli yupo sahihi kabisa kuusimamisha mradi wa bandari ya Bagamoyo,bandari ya Bagamoyo ikikamilika itakuwa chini ya China kwa miaka 40,ndani ya muda huu bandari zetu zitaathirika sana kimapato kwasababu nina uhakika wateja karibu wote wa bandari ya Dar watahamia Bagamoyo kwasababu ya ukubwa wake,mbaya zaidi mapato yote ya bandari ya Bagamoyo yataenda China, Sisi tutaambulia vijikodi tu, wakati bandari zetu wenyewe zinazotuingizia mapato kwa 100% zikijifia,huo mkataba wa ujenzi ya bandari ya Bagamoyo ni bomu linalosubiri kutulipukia,bora Magufuli ameanza kulishughulikia male a.
Kimweri,

Kuhusu possibility ya Magufuli kuja ku-ruin uchumi wetu endapo ataendelea hivi nakubaliana na wewe na kuna mtu nilishawahi kumwambia all you need to agree with everything kwa haya yanayoendelea ni your preferred management style. Kama management style yako ni ile ya kuhakikisha mtu yupo kwenye kiti chake ofisini na hata akienda kunywa maji anaenda kwa kukimbia basi lazima leo hii aone Magufuli anatupeleka nchi ya Ahadi!

Yaani kabisa kuna wengine wanasema eti bandari zote hizo za nini huku akisahau kwamba moja ya sababu ya kwanini Dar inapokea mzigo mdogo kuliko Mombasa ni kwa sababu hata hao walaji na wauzaji wa ku-attract mzigo mkubwa Dar es salaam hawapo!! Yaani watu hawafahamu kwamba ni umasikini wetu ndio unaofanya bandari ya Dar es salaam ionekane inatosha!
 
...ktk ushindani wa biashara ya bandari, tutakabiliana vp na bandari za lamu, mombasa, durban, na hata djibout? Hizi bandari zetu zina uwezo wa kuhudumia 3G, na 4G sea vessel, ambazo lamu port inaandaliwa kuziuhudumia? Tutahimili ushindani wa biashara ya bandari unakuwa? Tunatembea wakati wenzetu wanakimbia!
Kwa hiyo unataka kusemaje? Rwanda hawana bandari mbona wao wanakimbia?
 
Kuna Mtu anaongelea mambo ya 3G na 4G ambazo bandari za wenzetu zinalenga kuanzisha na hivyo kama nimemuelewa vizuri anasema tutashindwa kuingia katika ushindani na bandari za wenzetu. Swali langu ni Je, bandari za Dar, Tanga na Mtwara haziwezi kuboreshwa na kuingizwa hiyo mifumo ya 3G na 4G? (kama ni mifumo/technolojia anyway). Au hili lingewezekana tu kwa kujenga bandari ya Bagamoyo. Ni maoni yangu kuwa serikali imefanya tathimini ya kutosha juu ya hasara na faida za ujenzi wa bandari mpya kwa sasa kabla ya kufikia hatua iliyochukuliwa ya kusitisha ujenzi huo. Hivyo binafsi napongeza uamuzi uliochukuliwa na serikali wa kusitisha mradi huo.

nadhani muda muafaka umefika kwa sisi kama nchi kujua ya kuwa competition huegemea zaidi katika huduma na charges hivyo,kama bandari zetu zitapanuliwa vyema na kuwa na uwezo mkubwa zaidi hata kihuduma..tuna fursa kubwa kama nchi kibandari hasa kutokana jiografia ya nchi yetu...........

Anaebeza potentual ya bandari ya tanga inabidi akapimwe akili maana mzozo wa kuiendeleza kwa ajili ya majirani zetu haujaanza leo hivyo,kulipatia tiba ni fursa kubwa katika uchumi wetu........

Imefika hatua sasa miji mingine inabidi kuendelezwa pia ili kupunguza misongamano katika majiji na hata kufufua fursa za ajira..kuna hasara kubwa sana kwa nchi yetu kupumua kwa ajili ya dar na wakati kuna mikoa mingineyo yenye fursa kubwa zaidi za kiuchumi.
 
Bomba la gesi toka Ntwara nalo pia jipu.
 
