Serikali yatangaza ajira za ualimu kwa mwaka 2024 zaidi ya nafasi 11,000

Lakini huu mfumo wa kihuni,kwanini wasiufanye ukawa na uwanda mpana kwa mwombaji kufanya atakacho,sasa mfumo kama nilijisajili nina diploma baadae nikajiendeleza hadi masters unashindwa kunitambua basi kuna shida sehemu.

Wahusika waurekebishe
Unakutambua mkuu,watu wameweka mpaka vyeti vya phd mbona na mfumo unakuruhusu kuomba level zote za degree ata kama huko na masters
Ila hautakuruhusu kuomba nafasi za watu wa diploma na certificate ata kama una diploma na certificate
 
Vijana mna matatizo sana, usahili ndiyo ponapona yenu, ukiachwa unaachwa with tangible reasons siyo watu wanatoa majina tu bila taarifa za kueleweka.
Yani wanataka mfumo wa kupeana ajira kishamba na kwa bahati halafu waanze kumlilia Rais! Kisa wanaogopa usahili
 
Mtu anawezaje kubadilisha documents alizoweka ilia aweke mpya? Mfumo hauna sehemu ya delete
 
Kabisa mkuu. Siyo watu wanalala wanaamka na kuorodhesha majina mengiii afu mengine yamejirudia Kila page. Inaboa hiyo hasa hasa ukiwa haumo kwenye orodha husika.
Vijana mna matatizo sana, usahili ndiyo ponapona yenu, ukiachwa unaachwa with tangible reasons siyo watu wanatoa majina tu bila taarifa za kueleweka.
 
Wakuu msaada ...
Jamaa ali- certify vyeti vyake mwaka 2019 ,,, jee nakala hizo anaweza kuzitumia katika hizi ajira ,,, au anatakiwa aende tena mahakamani aka-certify na upya ili muhuri usije kuonekana wa zamani mno ???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…