kalacha mateo
Senior Member
- Sep 27, 2021
- 119
- 240
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa imesema katika kuhakikisha maslahi ya watanzania yanalindwa katika mkataba umeweka vifungu muhimu vinavyolinda ajira za watanzania, Haki za ardhi ya raia, ukomo wa mkataba mahsusi pamoja na masuala yote ya ulinzi na usalama.
Aidha serikali imeweka bayana kuwa wakati wa utekelezaji wa mikataba hiyo ambayo ni;
1. Mikataba itakayoandaliwa itawekwa bayana kipindi cha utekelezaji wake na ukomo wake.
2. Muda wa marejeo ya mikataba hiyo itakua kati ya mwaka mmoja, miwili, mitatu hadi mitano kutegemea na ukubwa wa mikataba hiyo.
3. Viashiria muhimu vya utendaji yaan "Key Performance Indicator" vitaainishwa kwa kila mkataba
4. Uandaaji wa mikataba utafanyika chini ya ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
5.Mikataba itakayoandaliwa italinda ajira za wafanyakazi wazawa pamoja na kuwajengea uwezo
6. Mifumo yote ya TEHAMA itakayosimikwa itasomana na mifumo ya serikali
7. Taasisi mahsusi za serikali zitaendelea na utendaji wake katika maeneo ya bandari.
8.Muwekezaji kuchukua hatua stahiki za masuala ya utafiti wa masoko ya bandari ya Dar es Salaam.