Serikali yatoa Tsh. Bilioni 66 Kurekebisha Miundombinu iliyoharibiwa na mvua

Hahahaha! mkuu najaribu kumlinda mleta mada. Unajua haya mambo hayakutakiwa kusemwa nayeye bali akina chawa kama L.M. isipokuwa kama Yohanambatizaji naye amekuwa..
Nimekuelewa Mkuu ila watanzania wengi tunajichanganya sana kwenye matumizi ya lugha! 😀
 
Hahahaha! mkuu najaribu kumlinda mleta mada. Unajua haya mambo hayakutakiwa kusemwa nayeye bali akina chawa kama L.M. isipokuwa kama Yohanambatizaji naye amekuwa..
Nimenukuu Kwenye Source ambao ni Clouds media
 
Rais wa JMT Dr Samia ametoa Jumla ya shilling billion 66 Ili kurekebisha Miundombinu iliyoharibiwa na mvua

Fedha hizo zimegawanywa Kwenye mikoa Yote iliyoathirika

Source: Clouds TV
Anafanya biashara gani Samia. Mbona anatoa hela nyingi sana kusaidoa Wadanganyika?
 
kwa fikra zako mkuu hilo ni tatizo la kutojua kiswahili au wewe ndio umechelewa mjini?
Ndio nimetoka kijijini ili nami nione maisha ya mjini, katika kupitia JF nikakutana na huu uzi, sasa nashindwa kuelewa anaetoa pesa ni mama au serikali?
 
Kazitoa mfukoni mwake
Safi sana,rais kaonesha moyo

Ova
 
Kumbe Samia ni bilioneaaa! Sikujua. Sijui nimwombe???!
 
Rais wa JMT Dr Samia ametoa Jumla ya shilling billion 66 Ili kurekebisha Miundombinu iliyoharibiwa na mvua

Fedha hizo zimegawanywa Kwenye mikoa Yote iliyoathirika

---
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa Bilioni 66 kwa ajili ya kuanza urejeshaji wa miundombinu ya barabara zilizoharibika nchini.

Fedha hizo tayari zimegawanywa kwa mameneja wa TANROADS mikoa yote iliyoathirika kwa ajili ya kufanya kazi kwa haraka usiku na mchana ili kurekebisha kadhia zilizozikumbumba barabara kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini.

Akizungumza Jijini Arusha mara baada ya kukagua Barabara ya Afrika Mashariki (Arusha bypass) iliyoharibiwa na mvua hizo, Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mha. Mohamed Besta amesema kuwa kutokana na udharula huo tayari Rais Samia ametoa fedha za matengenezo ya miundiombinu hiyo ambazo zimeshapelekwa katika Mikoa yote Nchini.

Mhandisi Besta amesema kuwa tayari kazi inaendelea katika maeneo yote nchini na fedha hizo zinaratibiwa na vitengo maalumu vya dharula vilivyopo TANROADS pamoja na ofisi za mikoa.

Ameongeza kuwa kutokana na tathimini iliyofanyika mpaka sasa zaidi ya Shilingi Bilioni 250 zinahitajika kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya Barabara kuu za Mikoa yote Nchini ambazo zimeharibika vibaya kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha sehemu mbalimbali nchini.

Amesema kuwa kuna baadhi ya maeneo kama Kanda ya Ziwa na Nyanda za juu kusini mwa Nchi mvua zimeendelea kunyesha tangu mwezi Oktoba mwaka jana, na sasa unaelekea mwezi wa saba na mvua bado zinaendelea kunyesha.

“Tunamshukuru Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani ametupatia shilingi bilioni 66 ambazo tumezisambaza katika Mikoa yote ambapo mameneja wote wa Mikoa wamepewa kutokana na hali ya dharura ya Mkoa husika’’ ameeleza.

Chanzo: Clouds
Huyo mama tajiri kiasi hicho?
 
"Ametoa",Neno silioendi hili basi yaani.
Huu uchawa wa kujikomba sijui utaisha lini Tanzania
 
Hvi nyie watu mnaodedicate kila kitu kwa Mh Rais hvi mko na akili zenu ama mmekatwa vichwa....kwamba kazama mfukoni mwake kafanya hisani ama mnamaanisha nini???
 
Rais wa JMT Dr Samia ametoa Jumla ya shilling billion 66 Ili kurekebisha Miundombinu iliyoharibiwa na mvua

Fedha hizo zimegawanywa Kwenye mikoa Yote iliyoathirika

---
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa Bilioni 66 kwa ajili ya kuanza urejeshaji wa miundombinu ya barabara zilizoharibika nchini.

Fedha hizo tayari zimegawanywa kwa mameneja wa TANROADS mikoa yote iliyoathirika kwa ajili ya kufanya kazi kwa haraka usiku na mchana ili kurekebisha kadhia zilizozikumbumba barabara kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini.

Akizungumza Jijini Arusha mara baada ya kukagua Barabara ya Afrika Mashariki (Arusha bypass) iliyoharibiwa na mvua hizo, Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mha. Mohamed Besta amesema kuwa kutokana na udharula huo tayari Rais Samia ametoa fedha za matengenezo ya miundiombinu hiyo ambazo zimeshapelekwa katika Mikoa yote Nchini.

Mhandisi Besta amesema kuwa tayari kazi inaendelea katika maeneo yote nchini na fedha hizo zinaratibiwa na vitengo maalumu vya dharula vilivyopo TANROADS pamoja na ofisi za mikoa.

Ameongeza kuwa kutokana na tathimini iliyofanyika mpaka sasa zaidi ya Shilingi Bilioni 250 zinahitajika kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya Barabara kuu za Mikoa yote Nchini ambazo zimeharibika vibaya kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha sehemu mbalimbali nchini.

Amesema kuwa kuna baadhi ya maeneo kama Kanda ya Ziwa na Nyanda za juu kusini mwa Nchi mvua zimeendelea kunyesha tangu mwezi Oktoba mwaka jana, na sasa unaelekea mwezi wa saba na mvua bado zinaendelea kunyesha.

“Tunamshukuru Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani ametupatia shilingi bilioni 66 ambazo tumezisambaza katika Mikoa yote ambapo mameneja wote wa Mikoa wamepewa kutokana na hali ya dharura ya Mkoa husika’’ ameeleza.

Chanzo: Clouds

Raisi hatoe pesa ana idhinisha pesa.
 
Back
Top Bottom