We jamaa unalalamika sana aisee sijui unataka serikali ikufanyie nini sasa
Hakuna ulazima wa wewe kuingiza taarifa za kufundisha kama hujawahi kufundisha na zipo options zote kama hujawahi kufundisha/ kujitolea unaachana na kipengere hicho unaendelea na taarifa zingine mbona ipo wazi tu hiyo?
Hizo barua za kufundisha ni barua ambazo unathibitishwa na mkuu wako wa kituo ulicho kuwa ukijitolea/ukifundisha na ikowezekana ofisa elimu kata waipitishe kuthibitisha huko kujitolea kwako
sasa sijui unalalama unatakaje, ? Sasa wewe utasema ulifundisha sawa kielelezo kwamba ulifindisha ni kipi? We hutaki kiulizwe? Watajiridhishaje kwamba usha wahi fundisha au wataota kwenye ndoto?
Na ukiona shule haipo kwenye list maana yake haipo kwenye orodha ya shule zenye uhitaji wa walimu sasa ulitaka waiweke ya nini?
We kama una aina yako ya ajira unayo itaka uletewe basi acha kuomba wenye shida wataomba hizi zilizopo. Usije kupotosha watu hapa kwa jambo ambalo linatokana na uelewa wako kuwa mdogo
Yaan hapo unastress za kuto ajiliwa halafu unajiongezea misononeko iso na tija.