Hapa sawa. Na aliyetoa amri ya kujengwa bandari hiyo ashitakiwe kwa matumizi mabaya ya ofisi na ubadhirifu wa mali ya umma. fedha nyingi sana ya walipa kodi imeshapotea kwenye ujinga huo.

Naanza kuona sababu za wageni wanafiki kutokukauka kwa Magufuli.
Wewe hivi umesoma kilicho andikwa? washitakiwe kwa lipi? Unaumwa?
 
Kuna wanafiki humu ndani waliwahi kutoa macho hapa jf, cjui watajifichia wapi kama habari hii ni ya kweli. Ukwel ni kwamba me naamin viongoz weng bado hawajafaham mambo ya serkal iliyopita, wakiyajua watajilaum kuwafukuza kaz watu, ambao pengine ni innocent kabisa, kwa vile tu walitekeleza maagizo.
 
Aaaaaaaaahhhhhh BAGAMOYO PAJENGWE BANDARI YA NCHI KAVU SIO USANII HUO,
 
Bandari za Mtwara na Tanga zikiimarishwa itapunguza mzigo kwa bandari ya Dar kwa kiwango kikubwa ....pia plan ya kujenga bandari kavu kubwa sana Chalinze pamoja na reli kutoka Bandarini Dar hadi hapo Bandari kavu Chalinze itaondoa kero ya foleni maana mizigo yote ya mikoani na nchi jirani itapelekwa kwa reli Chalinze ...ni mpango mzuri sana ukitekelezwa ...
Well put! Hili wengi ndil o hawapendi kulielewa kwamba msongamano wa Dar Port ni wa kujitakia wa kuifanya bandari ni sehemu ya kuweka makontena na kuua reli ambayo ingeweza kupeleka makontena kwenye Dry Port ya Chalinze ambayo pia ingefanya Chalinze iwe na mambo mengine ya uchumi ya kufanya kuliko kuuza mananasi. Hii ina faida kwa JK pia . Ukifanya hivyo kuna faida 3 muhimu: Ya kwanza ,Kusitisha malori makubwa yanayosomba transit goods kuja jijini Dar na kupunguza msongamano jijini Dar; pili, kutofautisha mizigo ya transit na ile ya Tanzania ambayo ingebaki Bandarini Dar. Kwa kuiteremsha sehemu tofauti kwa hiyo kurahisisha kazi ya TRA. Tatu, pale Chalinze kungetengwa sehemu mahsusi ya kupanga mizigo ya kila nchi: Malawi, Zambia, DRC, Rwanda na Burundi jambo ambalo lingerahisisha utoaji mizigo kwenda kwenye nchi husika.
Najua waliowekeza kwenye ICDs hapa Dar ndiyo wanawa"pofusha" wenye maamuzi wasione wazo hili jema la Chalinze kuwa Dry port. Hata hivyo siku moja wataona hili kwa maana Mwenyezi Mungu nyakati nyingine huingilia kati kwa niaba ya wanyonge. God sometimes intervenes on the behalf of the poor!
 
Halipwi mtu hapa! Wakabane na waliowadanganya. Isitoshe watu walilalamika kuhusiana na hiki Mzee wa Msoga akapuuza sasa ni juu yake. Bagamoyo ziendelee kujengwa hotel za kitalii kukuza sekta ya kitalii na pengine kujenga airport ndogo kwa ajili hiyo. Haya mbona hayachukui akili nyingi ni uthubutu sisi ni siasa na ubinafsi tuuuuu kila mahali
 
Tusifikiri wachina hawana data za Tanga , mtwara na dar, na msifikiri wao ni wanjinga kuchagua kujenga Bagamoyo, wamefanya survey kote huko. Mradi kama huu wa Bagamoyo port nagufuli alitakiwa awe makini sana kabla hajafuta, tuacheni ushabiki, hizi bandari zetu tulizonazo bado sana, sasa isiwe watu wana miradi yao kule Tanga/ mtwara then wakashawishi kufuta bandari ya Bagamoyo ambayo ingelijengwa kisasa zaidi, hayo mambo ndo yamekuwa yakifanya tanzania tusiendelee. Lazima tujifunze ushindani.
 
The Construction of the 10 billion (about Sh22 trillion) Bagamoyo Port has been suspended, The Citizen has learnt. The government wants to focus instead, on improving the capacity, performance and efficiency of the Mtwara and Dar es Salaam ports.

The Minister for Works, Transport and Communications, Prof. Makame Mbarawa, confirmed yesterday that the construction of what would be the largest port in Africa has been suspended, not shelved to pave way for upgrading berths 13 and 14 as well as developing the Mtwara Port depending on the availability of Funds. The activities would take years to complete, the minister said because the process has to start from finding funding.
Ni maamuzi ya busara Sana.


Source: THE CITIZEN
View attachment 315504
 
Bandari zilizopo zipanuliwe ili kukidhi haja ya meli kubwa kwakua ni upuuzi kujenga bandari mpy wakati hata zilizoko zinatushinda, "a bird in hand worth two in the bush."
 
Aiiibu kwa wabunge wa Ccm, tutakumbuka bunge lililopita hii issue wabunge wa upinzani walikataa. Na kushauri ziimarishwe bandari ya Dar na Mtwara, lakini mipasho ilitawala, vijembe vikawa ndio uchangiaji wa wabunge wa Ccm.
Sasa kuna viongozi wenye akili wamekubaliana na mawazo ya walio ona mbali.
Next time wabunge wa Ccm msijitoe ufahamu changieni mada kwa maslahi ya Taifa
 
Hivi unajua miaka 30 iliyopita pale ulipojengwa uwanja wa ndege Dar es Salaam palikuwa nje ya mji!?
Je, unajua miaka ya 1980s wakati inajengwa barabara ya 'kisasa' Port Access/Mandela Rd ilikuwa inapitia nje ya mji kuelekea bandarini!?
Na je, unadhani hao 'economic immigrants' ndio wataenda Bagamoyo alafu bandari iwafuate au wataifuta bandari huko!?
Ngoja nifuatilie miji mingine kwenye google na jinsi bandari zake zilivyo located. Nadhani hakuna anayepinga kuzidiwa kwa Dar es Salaam bali wanasema kuiboresha pamoja na Tanga na Mtwara ni faida zaidi kiuchumi badala ya Bagamoyo. Lakini tukumbuke Bagamoyo wanajenga wachina sijui na Oman alafu wanaendesha miaka 50 na hakuna anayejua mkataba unasemaje juu ya extension! Hivyo benefits zake ndio wanaozijua na kwa mwananchi wa kawaida ni sawa na mzee wa Isuna anayeishi kwenye tembe huku akiiona barabara ya rami ikipitisha magari ya kifahari kuelekea Mwanza, Kigari nk.
Sasa mnataka tuwaamini kweli watu ambao wameshindwa kufanya planning za miaka 5 tu kuwa wanaweza ya miaka 50 ijayo!?
Hitimisho ni kuwa titizo la Dar es Salaam ni foleni na Dar es Salaam hakuna barabara. Ukiwekeza trillion mbili kwa miaka mitano kwenye miundombinu ya Dar Es salaam unaweza kupata matokeo yasiyotarajiwa na kusahau hii mriadi tata!

Si ndio kukariri kwenyewe huku sasa tatizo liko wapi hivi dunia ya leo hela usipopata kwa Mchina, Mwarabu na mzungu nani mwingine anawekeza africa in infrastructure or putting physical investment zaidi yao hao watu wngine wakija ni kuvuna tu na kuondoka matter of fact China is the biggest investor by far in Afrika na miradi mingi ni dizaini hizi.

Unapozungumza investment za $10b kwa nchi maskini swala sio time frame only
Issue ni hizi what do you loose ukikataa; Hujui mwingine atakuja lini, kwa hivyo ni kupoteza mapato, ata mwingine akija hadi mradi ukianza tayari shillingi ngapi ushapoteza za mapato na ukuaji wa uchumi wa taifa kutokana kuikataa bandari ya kiwango, faida hiyo ungekuwa umefanya vitu vingapi vingine vya uzalishaji na vingewainua watu wangapi wengine, risk ujui mwingine atakuja na mkataba gani maana auna hata offer on the table and the list can go on and on why it is not a good dead at all under the national circumstances wakati mradi pekee unafaida kuliko hasara mzungu sasa hivi anakupigia future cost za kukataa mkataba in NPV unaweza kukuta umepoteza zaidi ya trillions of same amount in investment capital in five years kutokana na fiada zingine za uwepo wa mradi kisa uoni.kwa sababu ya upro mdogo wa kufikiri mambo haya yanawezekana afrika tu kufanya vitu bila kufikiria au kuzingatia angle zote za appraisal and weighing losses of investment risk kwa jamii kwa ukosekanaji wake.

Halafu nani kakwambia location ya sehemu unaamuwa kwa google au historical facts maswala ya social geography na inner city issues we unaleta habari za google kama ingekuwa uwepo wa bandari mjini hakuna tatizo mbona magari yaliyoyukuwa yanaingia na kutoka muda wowote siku hizi ni marufuku mchana je unadhani na port ingekuwa bagamoyo kungekua na restrictions hizo ukipata jibu
 
Last edited:
kati ya jambo la kishenzi kufanywa na serikali iliyopita hili ni namba moja ,nashukuru serikali hii imelitupilia mbali ,tunasubiri mikataba ya gas na mafuta maana huko nako kutakua na ukuda mwingi tu
 
Nakatishwa tamaa sana ninapoona hoja dhaifu kutoka kwa wasomi kama nyinyi,sasa hao wasiobahatika kwenda shule sijui wako ktk hali gani kiupeo?Dr Magufuli yupo sahihi kabisa kuusimamisha mradi wa bandari ya Bagamoyo,bandari ya Bagamoyo ikikamilika itakuwa chini ya China kwa miaka 40,ndani ya muda huu bandari zetu zitaathirika sana kimapato kwasababu nina uhakika wateja karibu wote wa bandari ya Dar watahamia Bagamoyo kwasababu ya ukubwa wake,mbaya zaidi mapato yote ya bandari ya Bagamoyo yataenda China, Sisi tutaambulia vijikodi tu, wakati bandari zetu wenyewe zinazotuingizia mapato kwa 100% zikijifia,huo mkataba wa ujenzi ya bandari ya Bagamoyo ni bomu linalosubiri kutulipukia,bora Magufuli
Kuna Mdau mmoja hapa nimemuuliza hayo mapato yote ni mapato yapi lakini hajanijibu labda nisaidie wewe kunipa darasa!!

Can I tell you something?! I am afraid ikiwa kweli unalifahamu vizuri hili suala kwa jinsi issue ya kodi ulivyoita vikodi!!

Guys, pesa nyingi bandarini inachukuliwa na TRA na sio TPA!! Na mapato ya TRA yanaongezeka kadri mzigo unaopitia bandarini unavyoongezeka; keeping other factors constant! Pesa inayoingia bandari ni ndogo sana ukilinganisha na inayoenda TRA! Na kv bandari ya Dar hawana eneo kubwa kimapato ndo wanaathirika zaidi na ndio maana sehemu kubwa ya mzigo unahifadhiwa na Privately owned ICDs!

Kule Bagamoyo, hata kama bandari itakuwa funded na Wachina kwa 100%; mapato/kodi za TRA through imports and export Mchina hazigusi kwahiyo ndo maana umenishangaza unaposema vikodi unless kama unamaanisha kodi zitazolipwa na Wachina wenyewe! Ikiwa bandari itakuwa na uwezo wa kupitisha mzigo mara 3 ya sasa, maana ake ni kwamba hata mapato ya TRA yatapanda kwa similar proportionality!

Halafu nitarudia tena kwako!! Bandari 3 au 4 sio nyingi kama mnavyodhani.... kwa sasa zinaweza kuonekana nyingi kv we don't produce so we don't export! Likewise, our purchasing power ni ndogo so we don't import much! Kwahiyo mnaweza kudhani bandari ni nyingi kumbe msingi wake ni bandari kutumiwa na nchi maskini! Leo hii uki-import smart tv milioni moja zitakudodea but assume nchi zinazutumia bandari ya Dar zinakuwa kiuchumi angalau mara tu na hivyo kuongea exports na purchasing power ya imported goods.... hivi bado hapo unaamini Dar port itakuwa abandoned kwa kukosa mzigo?!
 
Wadau ...kuna watu wameshaunguza fedha kuvizia bandari mpya ya Bagamoyo hivyo msishangae watu kutokwa povu ....kwanini lazima iwe Bagamoyo na si Mtwara wala Tanga?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom